KERO Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?

KERO Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Wakati unataka kuunganishiwa huduma ya umeme kama nyumba iko mbali kila nguzo moja ni sh. 515,000/, nguzo ni mali ya shirika, mwananchi ni mteja wa huduma ya umeme kwanini alipie nguzo?

Huu ni uonevu mkubwa sana. Kwanini mwananchi anunue kitu ambacho si mali yake? Mlitegemea bila nguzo mngesambazqje hiyo bidhaa yenu, yaani umeme?

Hii haina logic kabisa. Huku Arumeru hakuna cha kijiji kila eneo hiyo ndiyo bei yake. Serikali ituletee kampuni zingine za kusambaza umeme kuwe na ushindani
 
Shirika linapewa bure hizo nguzo?? Na kama ungependa iwe mali yako kwakuwa unalipia je uko tayari kulipia nguzo mpya kila mara inapotakiwa kubadilishwa?? Vipi kuhusu mita ya umeme nayo si unalipia, uko tayari kulipia kila inapopata hitilafu??
Kujenga miundombinu ya kusambazia umeme ikiwemo na nguzo linapaswa kuwa JUKUMU LA MTOA HUDUMA. Ni kama vile mitandao ya simu inavyofanya inatutoza gharama/bei ya huduma aliyoitoa tu wangekuwa na upuuzi kama wa Taniusiku ina maana tungelipa gharama ya minara au nguzo(kwa kipindi kile ttcl wanatumia nguzo kupitisha nyaya.
Hili la Taniusiku wizi kwa wananchi
 
Yaani kifupi inatakiwa ukilipia gharama zote hizo umeme nao utumie buree kufidia hasara. Tanesco waanze kulipisha baadae sana
Mkuu TANESCO ni zaidi ya TRA. Unamuuzia mteja nguzo, na wakija wateja mwengine zaidi ya 5 wanatumia /wana wasambazia umeme nguzo hiyohiyo uliyo nunua wewe bure, hii imekaa kaa je? Mtu amenunua nguzo yake ni mali yake mwachieni atumie atakavyo na sio kuifanyia biashara kwa wateja wengine.
 
Yote haya alisababisha mama wakati anarithi kiti chake Kwa kulazimisha Tanesco ipandishe bei kutoka 27000 Hadi 321000 ndani ya mita 30 Kwa madai mfu ya kuwa eti hiyo ndiyo bei halisi.kwa Nchi zinazojitambua kama ujerumani na Norway huduma ya umeme Huwa unaungwa Bure na wanaanza kukata kidogokigogo kwenye matumizi Yako ya umeme.mfano kama matumizi Yako Kwa mwezi ni 20000 watakupa umeme wa 15000 Hadi deni linaisha.Nchi zetu zinaongozwa na washamba sana
 
Ni kweli, hata vodacom wanakuuzia huduma ya mawasiliano na bado simu unanunua mwenyewe. Vilevile gesi ya kupikia mtungi unaulipia au siyo?
Mifano yako haiendani na kilichowasilishwa ..

Simu uliyonunua au mtungi ulionunua ukisitishiwa huduma utabaki navyo. Je, TANESCO wanaweza kukuachia nguzo uliyonunua ili uletewe huduma? Jibu ni hapana
 
Ni kweli, hata vodacom wanakuuzia huduma ya mawasiliano na bado simu unanunua mwenyewe. Vilevile gesi ya kupikia mtungi unaulipia au siyo?
Mbona mifano yako haiendani na unachokitetea.
Simu inabaki kuwa ya kwangu naweza kuiuza, same kwa mtungi wa gas wewe nguzo unaweza kuiuza? Mita unaweza kuiuza. Hiyo ni miundombinu yao wanapaswa kuigharamia. Mfano wa simu ni taa unazoweka kwenye nyumba na socket hivyo ndivyo mtu anastahili kununua na ndio maana vinabaki kuwa vya kwake.
 
Ni kweli, hata vodacom wanakuuzia huduma ya mawasiliano na bado simu unanunua mwenyewe. Vilevile gesi ya kupikia mtungi unaulipia au siyo?
Logic hamna, simu inakuwa mali yako 100% hupangiwi. Utanunua vocha tu ila simu unaenda nayo popote nchini.

Mtungi unaununua pia unakuwa wako 100% unaweza safiri nao toka Mwanza hadi Dar na ukaendelea kuutumia. Wewe ni kujaza gas tu.
 
Mbona mifano yako haiendani na unachokitetea.
Simu inabaki kuwa ya kwangu naweza kuiuza, same kwa mtungi wa gas wewe nguzo unaweza kuiuza? Mita unaweza kuiuza. Hiyo ni miundombinu yao wanapaswa kuigharamia. Mfano wa simu ni taa unazoweka kwenye nyumba na socket hivyo ndivyo mtu anastahili kununua na ndio maana vinabaki kuwa vya kwake.
Vipi kuhusu mabomba ya maji yanayoleta maji nyumbani kwako na mita ya maji, hua ni bure pia eeh?? Au unaruhusiwa kuviuza kwakua ulivilipia?
 
Back
Top Bottom