KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Inavyoonekana katika maelezo ya waziri, kikao kile kilimhusu Mfugale moja kwa moja, maanake uwepo wake ulikuwa ni wa lazima. Bila yeye kuwepo kikao kisingewezekana."Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo Katibu Mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee".
Mtu akijisikia vibaya si hupewa huduma ya kwanza na endapo hali ikizi kudhoofu si hulazimika kupelekwa hospitali!?
Hata alipowaambia anajisikia vibaya, badala ya kutafuta huduma za afya, wanamtaka aendelee kuwepo katika eneo hilo la mkutano; pengine aweze kujibu maswali yanayoelekezwa kwake.
Huko ofisini alikokwenda kupumzika, kulikuwa na wafanyakazi. Cha ajabu ni kwamba hawa wafanya kazi ni kama hawakuwa na habari kabisa na marehemu Mfugale. Huyu alikuwa ni mtu mwenye wadhifa mkubwa kwenye wizara ile. Kiongozi huyo, anaingia ofisini, sijui aliwaambia pia kuwa hajisikii vizuri na kuomba kiyoyozi kiongezwe, halafu na kukaa kwenye kiti ofisini na kuachwa/kutelekezwa bila hata ya uangalizi wowote, hata kule kuchungulia tu, boss anaendeleaje? Hadi Katibu mkuu alipokuja na bila shaka marehemu kishafia hapo hapo kwenye kiti?
Ofisi ile, haikuwa na mahusiano mazuri na marehemu Mfugale.
Sasa hawa ndugu wanaolalamika, na hata kilichosababisha kifo cha ndugu yao hawajui:
Mbona wamekubali msiba uendelee na kumchukuwa ndugu yao wakamzike wakati kukiwa na utata mkubwa namna hii?
Hospitali watasemaje hawajui kilichosababisha kifo?
1. Wamepima hakuwa na COVID-19?
2. Postmortem imefanyika, ndugu waliomba pawepo na mwakilishi wao katika uchunguzi huo, kujua ni nini kilichosababisha kifo?
3. Sampuli za mabaki ya chakula/kilichomo tumboni na sampuli za damu zilichukuliwa ili wawe na hakika sumu haikuhusika katika kifo cha ndugu yao?
Maswali ni mengi, lakini inashangaza kuona hawa ndugu wakilalamika tu, halafu hawachukui hatua zozote za kutaka kujua sababu ya kifo cha ndugu yao.