TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

RIP Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi.

Asante Dr kwa salamu za pole kwa Mtanzania mwenzako. Bora wewe sasa hivi ukiugua huko US unatibiwa hospitali za huko ambazo ni bora zaidi kuliko Mwananyamala au Apollo India. Mie nakusifu sana Dr kwa jinsi ulivyozicheza karata zako vyema, ona sasa unajilia pension yako na family kwa raha zako majuu huku ukilipiwa kila kitu na wale waliokuwa wanakutukana na kukubeza. Wewe ulivumilia ukijua kuna siku watajua tuu kuwa wewe ni mashine kubwa.
Anyway,hayo tuyaache sio wakati wake huu ila bado siamini kama haya yametokea pamoja na majaribu mengi kuwazunguka binadamu.
 
RIP Mh Kombani.

Ni ugonjwa gani umemuua?
 

Juzi amekufa MTOI humu baadhi ya CCM walikua washangilia@IBRAHIM MGAYA na kusema MBOWE ametoa kafara
leo nyie mwaumia...?!
tujifunze kubakisha maneno jamani dunia si yetu hii
anavyokashifiwa lowassa na ugonjwa wake leo mbona tunakufa sie wazima
 
RIP mama kombani. Nimekusamehe kosa lako la kuchakachua katiba ya wananchi ili MUNGU aweze kukulaza mahala pema peponi. Amen
 
R.I.P. Mama Celhna. Daima tutakukumbuka kwa upendo, Upole,busara na utu wa kuthamini wenzio na kutopenda makuu na mbwembwe.
 
R.I.P mama na ni ushaur wa bure tu afya ni majaliwa yake mungu na wale wote wanaofhihaki afya za watu wangali hai wapate fundisho hapa
 
Kitu cha ajabu sana, Uzi unazungumzia msiba watu wanaingiza na mitazamo yao.
Muombe mungu sana na wewe usije kuwa mtu ambaye utaanza kuadhibiwa kabla mwili wako haujasitiriwa ndani ya kabri!
Siyo dalili nzuri hata kidogo ukisikia ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga siyo lazima ukatwe panga !!
Dunia inamafundisho mengi sana hakika tukiyazingatia basi kabla ya kuzikwa dua nzuri utakazo zipata kutoka kwa uliyo waacha duniani zitakupunguzia adhabu za kabrini !
Hakika zote ni wa mwenyezimungu na zote tutarejea kwake eeh mwenye zimungu tunakuomba utuepushe na ghiliba za dunia amiin
 
Usiku wa September 24 2015 taarifa ya Majonzi imesambaa na kuwafikia watu kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya Kijamii, Serikali ikathibitisha pia kuhusu msiba wa aliyekuwa-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mama-Celina Kombani-amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani, na amefariki akiwa India ambako alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu
Kuhusu taratibu zinazofatia, nimeipata taarifa kutoka Ofisi za Bunge ambapo inaonesha mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu mpaka Dar es Salaam inafanyika na mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar JumatatuSeptember 28 2015, na baadae msiba utasafirishwa kupelekwa Mahenge Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mazishi.

Marehemu Mama-Celina Kombani-amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na-alikuwa-Waziri-na pia-Mbunge-wa-Jimbo la Ulanga Mashariki.
Kwa picha na maelezo zaidi tembelea MTAA WA HABARI
 
Duh..... poleni sana wanandugu na jamaa wa karibu na Marehemu.

Mungu amlaze mahali pema.

Oooooooooooooh! Unbelievable, R.I.P Mama, Pole kwa Mizengo Pinda, Anne Makinda na Wafiwa
 

yaani mie namshukuru MUNGU amewafunza jambo wanaCCM tena kubwa mnoo
 
Last edited by a moderator:
kila kinapotokea kifo huwa nakumbuka neno hili MTU AMEPEWA KUISHI NA KUFA MARA MOJA TU NA BAADA YA KUFA HUKUMU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…