Waziri Gwajima ampatia cheti mwanaume aliyekimbiwa na mkewe siku ya harusi

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na makundi maalumu, Doroth Gwajima ametoa cheti kwa mwanaumea aliyekimbiwa na mkewe siku ya harusi kutambua mchango wake na uvumilivu wake siku ya tukio.

Vipi wakuu mngekuwa nyinyi mngeweza kuvumilia kukimbiwa siku ya harusi?

Pia Soma >> Wizara ya Maendelo ya Jamii: Kumpa tuzo aliyekimbiwa na Bi. Harusi, Waziri Gwajima ampigia simu

===
SaveClip.App_565956137_18067620932523234_5809907018939396889_n.webp

Bw. Futakamba alikimbiwa na Bi. Harusi wake kuelekea kwenye kufunga ndoa yao tarehe 26/07/2024 huku akiwa alishapokea michango mbalimbali na kulipia gharama zote za harusi hiyo.

Katika kulibeba jambo hilo zito na la ghafla, Bw. Futakamba aliamua kutulia, kuvuta subra na hekima iliyomfanya aamue kufanya sherehe hiyo peke yake badala ya kuanzisha mzozo ambao, ungeweza kuishia kwenye ukatili wa kijinsia.

Aidha, alipoulizwa aliipokeaje hali hiyo alisema, unapopatwa na changamoto lazima kwanza, umrudie Mungu akuongoze kukupa njia sahihi. Vilevile, alisema, amefarijika kuona jambo hilo likipokelewa vizuri na watanzania ikiwemo Waziri wa Maendeleo ya Jamii.

Kuhusu matarajio yake ya ndoa alisema, suala hilo bado lipo iwapo, Bi. harusi huyo bado atakuwa tayari. Aidha, kuhusu Waziri wa Maendeleo ya Jamii kumpa Tuzo ya Pongezi alisema: Mhe. Waziri pia, ahimize malezi kwa wazazi na aikumbushe jamii juu ya kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na jamii ibadili mtazamo juu ya changamoto kwani, jambo la hasira limepitwa na wakati, alitoa Zaburi 23.

TUNAJIFUNZA NINI? Kumcha Mungu ni chanzo cha Hekima inayoweza kuepusha madhara yasiyo ya lazima pale penye jambo la maudhi. Aidha, ni muhimu Vijana wapewe elimu ya mahusiano na elimu ya maisha kwa ujumla.

LENGO LA CHETI.

1. Kutambua hekima na ujasiri wa Bw. Futakamba na wengine wote waliowahi kukutwa na mkasa kama huu na wakatoka salama kwa hekima.

2. Cheti hiki kuwa utambulisho kwa wadau wote ambao, wangependa kushirikiana na Bw. Futakamba katika kueneza hekima hii kwa vijana wote.

3. Kutoa wito kwa yeyote yule aliye kwenye harakati za kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia kuiona hekima chanya ya Bw. Futakamba na kumshirikisha kwenye kuongeza nguvu ya kuelimisha jamii.

HITIMISHO; kwa upande wa Wizara, tutamshirikisha Bw. Futakamba kujifunza mikakati ya kisera ili, kutumia mchango wake katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia. Aidha, kila anayeguswa kumpa Pongezi za kumtia moyo Bw. Futakamba, anapatikana Katavi, Mpanda, simu 0625607090.

SHUKRANI Ayo Tv waliorusha tukio hili na kuutarifu umma wa watanzania kuhusu ujasiri na hekima ya Bw. Futakamba.
1760345469072.png
 
Michango ya harusi isiwepo kama mambo ndio haya hakuna kutoa mchango wa harusi
 
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na makundi maalumu, Doroth Gwajima ametoa cheti kwa mwanaumea aliyekimbiwa na mkewe siku ya harusi kutambua mchango wake na uvumilivu wake siku ya tukio.

Vipi wakuu mngekuwa nyinyi mngeweza kuvumilia kukimbiwa siku ya harusi?

Pia Soma >> Wizara ya Maendelo ya Jamii: Kumpa tuzo aliyekimbiwa na Bi. Harusi, Waziri Gwajima ampigia simu

===
View attachment 3487891
Bw. Futakamba alikimbiwa na Bi. Harusi wake kuelekea kwenye kufunga ndoa yao tarehe 26/07/2024 huku akiwa alishapokea michango mbalimbali na kulipia gharama zote za harusi hiyo.

Katika kulibeba jambo hilo zito na la ghafla, Bw. Futakamba aliamua kutulia, kuvuta subra na hekima iliyomfanya aamue kufanya sherehe hiyo peke yake badala ya kuanzisha mzozo ambao, ungeweza kuishia kwenye ukatili wa kijinsia.

Aidha, alipoulizwa aliipokeaje hali hiyo alisema, unapopatwa na changamoto lazima kwanza, umrudie Mungu akuongoze kukupa njia sahihi. Vilevile, alisema, amefarijika kuona jambo hilo likipokelewa vizuri na watanzania ikiwemo Waziri wa Maendeleo ya Jamii.

