Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Pinga pinga chadema kazini
Hii ni taaluma sio swala la kisiasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pinga pinga chadema kazini
unarudishwa nyuma kwa kutumia kiswahili🙄🙄??Hii nchi hii,
Itoshe kusema viongozi wetu wanaturudisha sanaa nyuma
ukitaka hukatazwi kujifunza lugha ya kiingereza kwa ajili ya mawasiliano inapo bidi, hata taifa la urusi lugha yao ni kirusi na inapo bidi wana wasiliana kwa kiingereza kupitia mkalimani.Rafiki sheria ya Tz haiishi hapa Tanzania tu, kuna nchi za jumuia ya madola nao wanaziangalia pia na kuzitumia.
Zaidi ya yote, sheria ni taaluma na lugha ya taaluma Tz ni kiingereza
Usisahau kiswahili ni lugha ya taifa na si lugha ya taaluma.
Official languages za Tanzania ni mbili:
1) English
2) Swahili
Kama lugha yetu rasmi ya kwanza ni English, kwa nini kusifanyike utaratibu utakaowezesha Watanzania kuzijua vizuri lugha zet zote mbili zilizo rasmi.
Hapo zamani Watanzania hawakuwa na lugha ya Kiswahili lakini kwa jitihada mbalimbali, leo sote tunajua. Kwa nini isifanyike hivyo hivyo kwa Kiingereza? Mtu mmoja kushindwa kukimudu Kiingereza isiwe sababu ya kubadilisha mfumo mzima wa matumizi ya lugha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na hapa Afrika ni nchi gani inayotumia lugha yao ya asili?Kujua kiingereza sio weledi wa kujua sheria, kinacho takiwa watanzania waelewe haki zao, kwa nini wasumbuke kwa kulazimishwa na kizungu?!! mataifa mbali mbali yanatumia lugha zao ktk mambo yao, mfano china, urusi, uturuki, ufarnsa, n.k.
Lugha ya kiingereza ibaki kama lugha tu lkn isiwe ndio inaongoza taratibu za utoaji haki za watanzania ambao wengi wao hawajui lugha ya kizungu.
Imepita miaka mingapi mnatumia Kiingereza kama Official language kwenye idara nyeti na maisha yakasonga upambavu wenu unawafanya mjione wajuaji wakati ni zero brained huyo ncheba aliiba pesa huko EPA leo anataka kuihujumu sheria.Huo mfumo wa matumizi ya lugha ya Kiingereza ktk shughuli za kiserikali ulikuwa ni mfumo/utaratibu ulio wekwa navwakoloni Kwa faida ya wakoloni Kwa sasa hakuna haja ya kutumia kiingereza ktk shughuli zote ZA serikali hiyo haimaanishi kuwa umekatazwa kujifunza kiingereza bali utajifunza tu kama ilivyo Kichina au kifaransa, ila ktk matumizi ya serikali haswa ktk utoaji haki hakuna sababu yoyote ya kutumia lugha ya kigeni/kiingereza au Kichina au kifaransa wakati tuna lugha yetu iliyo jitosheleza kiswahili.
Hata hivyo lazima wapo "watumwa" wachache watapinga na kubeza kwa masilahi yao binafsi lkn hatua iliyo fikiwa na serikali ni safi sana
Kabudi na Mwakyembe ni wanasheria wabobezi lakini wameshindwa kulinda taaluma zao kwa kisingizio cha kuokotwa majalalani shem on them hata tutumie lugha zetu za kuzaliwa kama kuna mtu anadharau sheria haisaidii kitu ataendendelea tu kutupumbaza kwa sababu mamlaka anayo,hela anayo,dola anayo,mahakama ni za kwake,polisi ni wake,jeshi ni lake nk.hapo hakuna ahueni jitahidini kutumia akili Kikwete alishasema.Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba kwa kuweka mkazo la matumizi ya kiswahili ktk mambo yanayo tuhusu watanzania na haswa katika maswaala ya haki.
Watanzania karibu 95% wanafahamu kiswahili sio kiingereza hivyo jambo hilo litawasaidia watanzania wengi kujua sheria na jinsi ya kudai haki zao, na tunaomba hilo liende sambamba na hukumu zinazo tolewa pia ziwe kwa lugha yetu ya kiswahili ili tuweze kujua kilicho andikwa.
Hakika matumizi ya lugha yetu yatarahisisha zaidi upatikanaji wa haki za wananchi kuliko matumizi ya kiingereza.
tunaomba maamuzi haya yatekelezwa haraka kama waziri alivyo sisitiza.
Ukweli mtupu, mbumbumbu watakupinga.Ni wazo zuri ila kusema sheria ziandikwe kwa kiswahili ili watanzania waweze kuelewa hapa nadhani mheshimiwa hajaelezwa vyema.
Kujua lugha fulani sio kujua sheria, sheria ni zaidi ya hapo.
Uingereza wanaongea kiingereza lakini bado sheria ni moja ya fani ngumu kuielewa.
