Waziri Dkt. Pindi Chana alishuhudia Mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba Sports Club dhidi ya Raja Casablanca

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Kuna shutuma zimetolewa na MINOCYCLINE zikiwa na lengo la kuichafua Serikali, Waziri Dkt. Pinda Chana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Serikali kupitia Waziri Dkt. chana imehudhuria michezo yote ya Simba na Yanga na sio mchezo wa Yanga pekee kama ambavyo MINOCYCLINE ameeleza.

MECHI YA SIMBA

Waziri Dkt. Pindi Chana alishuhudia Mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba Sports Club dhidi ya Raja Casablanca ya nchini Morocco, uliochezwa Februari 18, 2023 katika Uwanja wa Mkapa Dar. Mpira ulimalizika kwa Timu ya Raja Casablanca kushinda magoli 3 kwa 0.



MECHI YA YANGA

Waziri Pindi akikabidhi zawadi ya shilingi milioni 15 kwa Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said ikiwa ni ahadi ya Rais wa Tanzania Suluhu Samia kwa Klabu hiyo baada ya kuifunga Timu ya TP Mazembe ya nchini Kongo magoli 3 kwa 1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

 
Mbona ile Jana hakuwa na Furaha Kubwa pale VIP kama aliyokuwa nayo leo?

Hivi kuna Mtu asiyejua kuwa CCM inajinasibu na Yanga SC na Yanga SC nayo inajinasibu na CCM?

Nashukuru kwa kuwahi kufanya Counter juu ya Uzi wangu na najua Ujumbe umeshawafikieni.


Hovyo kabisa......!!!!!!
 
Suala sio furaha; hoja yako ulisema Serikali na Waziri Dkt. Chana hawakuwepo siku ya jana katika mechi ya Simba.

Suala la furaha au tabasamu siku ya jana halikuwepo kwa watanzania wote; jana nchi ilipata aibu, ilikuwa ni siku yenye huzuni na haikuwa busara kwake kuonyesha tabasamu katika hali ile ya kufungwa.

Kama watanzania, tulikuwa kwenye maumivu ya kufungwa.
 
Ni hili popoma peke yake limekurupuka. Halikujua kama waziri alikuwepo uwanjani, linajibiwa linageuza Gia eti mbona hakuwa na furaha.

Ni Nani alikuwa na furaha Juzi pale?
Nahisi hakuamini kuwa Yanga atashinda.
 
Hivi angekua na furaha timu imefungwa? Si angeonekana anafurahia timu kufungwa? Yaani ni sawa na kucheka msibani asingefanya hivyo me popoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…