Waziri George Simbachawene: Waliowashambulia wapenzi wakiwa faragha kwa madai ya kuwafumania wakamatwe

safi sana..umesoma mpaka la ngapi?
 
ni upumbavu kwenda kumfunania mkeo au mumeo na mtu ambaye hafahamu chochote kuhusu historia ya mahusiano ya mhusika..

yaani mkeo kakutana na jamaa barabarani katongozwa na jamaa hajui chochote kuhusu wewe kuwa na ndo na huyo mkeo..na mkeo kakubali na hakusema kama yeye ni mke wa mtu..Kosa la mfumaniwa ni nini hapo kama sio upumbavi wa mkeo au mmeo..
 
Naamini Huyu jamaa ana Mke...namshauri awe makini asije kuwa kama Kangi aliekaa hapo akaanza kujisahau....Hili jambo la mtu kuchukua mkeo ukimkuta umchekee?? Hivi wewe simbachawene ukikuta mtu na mkeo unafanyaje?? Sasa utawashtaki na sheria gani.??

Nchi ina mambo ya ajabu hii..
 
Kwa hyo ukikuta mke wako ananyanduliwa home inabid urudi ulipotoka hadi wamalize!!!??
Naam....maana ukiingilia utafungwa kwa kosa la kuharibu faragha za watu na shahidi atakuwa mkeo.
 
Pale ambapo unapata sababu nyingine ya kuwaambia ndugu kwanini huwowi
 
Kutoka Maktaba!

Mnakumbuka mwaka fulani enzi za Utawala wa JK, ilivuma kwamba mbunge fulani kwa jina la Tembochawenu, alifumaniwa akiwa na mke wa mtu, na alipokea kichapo sana huyo Tembochawenu, na ikavuma kwamba amekatwa mkono kwa panga. Watu walikuwa wanauchunguza mkono sana, kama ni kweli umekatwa au la, na jamaa anavaa shati refu mpaka leo!
 
Ukweli mchungu.. Watu wanajifasahaulishaga hili.
 
Mojawapo ya kiashiria kinachoonesha kiwango cha chini cha ustaarabu na utu wa mwanadamu ni kupigana, kuharibu, kujeruhi au kuua kwa sababu ya mapenzi.

Binadamu waliofikia viwango vya juu vya ustaarabu walishatoka katika hali za aina hii za uhayawani na ushenzi(barbarism). Wanafahamu kuna wakati na inawezekana mapenzi ya mwenzi wao yanaweza kuisha kabisa na hivyo huwa wepesi kukubaliana na hali hiyo inapotokea hivyo hata kama waliishi pamoja nusu karne.

Binadamu wasiostaarabika ndio huwa kama Sokwe au Penguins inapotokea mwenzi wake ameishiwa mapenzi naye na anaonekana kuhamishia au kutaka kuhamishia mapenzi hayo kwengine. Hapo ndipo fitna na ukatili wa kila aina utakapoibuka dhidi ya huyo mwenzi wake ikwepo matukio kama "kuandaa fumanizi", " kupaka mafuta" kuchoma watu ndani ya nyumba, kuharibu biashara yake na wengine kufikia hadi kuua!

Hongera Waziri Simbachawene kupiga marufu mmojawapo ya hizi tabia za kishenzi ambayo imechekuliwa kama ni jambo lilio sawa na sahihi kwa muda mrefu sana. Lazima watu wajifunze na wafahamu mapenzi hayalazimishwi, yakiisha yameisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…