Hakuna uhuru wa kutumia uchi nje ya ndoa.kumbuka ndoa ni mkataba wa watu wawili kwa hiari kuishi kwa uaminifu mpaka mwisho wa maisha yao,sasa huo Uhuru wa kutumia uchi wako wakati ukiwa na mkataba na mtu mwingine unautoa wapi?
Unataka kutumia uchi wako kwa Uhuru,ni rahisi tu jitoe kwenye ndoa,ila una ndoa ulilipiwa mahari,unaishi kwa mumeo,unatumia jina lake,una watoto nae nk halafu useme uko huru kutumia uchi wako huko nje halafu bado unarudi tena kwa mwenza wako,huo Uhuru haupo,jiandae kufumaniwa tu,na anayekufumania omba awe mstaarabu utoke salama.
Mwisho,kufumania ni hatua mojawapo ya kupata ushahidi usioacha shaka wa usaliti wa mwenza wako kwa hatua zaidi za kisheria au kimaamuzi,lakini sio lazima inategeme mtu wa mtu,kama unaweza kupata ushahidi kivingine sawa.
Tena wakristo tunaambiwa Mwanamke hana haki juu ya mwili wake Bali mumewe na mume hana haki juu ya mwili wake Bali mkewe,hauko huru.