Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonesha sintofahamu (ombwe) kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni

Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonesha sintofahamu (ombwe) kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni

"Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo Katibu Mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee".

Mtu akijisikia vibaya si hupewa huduma ya kwanza na endapo hali ikizi kudhoofu si hulazimika kupelekwa hospitali!?
Inavyoonekana katika maelezo ya waziri, kikao kile kilimhusu Mfugale moja kwa moja, maanake uwepo wake ulikuwa ni wa lazima. Bila yeye kuwepo kikao kisingewezekana.

Hata alipowaambia anajisikia vibaya, badala ya kutafuta huduma za afya, wanamtaka aendelee kuwepo katika eneo hilo la mkutano; pengine aweze kujibu maswali yanayoelekezwa kwake.

Huko ofisini alikokwenda kupumzika, kulikuwa na wafanyakazi. Cha ajabu ni kwamba hawa wafanya kazi ni kama hawakuwa na habari kabisa na marehemu Mfugale. Huyu alikuwa ni mtu mwenye wadhifa mkubwa kwenye wizara ile. Kiongozi huyo, anaingia ofisini, sijui aliwaambia pia kuwa hajisikii vizuri na kuomba kiyoyozi kiongezwe, halafu na kukaa kwenye kiti ofisini na kuachwa/kutelekezwa bila hata ya uangalizi wowote, hata kule kuchungulia tu, boss anaendeleaje? Hadi Katibu mkuu alipokuja na bila shaka marehemu kishafia hapo hapo kwenye kiti?

Ofisi ile, haikuwa na mahusiano mazuri na marehemu Mfugale.

Sasa hawa ndugu wanaolalamika, na hata kilichosababisha kifo cha ndugu yao hawajui:
Mbona wamekubali msiba uendelee na kumchukuwa ndugu yao wakamzike wakati kukiwa na utata mkubwa namna hii?

Hospitali watasemaje hawajui kilichosababisha kifo?
1. Wamepima hakuwa na COVID-19?

2. Postmortem imefanyika, ndugu waliomba pawepo na mwakilishi wao katika uchunguzi huo, kujua ni nini kilichosababisha kifo?

3. Sampuli za mabaki ya chakula/kilichomo tumboni na sampuli za damu zilichukuliwa ili wawe na hakika sumu haikuhusika katika kifo cha ndugu yao?

Maswali ni mengi, lakini inashangaza kuona hawa ndugu wakilalamika tu, halafu hawachukui hatua zozote za kutaka kujua sababu ya kifo cha ndugu yao.
 
Prof Assad nakukumbuka,serikali inawatumishi vilaza karibu wote, katibu unafahamu umri wamzee huyo anakwambia najiskia vibaya badala umkimbize hospitali eti kapumzike au alijua mpango fulani
 
Nimesomaaa weeee NAONA wanne mnajisikia viba ya RUDINI ofisini jf
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurilo: Poleni sana kwa kumpoteza Injinia Patrick Aron Mfugale, mheshimiwa Rais tumesikia maelezo mengi yametolewa kuhusu elimu na ajira ya marehemu, tumesikia vilivile kuhusu mchango wake wa kitaalamu, tumesikia vilevile kuhusu tuzo mbalimbali ambazo amezipata kutokana na utumishi wake uliotukuka.

Vilevile tumepata ushuhuda kutoka kwa watoto na viongozi mbalimbali walioshiriki katika miradi ambayo ameisimamia, itoshe hapo nisiongeze mengine bali niseme nasi tuendelee kumuenzi katika yale aliyokuwa akiyafanya na tujitahidi kadri tuwezavyo kuhaulisha yale yote aliyoyasimamia ili nasi tuendelee kuyafanya kama alivyokuwa akiyatekeleza.

Mheshimiwa Rais, katika salamu za familia wameonyesha ombwe kwamba familia ilikuwa haifahamu ni jinsi gani limetokea na mimi kama msimamizi mkuu wa wizara ninawajibika kutoa maelezo mafupi.

Katika uongozi wa wizara tuna mikutano mbalimbali na ambapo tulikuwa na mkutano kati ya wizara na Tanroads siku ya Ijumaa wiki iliyopita ambao haukufanyika kwasababu marehemu aliomba kikao kisogezwe hadi Jumanne kwani alikuwa ana majukumu mengine ambayo kasababu hakuweza kuyaahirisha.

Kwasababu tunafanya kazi pamoja tuliridhia ombi hilo na kikao kilifanyika Jumanne kama ilivyopangwa, Jumanne tuliamka mimi nikaelekea Bungeni na katibu mkuu wangu sekta ya ujenzi aliongoza kikao hicho.

Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo katika mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee.

Aliamka mwenyewe bila usaidizi wowote na kwenda katika ofisi ya katibu mkuu sekta ya Ujenzi na kikao kiliendelea lakini katibu mkuu aliwaambia kwenye kikao endeleeni na kikao kwanza niende nikamuangalie mhandisi mfugale kisha tuje naye tuendelee na kikao chetu.

Katibu mkuu alipofika ofisini kwake, alimkuta marehemu ameketi kwenye kiti lakini alionekana dhahiri hali yake si nzuri kwahiyo aliuliza wale wasaidizi, kumetokea nini.

