Waziri George Simbachawene: Waliowashambulia wapenzi wakiwa faragha kwa madai ya kuwafumania wakamatwe

Waziri George Simbachawene: Waliowashambulia wapenzi wakiwa faragha kwa madai ya kuwafumania wakamatwe

The thing is
Kuna baadhi ya wanawake ambao sio waaminifu tena unakuta hata hawajaolewa.
Wanawake hawa wanashirikiana na wanaume ambao sio waaminifu ambapo mmoja anajifanya mume wake .
Hao wanawake ambao sio waaminifu wanajiachia kwenye mabar makubwa wanajitongozesha kwa wanaume
Ukiingia anga zake anakukubalia mnaenda lodge yeye anawasiliana na wale wanaume wanakuja lodge mlipo wanajifanya wamefumania.
Hizo tabia zilishamiri sana dsm hadi wajuba wakawa wanawanyanganya mademu simu wasifanye makati wanaelekea lodge wanarudisha akimaliza tukio.
Hizi tabia zilishamiri sana .
Mwisho nashauri wanaume wenzangu msipende kuchepuka na wake za watu
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Geoge Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa waliowashambulia wapenzi wakiwa kwenye faragha wakidai kuwa wamewafumania.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 jijini Dar es Salaama baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha.​
Nahisi huyu Waziri ana mchepuko mke wa mtu, anaogopa kufumaniwa!
 
Naamini Huyu jamaa ana Mke...namshauri awe makini asije kuwa kama Kangi aliekaa hapo akaanza kujisahau....Hili jambo la mtu kuchukua mkeo ukimkuta umchekee?? Hivi wewe simbachawene ukikuta mtu na mkeo unafanyaje?? Sasa utawashtaki na sheria gani.??

Nchi ina mambo ya ajabu hii..
Heeee!!mkuu mbona inaonekana kama unaendeshwa na hisia tu kuliko sheria?!kosa la waziri ni nini, kwani sheria ipo wazi ukimfumania mke/mme hiyo ni kesi ya madai, kafungue madai yako mahakamani, nakushangaa unaposema eti utawashitaki kwa sheria ipi?!!wewe ukimpiga au kumdharirisha kibao lazima kikugeukie tu na ina kuwa jinai!!muulize jamaa aliyemfumania jamaa akaja na mabouncer wakamlawiti, walichezea mvua 30, wapo segerea!!na huyo jamaa sasa ndio anaishi na mke wa jamaa sasa!!nani mjinga hapo?!!ni kitu kinauma lakini busara yako ndio itakuokoa.
 
Kujiondosha kwenye huo muunganiko ndio njia sahihi, na ufanye hivyo bila vurugu.
Nipo kwangu mtu namlisha namvisha kila huduma namhudumia, kujiondoa hataki then anafanya hivyo nje, pata picha hapo!
 
Nakumbuka hata Waziri Simbachawene ilishawai kuletwa kashfa yake ya fumanizi akajeruhiwa mkono.
Kwahiyo mara hii anataka arudie yaliyosababisha ajeruhiwe mkono lakini asifumaniwe au akifumaniwa awe na haki kisheria kumshitaki mwenye mke, kwahiyo ameamua kutangaza hivyo ili kujilinda yeye na wazinzi wenziwe?!
 
The thing is
Kuna baadhi ya wanawake ambao sio waaminifu tena unakuta hata hawajaolewa.
Wanawake hawa wanashirikiana na wanaume ambao sio waaminifu ambapo mmoja anajifanya mume wake .
Hao wanawake ambao sio waaminifu wanajiachia kwenye mabar makubwa wanajitongozesha kwa wanaume
Ukiingia anga zake anakukubalia mnaenda lodge yeye anawasiliana na wale wanaume wanakuja lodge mlipo wanajifanya wamefumania.
Hizo tabia zilishamiri sana dsm hadi wajuba wakawa wanawanyanganya mademu simu wasifanye makati wanaelekea lodge wanarudisha akimaliza tukio.
Hizi tabia zilishamiri sana .
Mwisho nashauri wanaume wenzangu msipende kuchepuka na wake za watu
Basi angeweka wazi au angepitisha azimio kuwa ni afadhali mtu akitaka kumfumania mtu wake avihusishe vyombo vya dola, ingeleta maana sana tena sana.
 
yeah no hard feelings enjoy maisha mkuu life is too short ukichanganya na haya ma covid utakufa hujafaidi hela yako
Na vile chawene amesema kunifumania huruhusiwi mpaka ue umetembea na cheti cha ndoa.

