Ndugu
Mwigulu Nchemba mimi naomba nikupe pongezi za ziada kabisa maana umefungua mlango mkubwa sana ambao ulikuwa umefungwa kwa miaka mingi sana kwenye utoaji wa haki. Lakini mimi kama mwanasheria naomba nikupe ushauri mwingine ambao nadhani utasaidia katika utekelezaji wa hii adhma yako.
Mosi, lugha inayotumika kuandika sheria ni lugha ya kitaalamu ( A Technical Language/ Legalese), hivyo hata utatafsiri kwa lugha yako mama suala la uelewa bado litakuwa ni changamoto kubwa. Hili tatizo siyo lipo tu Tanzania, bali hata kwa nchi kama Uingereza kwasababu lugha ya sheria hutooa baadhi ya maneno kutoka lugha nyingine kama kilatini, kifaransa na kigiriki.
Hii hutokana na sababu kwamba tukibadilisha baadhi ya maneno ya lugha ya kilatini, kifaransa na kigiriki kuja katika lugha zetu basi tunaweza tukawa tumebadilisha maana nzima ya neno kisheria. Hivyo wataalamu wengi husema kukwepa kadhia hii hushauri tusibadilishe maneno hayo kuja katika lugha zetu. Japo wataalamu wengine hushauri kwamba tujitahidi kutumia lugha rahisi (Plain Language) kadiri iwezekanavyo: Hili linawezekana lakini katika upande mwingine kuna baadhi ya maana hubadilika kabisa.
Katika hili nashauri tutumie njia ambazo wenzetu wa mashirika makubwa ya kimataifa kama The International Commission of The Red Cross (ICRC) na The International Law Commission (ILC) hufanya. Wao mbali na kusaidia kufanya tafiti na kuandika sheria mbalimbali husaidia sana katika kuandika
COMMENTARIES ON INTERNATIONAL LAW. Hapa wanauchukua mkataba fulani wa kimataifa au kanuni ya kimataifa na kuielezea katika lugha rahisi kabisa bila kubadilisha maana: Wanaandika historia ya hicho kifungu cha sheria, jinsi gani kinategemewa kutumika na mifano halisi panapo wezekana.
Nakumbuka Tanzania baada ya kupata uhuru wizara ya mambo ya nje ilikuwa na utaratibu mzuri wa kuandika COMMENTARIES kwenye mikataba ya kimataifa. Walishawahi kuandaa kitu kiitwacho T
ANZANIA TREATY SERIES, ambacho kilizungumzia kwa undani baadhi ya mikataba katika uelewa wa mtu wa kawaida kabisa.
Pili, sheria inayosimamia utendaji wa ofisi ya mwansheria mkuu (The Office Attorney General's Discharge of Duties Act) na marekebisho yake ya mwaka 2018, yameanzisha kitu kiitwacho
GOVERNMENT LEGAL TEAM ambacho kina wanachama wafuatao: The Attorney General, The Director of Public Prosecutions, The Solicitor General, The Administrator General, The Executive Secretary of the Law Reform Commission of Tanzania, The Chief Parliamentary Draftsman, The Director of Legal Services in Ministry of Justice, and The Director of Legal Services in the ministry responsible for local government.
Kazi kubwa ya hii timu ni kuhakikisha wanasaidia kutengeneza mbinu ambazo zitarahisisha utoaji wa mzuri wa haki kwa wananchi. Hivyo wanafanya vikao viwili na kuandaa repoti ambazo zinamfikia waziri, hivyo kwasababu hii timu inawajibika kwako wewe Waziri wa Katika na Sheria basi nashauri anza nao hawa wataalamu halafu usikie nini mawazo yao. Unachopendekeza ni kitu kizuri sana, lakini ni kikubwa sana kiutekelezaji na kina changamoto za kiuetendaji na kifedha, hivyo nadhani hii timu itakushauri vizuri sana kufanya tafiti za kutosha katika hili.
Tatu, kama hili litafanikiwa basi nadhani kuwe na kitengo maalumu aidha ndani ya Ofisi ya Mwansheria Mkuu Uandishi wa Sheria au Tume ya mabadiliko ya sheria, ambacho kitakuwa kinafanya kazi ya kuandikia
COMMENTARY kila sheria ambayo inagusa maisha ya mwananchi wa kawaida moja kwa moja (Ikumbukwe siyo lazima ufanyie hivi kila sheria); Unaweza kufanyia haya kwa sheria muhimu kama Katiba, sheria za ardhi, sheria za kodi na sheria za ndoa.
Naomba nikikumbushe yaliyotokea tume ya mabadiliko ya Katika Jaji ya Warioba: Wao waliandaa kitu kiitwacho
BANGO-KITITA YA RANDAMA YA KATIBA, ambayo ilikuwa ni kama
COMMENTARY ambayo ilirahisisha uelewa wa vifungu vya ile katiba. Mle ndani kila kifungu kilielezewa kwa undani na jinsi kilitegemea kutumika.
Nadhani kazi hii ya kuandika COMMENTARY asiruhusiwe kufanya kila mtu, maana wanaweza kutuletea mabalaa. Mfano NGO's au Vyuo Vikuu vinaweza kutaka kufanyia COMMENTARY baadhi ya sheria na wakatuletea matatizo ya kiulewa na tafasiri, hivyo nadhani kuwe na chombo maalumu chenye wataalamu wa sheria ambao watakuwa na EXCLUSIVE MONOPOLY katika kufanya hii kazi.
NB: Mheshimiwa ukiwa unafanya mambo ya msingi kama haya nadhani hata sisi ambao hatuukubali huu utawala tunaweza kujifikiria kukuunga mkono. Lakini ule unazi wako wa kuvaa kofia za kina Mao Zedong na kuhubiri siasa za majitaka nadhani ifike mahali uwaachie akili fupi wakina Humphrey Polepole, Nape na MATAGA.
Wewe ni msomi wa PhD so act like one, tunategemea utakuwa unafanya mambo makubwa (Stragegic Issues) kitaifa kama haya na siyo kubishana na Zitto Kabwe kule mitandaoni. Sifahamu kama unafahamu uzito wa wizara uliyonayo, lakini wewe unaweza ukashawishi wimbo la mabadiliko makubwa hadi kwenye mhimili wa mahakama. Hivyo jiheshimu, achana Cheap Popularity, Worship of State Power and Fanaticism, they'll blind you.
Hongera sana kwa kuwa na nia njema mheshimiwa,
Naomba ubadilike tabia na huu mpango usiwe kwenye makaratasi tu.