Wasaidizi wakasema hapana, alipofika hapa aliomba kiyoyozi kiongezwe ubaridi, kitu ambacho kilifanywa kisha akaketi kwenye kiti, kwahiyo katibu mkuu alifanya uratibu haraka wa magari pale na kumchukua marehemu Mfugale kumtia kwenye gari na kumkimbiza katika hospitali ya Benjamin Mkapa, wakati huo alifanya uratibu na katibu mkuu Afya ambae aliandaa madaktari ambao walipofika pale Benjamin Mkapa, walikuta wanasubiriwa na wakamchukua na kumkimbiza ili apate huduma stahiki.

Baada ya kufanya uchunguzi mfupi, walisema Mhandisi Patrick Aron Mfugale tayari amekwishafariki, baada ya hapo tulianza uratibu wa kuitafuta familia ili tuijulishe kabla ya taarifa nyingine kuifikie jamii.

PIA, SOMA=> Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui
Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo katika mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo Katibu Mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee".

Mtu akijisikia vibaya si hupewa huduma ya kwanza na endapo hali ikizi kudhoofu si hulazimika kupelekwa hospitali!?
Kuna vitu vinatisha Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umskini wa ukoo wako ndio unakufanya uwe na roho mbaya. Miaka yote aliyofanya kazi ya mabilioni ulitaka amiliki banda Majohe na IST? Na awe ananila tu tako Manina wewe!!!??

CCM ndiyo mnafundishwa matusi?
 
Huenda ni mshituko wa Moyo na ishu ilikuwa malipo hewa ya Tanroads
Hoja za kikaguzi ambapo CAG amesema ni mapungufu na siyo ubadhirifu haziwezi kumtisha mtu ambae ameshakutana na hoja mbalimbali za ukaguzi. Watu ukiwasikiliza hufikiri kua hoja za ukaguzi ni ubadhirifu bali hua ni Audit Query(Hoja za ukaguzi) ambazo hujibiwa na baadae kua cleared. Hoja mbaya ni ile kama iliyotokea kwa Boss wa TPA ambapo kulikua na viashiria vys UBADHIRIFU na siyo MAPUNGUFU kama barua ya Mkurugenzi wa Rais Ikulu ilivyofafanua ripoti ya Ukaguzi maalum.
 
Huyu mtu alikua na majukumu mengi sana wakati umri umeenda sana.
Mnafikiri wazungu waliposema watu wa staafu na miaka 55 mpaka 60 walikua wajinga?
Kuna mtu mmoja Sasa hivi mwendazake alikua anasema hadharani kwamba akiondoka yeye miradi hii itasimamiwa na nani?
Je? Sasa hivi hayupo, miradi inasimamiwa na nani?
Sasa hivi amekua mpendwa wetu lkn alipokua hai amepitiliza umri wa kustaafu hakuna aliyeweza kum face na kumuambia akacheze na wajukuu. Kwa sababu Kuna manufaa ambayo watu walipata kutoka kwa marehemu waliendelea kumsifia ili aendelee kuumia ili wapate ugali. Hata familia haikumshauri astaafu kwasababu kwa njia moja walikua wanafaidika huyu CEO akiwa kazini ilhal alikuwa anaonekana kabisa kwamba amechoka.
 
Unajua Donald Trump alikua rais akiwa na umri gani? Pia angalia umri wa yule mama speaker wa bunge lao. Halafu uje tena na hoja ya umri.

Nadhani ni mazingira yetu na mfumo wa maisha yetu ndio shida
 
Hatari sana nenda kapumzike kikao kiendelee wakati kasema walihairisha kikao sababu alikuwa na majukumu mengine leo kikao kinaanza mtu anatoka hajisikii vizuri unasema kapumzike kikao kiendelee sasa mlihairisha kikako cha nini wakati uwepo wake sio muhimu? hapa kuna maswali mengi sana mtu anajiskia vibaya hujui ana nini unamwambia kapumzike ofisi jirani?
"Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo Katibu Mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee".

Mtu akijisikia vibaya si hupewa huduma ya kwanza na endapo hali ikizi kudhoofu si hulazimika kupelekwa hospitali!?
 
Alitoka kwenda kupumzika kwingine
Husomi?.
Kikao kilisogezwa mbele kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine kaja kwenye kikao hajisikii vizuri kikao kinaendelea kaambiwa kapumzike sasa kikao kilihairishwa kwa sababu zipi? kwa haraka uwepo wake haukuwa wa lazima huwezi kusukuma masiku kikao kwa kuwa hatoweza kuja siku kaja hawezi kukaa kwenye kikao lakini kapumzike kikao kinaendelea hivi inaingia kwenye akili kweli? mtu mzima hajisikii vizuri kitu cha kwanza utaita first aid na kikako utahairisha kidogo kumshughulikia key person kwenye kikao sio nenda kampumzike kwani alisema kachoka au hajisikii vizuri? Kufa kwa ghafla kupo sana tu na sisemi labda kafanyiwa kitu ila uwezo wetu wa ku deal na emergency ni very poor au hakuna kabisa. pale mji wa serikali ni lazima ijengwe clinic first aid kwa wafanyakazi wa wizara zote pale.
 
Back
Top Bottom