Mfano wapili, Katiba yetu ipo kwa lugha ya kiswahili lakini watanzania hawajui hata haki zao zilizopo kwenye katiba.
Wazo zuri ila halitatibu tatizo. Tatizo lipo nje ya lugha ya kiingereza inayotumika kwenye mambo ya kisheria nchini.
Sheria ya ardhi inayo nakala ya kiswahili lakini bado migogoro inaongezeka vile vile sheria za mirathi na kanuni ya adhabu.
fact.Hamjui lugha acheni visingizio! Hata kiswahili tu hamjui, utasikia "miladi" " laisi" "bizaa", "mirasi". Suluhisho ni kutoa elimu bora na Watanzania wapende kujifunza na kutafuta maarifa.
Unaweza kumpeleka ng'ombe mtoni, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.Ni wazo zuri ila kusema sheria ziandikwe kwa kiswahili ili watanzania waweze kuelewa hapa nadhani mheshimiwa hajaelezwa vyema.
Kujua lugha fulani sio kujua sheria, sheria ni zaidi ya hapo.
Uingereza wanaongea kiingereza lakini bado sheria ni moja ya fani ngumu kuielewa.
Mfano wapili, Katiba yetu ipo kwa lugha ya kiswahili lakini watanzania hawajui hata haki zao zilizopo kwenye katiba.
Wazo zuri ila halitatibu tatizo. Tatizo lipo nje ya lugha ya kiingereza inayotumika kwenye mambo ya kisheria nchini.
Sheria ya ardhi inayo nakala ya kiswahili lakini bado migogoro inaongezeka vile vile sheria za mirathi na kanuni ya adhabu.
Huu ndo ukweli mchungu ambao wengi hawajui au wanafumbia macho makusudi.....Sheria ina lughà yake ngumu sana kuelewa kwenye lughà yoyote hata kwa wanasheria wenyewe ndo maana Katiba na Sheria hata kwenye matumizi ya kawaida tafsiri halisi hutolewa na Mahakama Kuu baada ya kupitiwa na jopo la Majaji.
usipo enzi lugha yako iko siku tutatumia lugha hata lugha ya kiarabu ktk shughuli za serikali kwa sababu tu eti kiarabu pia ni lugha ya kimataifa. Usipo kuwa na msimamo na kitu chako ukubali kuendeshwa kama gari bovu.Na hapa Afrika ni nchi gani inayotumia lugha yao ya asili?
Mwigulu alivyo na akili finyu Law School siyo watunga sheria wala siyo wenye mamlaka ya kuzitafsiri hizo sheria.Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kutafuta wataalamu mara moja wenye uwezo wa kutafsiri sheria zote za nchi kwa lugha ya Kiswahili
Imeamriwa kufanywa hivyo ili iwe rahisi kwa wananchi kuelewa sheria hizo hususan wakati wa kesi na hukumu ili kurahisha uelewa
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo, Dar es Salaam katika ziara yake katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo, ambapo amesema wananchi wanapata shida kuelewa sheria za nchi kutokana na lugha inayotumiwa
Aidha ameitaka Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kuwaandaa wanaopata mafunzo hayo kwa muelekeo wa Kiswahili hata kama watatumia kiingereza.
Unaweza kujifanya unajua sana lakini hiyo haitaondoa ukweli wa usichokijua.Huo mfumo wa matumizi ya lugha ya Kiingereza ktk shughuli za kiserikali ulikuwa ni mfumo/utaratibu ulio wekwa navwakoloni Kwa faida ya wakoloni Kwa sasa hakuna haja ya kutumia kiingereza ktk shughuli zote ZA serikali hiyo haimaanishi kuwa umekatazwa kujifunza kiingereza bali utajifunza tu kama ilivyo Kichina au kifaransa, ila ktk matumizi ya serikali haswa ktk utoaji haki hakuna sababu yoyote ya kutumia lugha ya kigeni/kiingereza au Kichina au kifaransa wakati tuna lugha yetu iliyo jitosheleza kiswahili.
Hata hivyo lazima wapo "watumwa" wachache watapinga na kubeza kwa masilahi yao binafsi lkn hatua iliyo fikiwa na serikali ni safi sana
Safi saana waziri,nakupongeza sana kwa kuliona hili.Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kutafuta wataalamu mara moja wenye uwezo wa kutafsiri sheria zote za nchi kwa lugha ya Kiswahili
Imeamriwa kufanywa hivyo ili iwe rahisi kwa wananchi kuelewa sheria hizo hususan wakati wa kesi na hukumu ili kurahisha uelewa
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo, Dar es Salaam katika ziara yake katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo, ambapo amesema wananchi wanapata shida kuelewa sheria za nchi kutokana na lugha inayotumiwa
Aidha ameitaka Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kuwaandaa wanaopata mafunzo hayo kwa muelekeo wa Kiswahili hata kama watatumia kiingereza.