TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

Kila mtu anapofariki dunia tunapaswa kusikitika.Ila niseme ukweli wangu,hata siku moja sikuwahi kupenda mawazo ya huyu mama.Mambo yake aliyafanya kama hatakuja kuondoka hapa duniani.Kwa kiasi fulani amechangia kufanya CCM iwe na kichwa ngumu na kwa hiyo kwa njia moja au nyingine amechangia katika umaskini wa Watanzania.Kwa kifo hiki waliobaki CCM wakumbuke kwamba dunia ni mapito tu na ipo siku ambayo kila mmoja wetu atasimama mbele za Mungu na kupokea hukumu kulingana na kila jambo alilolifanya duniani kama ni zuri au baya.Kwa hiyo ni vema tukawa makini na kila jambo tunalolifanya.
Nasikitika Kuwapa taarifa ya kifo cha Waziri wetu, Celina Kombani kilichotokea huko India..

Celina.jpg

Celina Ompeshi Kombani (19 June 1959 - 24 September 2015) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Ulanga East constituency since 2005.

She was the Minister of State in the President's Office for Public Service Management.
 
Nipo mahali flani baada ya hii habari kutangazwa sikuamini nilichokisikia kutoka kwa wasikilizaji wa taarifa hii. Eti wanaUKAWA wakashangilia na kupga makofi utadhani walikuwa wanashangilia mpira. Hiviii kweli hii ndo ile Tanzania aliyoicha Mwl Nyerere?? Kwel cc ndo wale watanzania tuliokuwa wamoja?? Hiviii kwel mwaka huu amani atakuwepo kama mtindo ndo huu wakuombeana vifo??? Leo hii watu watashindwa kuwaua wana ccm?? Hiviii UKAWA wakipata madaraka wakawa na nguvu hao wapinzani watakuwa na hali gani?? Si mtawaua na kuwapoteza?? MUNGU ilinde Tanzania tusije tukawa ni watu wakujuta kama mataifa mengine

Nimejaribu kufuatilia huu uzi tokea jana, kwa kweli hali halisi inaonyesha jinsi gani tulivyo na ushirikiano wetu ulipofikia. Hii hali haikuja kwa bahati mbaya japo mnataka watu wajifanye kuonyesha heshima ya kinafiki kwa marehemu. Ni kweli sisi kama watanzania tunapaswa kuheshimiana na kupendana, lakini upendo gani unaojengwa siku ya msiba tu? Chama cha mapinduzi baada ya kukaa madarakani kwa muda mrefu imefikia mahali imejisahau, na imefikia mahali watu wengine wanataka kukitoa. Kwa bahati mbaya wanaccm hawakuikubali hali hii kama sehemu ya ushindani, walichofanya ni kupandikiza chuki kwenye jamii dhidi ya wapinzani kama sehemu ya kuhakikisha wanabaki madarakani. Mifano ni mingi sana, ukiwa mpinzani nchi hii unafanyia vitendo vya hujuma za waziwazi, utatukanwa na kubezwa kwa kila aina. Wanaccm wengi walio madarakani wamegeuka ni miungu watu kiasi cha kujibu na kutenda wapendavyo, hali hii imesababisha watu wa upinzani kuamua kujibu mapigo na matokeo yake ndio haya unayaona. Kwa taarifa yako huyo marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi alikuwa ni mmojawapo ya watu waliolewa madaraka kiasi cha kujisahau. Sina tabia ya kumsema marehemu vibaya lakini hiyo hainizuii kusema ukweli. Mfano mwingine nadhani unauona kwenye majukwaa ya kampeni za ccm, tena mbele ya mgombea urais mtu anadiriki kusema mgombea mwingine alijinyea tena mbele ya watoto na watu wa jinsia na rika tofauti, hapo utalazimisha kuwe na kuheshimiana na upendo wakati wa kifo? Kuna uwezekano wa kunenepeshea ng'ombe mnadani kweli?

Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu, badala ya kulazimisha upendo wa kinafiki wakati wa msiba ni vyema tukarebisha tabia zetu, na kuanza kuheshimiana tukiwa hai ili ikitokea msiba tuwe kitu kimoja. Tutofautiane bila kukashifiana na kudharauliana. Na ni vyema pia tukatenda haki kwa kila mmoja iwe mwanaccm au mpinzani hapo upendo utarejea. Lakini kinyume na hapo hizo huruma tunazozililia sasa hazitokaa zitokee pindi mtu mwenye mtazamo tofauti na wewe anapofariki.
 
alikua anadharau huyo mama tabia za kujifanya kma hii nchi ni ya kwao, kupindiasha ukweli na kuchakachua maoni ya wananchi. anyway mwenzezi mungu amuweke panapo stahili
 
maoni yako yamenigusa sana.. kwa kweli tunatakiwa tujifunze na tupate funzo la msingi sana. Tukumbuke sote tutarudi mavumbini hivyo basi tupendane, tujaliane, tuheshimiane BILA KUJALI VYAMA VYETU.. Na pia napenda kuwaasa wanaCCM wachache wenye dharau nakujiona Miungu watu waache hizo tabia.
 
