Waziri Bashungwa: Wanafunzi Wapewe Elimu ya Matukio ya Dharura

Waziri Bashungwa: Wanafunzi Wapewe Elimu ya Matukio ya Dharura

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Viongozi na Wasimamizi wa Shule za Serikali na binafsi kutoa elimu kuhusu matukio ya dharura yanayoweza kutokea katika mazingira ya shule ikiwa ni pamoja na elimu juu ya majanga ya moto ambayo yamekuwa yakitokea.

Bashungwa ameeleza hayo leo tarehe 19 Aprili 2024 mara baada ya kuzindua Bweni jipya la Wavulana katika Shule ya Msingi ya Kingereza KARADEA katika Kata ya Bugene Wilaya Karagwe.

“Ujenzi wa Bweni umezingatia masuala ya dharura pia niwaombe hata kama dharura haipo tutengeneze mazingira ya dharura ambayo yatawawezesha kupata elimu kuhusu matukio hayo”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amelipongeza Shirika la KARADEA kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika shule hiyo na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ambazo zimeendelea kuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya Watanzania.

Bashungwa amechangia mabati 100 ambayo yatawezesha ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ili kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunza na kufundishwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule Lenadius Lemingthon amesema Bweni lililozinduliwa lina uwezo wa kulaza wanafunzi 320 na lina mahitaji yote muhimu kwa wanafunzi ikiwemo vyoo, bafu, maeneo ya kufulia pamoja na vifaa vinavyotumika wakati wa dharura.

WhatsApp Image 2024-04-19 at 13.26.03.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-19 at 13.26.04.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-19 at 13.26.04(1).jpeg
 
Jana Mheshimiwa Bashungwa mbunge mwenye sifa rukuki alitufungulia Bweni la shule ya KARADEA yenye capacity ya vitanda 320 waoo. Pamoja hotuba yake nzuri ya kuwaomba walimu wawafundishe watoto namna ya kujikinga na ajari mbalimbali, lakini hilo Bweni peke yake ni ajari unawezaje kuwaweka watoto 320 ndani ya chumba kimoja, licha ya ajari vipi kuhusu kuambukizana magonjwa, na kuibiana. Tunapojenga majengo tuzingatie afya ya watoto wetu.. Pamoja na kutafuta pesa wawekezaji wa sector binafsi tuzingatie ubinadamu wa watu tunaowahudumia.
 
Tatizo lenu wahaya ni ujuaji. Hayo yenu yanayojali utu mbona hamkujenga.??
 
Sifa rukuki haya tumekuelewa endelea na uchawa wako.
 
Daahh tunasikitisha Sana kama nchi viongozi wetu wengi ni vilaza kupindukia
 
Jana Mheshimiwa Bashungwa mbunge mwenye sifa rukuki alitufungulia Bweni la shule ya KARADEA yenye capacity ya vitanda 320 waoo. Pamoja hotuba yake nzuri ya kuwaomba walimu wawafundishe watoto namna ya kujikinga na ajari mbalimbali, lakini hilo Bweni peke yake ni ajari unawezaje kuwaweka watoto 320 ndani ya chumba kimoja, licha ya ajari vipi kuhusu kuambukizana magonjwa, na kuibiana. Tunapojenga majengo tuzingatie afya ya watoto wetu.. Pamoja na kutafuta pesa wawekezaji wa sector binafsi tuzingatie ubinadamu wa watu tunaowahudumia.
Kiwango cha Serikali ni bweni kulaza watoto 80 tu.
 
Back
Top Bottom