Kuhusu matarajio yake ya ndoa alisema, suala hilo bado lipo iwapo, Bi. harusi huyo bado atakuwa tayari. Aidha, kuhusu Waziri wa Maendeleo ya Jamii kumpa Tuzo ya Pongezi alisema: Mhe. Waziri pia, ahimize malezi kwa wazazi na aikumbushe jamii juu ya kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na jamii ibadili mtazamo juu ya changamoto kwani, jambo la hasira limepitwa na wakati, alitoa Zaburi 23.

TUNAJIFUNZA NINI? Kumcha Mungu ni chanzo cha Hekima inayoweza kuepusha madhara yasiyo ya lazima pale penye jambo la maudhi. Aidha, ni muhimu Vijana wapewe elimu ya mahusiano na elimu ya maisha kwa ujumla.

LENGO LA CHETI.

1. Kutambua hekima na ujasiri wa Bw. Futakamba na wengine wote waliowahi kukutwa na mkasa kama huu na wakatoka salama kwa hekima.

2. Cheti hiki kuwa utambulisho kwa wadau wote ambao, wangependa kushirikiana na Bw. Futakamba katika kueneza hekima hii kwa vijana wote.

3. Kutoa wito kwa yeyote yule aliye kwenye harakati za kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia kuiona hekima chanya ya Bw. Futakamba na kumshirikisha kwenye kuongeza nguvu ya kuelimisha jamii.

HITIMISHO; kwa upande wa Wizara, tutamshirikisha Bw. Futakamba kujifunza mikakati ya kisera ili, kutumia mchango wake katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia. Aidha, kila anayeguswa kumpa Pongezi za kumtia moyo Bw. Futakamba, anapatikana Katavi, Mpanda, simu 0625607090.

SHUKRANI Ayo Tv waliorusha tukio hili na kuutarifu umma wa watanzania kuhusu ujasiri na hekima ya Bw. Futakamba.
Mwanamme wa shoka ukikimbiwa na bi harusi siku ya harusi unatakiwa kufanya maamuzi magumu unachagua mwanamke mwingine hapo hapo kwenye harusi, hata bridesmaid mmoja ambaye hajaoelewa unampanga mnaendeleza jambo lenu.

Katika wanawake wote waliokuja kwenye harusi utakosa anayekutamani na kutaka kuolewa hapo?

Mnamaliza lengo la siku hiyo mengine mtajuana baadaye.

One monkey doesn't stop a show 🤣🤣🤣
 
hahaha umetishaa aisee yaani ningekuwa mimi ningetafuta hata ma x girlfriend zangu wa primary wa kureplace huyo mbwaa
 
Kidume cha mbegu inatakiwa siku ya harusi hata kabla bi harusi hajakukimbia uanze wewe kujisikia vibaya unamuoa huyu wakati kuna vyuma vikali zaidi ndiyo kwanza unaviona siku ya harusi.

Sasa hapo akikukimbia siku ya harusi ndiyo kwanza unasema "Yeeeeees, kanipa nafasi kuopoa chuma kikali zaidi kile palee siti za mbelembele pale nimekikubali..." 🤣🤣🤣
 
Mwanamme wa shoka ukikimbiwa na bi harusi siku ya harusi unatakiwa kufanya maamuzi magumu unachagua mwanamke mwingine hapo hapo kwenye harusi, hata bridesmaid mmoja ambaye hajaoelewa unampanga mnaendeleza jambo lenu.

Katika wanawake wote waliokuja kwenye harusi utakosa anayekutamani na kutaka kuolewa hapo?

Mnamaliza lengo la siku hiyo mengine mtajuana baadaye.

One monkey doesn't stop a show 🤣🤣🤣
Huko ni kutumia akili mnemba
 
Naona tumekuwa wazuri wa kutengeneza content which is well good and fair lakini wakati tunaburudika na haya tusisahau yanayotungojea kesho (na haya kweli ndio nguzo za ustawi wa jamii) haya mengine ni mazungumzo baada ya habari

hahaha umetishaa aisee yaani ningekuwa mimi ningetafuta hata ma x girlfriend zangu wa primary wa kureplace huyo mbwaa
utakuta hao classmates ni wazee kuliko wewe, sasa jitu lina umri mkubwa utalipeleka wapi?
 
Haya matukio ya kukimbiwa siku ya harusi ni mengi na hayaripotiwi. Wengine huachwa muda mfupi baada ya ndoa kufungwa na wengine huachwa hapohapo wakati wa kufunga ndoa mwanaharusi anakataa kula kiapo cha ndoa na zoezi linaishia hapohapo. Ndio maana siku hizi mchumba hutafunwa sana hata akija kukataa kufunga ndoa tayari ashanyanduliwa sana tu akichomoa haina uchungu
 
Hicho cheti kitakuwa na msaada wowote kweli Kwa huyo mhanga? Au ni mbinu ya kisaikolojoa ya kumpoza asiumie zaidi au hata kupelekea kujitoa uhai.
 
Kama hiyo hali ingelinitokea mimi ,yaani sirembi aisee , hapohapo naita mchepuko wangu chap then ngoma inaenda hivyo.
 
Back
Top Bottom