Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Nasikitika Kuwapa taarifa ya kifo cha Waziri wetu, Celina Kombani kilichotokea huko India..
Celina Ompeshi Kombani (19 June 1959 - 24 September 2015) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Ulanga East constituency since 2005.
She was the Minister of State in the President's Office for Public Service Management.
============================
Nyongeza kutoka Magazeti ya leo 25 Sept 2015
Chanzo: Mwananchi
Celina Ompeshi Kombani (19 June 1959 - 24 September 2015) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Ulanga East constituency since 2005.
She was the Minister of State in the President's Office for Public Service Management.
============================
Nyongeza kutoka Magazeti ya leo 25 Sept 2015
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani amefariki dunia jana jioni katika hospitali ya Appolo nchini India, alikokwenda kwa matibabu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema Kombani alipelekwa nchini humo wiki tatu zilizopita.
"Ni Kweli amefariki dunia leo jioni (jana) ndiyo ninachoweza kusema kwa sasa," alisema Dk Kashillilah kwa ujumbe mfupi bila kueleza waziri huyo alikuwa akisumbuliwa na nini.
Katika mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM, chama hicho kilimpitisha Kombani kuwa mgombea tena ubunge katika jimbo la Ulanga.
Waziri huyo alishiriki vikao vyote vya Bunge la Bajeti lililomalizika mwezi juzi mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2015/16.
Wasifu wa Celina Kombani
Celina Kombani alizaliwa Juni 19, 1959.
Alisoma katika Shule ya Msingi Kwiro mwaka 1968-1975, Sekondari ya Kilakala 1975-1978 na baadaye katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora kwa masomo ya juu 1979-1981.
Baada ya masomo ya elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe 1982-1885 na kati ya mwaka 1994-1995 alisomea shahada ya pili ya uongozi katika Chuo cha Mzumbe.
Kabla ya wadhifa wake wa sasa ndani ya utumishi, Kombani aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi) 2008-2010, Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri Tamisemi, Ofisa Utawala mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Meneja wa Kiwanda cha ngozi Morogoro na ofisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Chanzo: Mwananchi
MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM LEO JIONI
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
Picha na Emmanuel Massaka.