Watanzania akili zetu zimeingiliwa na kitu gani lakini? Hapa tumeletewa tanzia ya kifo ya Mtanzania mwenzetu,badala ya kuhungana na kumuombea apumzike kwa amani peponi, sisi tunatanguliza masuala ya itikadi za vyama na kejeli juu, tunajisahau kabisa kuwa kila nafsi itaonja muhuti!! Huku kama sio kuchanganyikiwa ni nini?

Tulitakiwa tumuombee akiwa hai, kwa sasa ameshakufa hakuna maombi yatakayofanya kazi, yuko sehemu inayostahili matendo yake hapa duniani,nina imani kubwa atakuwa alitubu makosa yake na kufunguliwa mlango wa mahali pema peponi.
 
Na Kama Kweli ALIMNENEA MANENO MABAYA LOWASA, Basi Mungu Katenda Haki, Tena Afadhari KURA ZA WANYANG'ANYI ZIMEPUNGUA.

naona umefurahi sana. Lakn tambua kwanzia sasa hatujui nan anafuata kat ya mm au ww au mamvi.
Mtamsema sana lakn ndio hvyo hataweza kuwajibu hoja zenu.
Najua wengi wanatoa dhihaka kamakwamba wao ndio wataishi milele wakat hesabu imebaki kwetu.
 
Inauma mkuu mbona CCM ugonjwa Wa MTU inageuza siasa? Inawalipa the Comedy wamdhihaki Lowassa ila Malipo hapa hapa duniani

Naomba Mungu anipe uhai na ampe Mgombea kipenzi cha watu Ngoyai uhai.Ili kabla hatujachukuliwa na Baba kurejea kwake basi tuwe tumemsindikiza kwanza mmoja wa hawa vijana waliojaa dhihaka ze comedy
 
Kumbe na nyie ccm ni wagonjwa?mie nilifikiri wagonjwa wako ukawa tuu,somo kwako Mwiigulu na Bulembo,afya ni zawadi kutoka kwa Mungu,R.I.P. DADA YETU!
 
Tulitakiwa tumuombee akiwa hai, kwa sasa ameshakufa hakuna maombi yatakayofanya kazi, yuko sehemu inayostahili matendo yake hapa duniani,nina imani kubwa atakuwa alitubu makosa yake na kufunguliwa mlango wa mahali pema peponi.

Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma...isiyo na kifani.
Kama wewe unaamini hivyo...vipi ukizikwa kama mzoga bila ya sala/dua yoyote ile.
 
alikua anadharau huyo mama tabia za kujifanya kma hii nchi ni ya kwao, kupindiasha ukweli na kuchakachua maoni ya wananchi. anyway mwenzezi mungu amuweke panapo stahili

Amechangia umasikini na ufukara kwa Watanzania wengi. Mwenyezi Mungu ampatie hukumu anayo stahili.
 
kuzaliwa kusingalikuwa na maana kama kufa kusingalikuwepo..................................maneno ya kwenye mbiu ya pasaka
 
Kapteni mstaafu wa Jeshi John Komba alipata kusema Warioba kaona anakaribia kufa ndiyo anataka kutuachia matatizo ya katiba. Matokeo yake Warioba yupo lakini yeye katangulia na Warioba akatoa salam za rambi rambi.
Akaja Celina Kombani. Yeye aliwahi kusema kuhusu Lowasa kuwa "Afadhali mgonjwa ameondoka mwenyewe, maana angetufia tu". Kilichotokea taifa lipo kwenye msiba mbichi kabisa tukiomboleza kumpoteza 'mpendwa' wetu huyu.
Kama hatazuiwa, huenda Lowasa akahudhuria mazishi yake.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
ananikumbusha nilikuwa pale kivuko cha kilombero alipita pale akapewa kipaumbelw cha kuvushwa na gali yake
 
wew ni nan mpak uhukumu? Ebu achen maneno ya kashfa huwezi jua huwenda kabla ya kutwaliw alipew nafasi ya kujisafisha, ebu tubadilike tuache kunyooshe wengine vidol ikiw cc ni wachafu zaid yao...R.I.P MAMA G
 
Back
Top Bottom