Ngoja ninoe mtalimbo,kuwa na kiongozi mwanamke wananchi tunajienjoy sana.
 
Unataka kufumania ili iweje? Itakusaidia nini ukifamania?
Basi angeweka wazi au angepitisha azimio kuwa ni afadhali mtu akitaka kumfumania mtu wake avihusishe vyombo vya dola, ingeleta maana sana tena sana.
 
That's not what he said, amedai fumanizi lisiwe la kupanga hata kama una cheti cha ndoa, ukiwafumania 'accidentally'[emoji38][emoji38] kama kuna kitu cha aina hiyo na una cheti cha ndoa ndipo unawashitaki polisi[emoji1787][emoji1787].
Hairuhusiwi kuwadhalilisha wala kuwarekodi, hapo unakuwa umefanya jinai.
Halafu mjini hapa tunaishi kwa matukio
 
yani watu kupewa nafuu ya kuchepuka tumesahau hadi tozo za miamala
 
Tumefulai na kushukulu kwa kututetea
Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene amekea tabia ya watu kukusanyana na kuvamia watu walioko kwenye faragha kwa kisingizio cha fumanizi akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na utu na watakamatwa wakigundilika.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 6,2021 ambapo amesema baadhi ya watu wamejingea mazoea ya kuwavamia watu wenye uhusiano ya kimapenzi wakiwa kwenye faragha zao mahali wanapokuwa katika nyumba au hotelini.

“Tabia hii imeshamiri sasa kama ambavyo video nyingi zinarushwa rushwa mitandaoni, leo nitumie fursa hii kutoa msingi wa kisheria lakini kukemea tabia hii ambayo imeanza kuonekana inaota mizizi. Ni kinyume cha sheria kabisa kuwaingilia watu walio kwenye faragha,” alisema

“Wakati mwingine watu wanafanya hivyo kwa kisingizo kuwa wamefumania, hakuna fumanizi ambalo linaweza kupangwa na kikundi cha watu, wanawake na wanaume wanapanga kwenda kuwavamia na kuwaingilia uhuru wao waliopo faraghani, kitendo hicho ni kinyume cha sheria ,”

Amesema hata kama ni fumanizi litakuwa pale ambapo si jambo la kupangwa na huyo anayefumania awe na ndoa halali na cheti halali cha ndoa lakini sio kwa mtu ambaye ulikuwa naye tu “Huwezi kusema umemfumania hawala yako, mahusiano ya hawala ni ya kupita”.

Amesema tabia hiyo inakiuka misingi ya utawala bora, heshima na utu na hasa heshima ya wanawake kwakuwa wanaodhalilishwa sana katika hilo ni kina mama ambao walishakuwa na uhusiano na mwanaume fulani wakaachana akawa na mwingine halafu yule wa mwanzo anamfumania.

“Suala la kudhalilisha watu wako uchi wa mnyama na wanapata kipigo hilo haliwezi kukubalika katika nchi yetu, kwa nafasi yangu nachukua nafasi hii kuliagiza jeshi la polisi wahakikishe wanafuatilia matukio haya hususani hili linalozunguka kuanzia jana, wahakikishe wale wote waliohusika wanakamatwa,” amesema Simbachawene.

Chanzo: Mwananchi online.

Tuongee kikubwa, kumbe sheria ya faragha inaruhusu hadi kunyandua mbususu za wake za watu?
 
Vyombo vya dola vina kazi nyingi za maana za kufanya kuliko kufuatilia mambo ya kipuuzi.
Basi angeweka wazi au angepitisha azimio kuwa ni afadhali mtu akitaka kumfumania mtu wake avihusishe vyombo vya dola, ingeleta maana sana tena sana.
 
Vyombo vya dola vina kazi nyingi za maana za kufanya kuliko kufuatilia mambo ya kipuuzi.
Hili ndio jibu nililokuwa nalingoja, je vipi aliyetoa kauli kuhusu hayo mambo ya kipuuzi?
 
Back
Top Bottom