Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, alidai atamfufua Chifupa pia alikutwa na Mrembo akasema mkono wa Baunsa

Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, alidai atamfufua Chifupa pia alikutwa na Mrembo akasema mkono wa Baunsa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Waziri wa Afya, Dkt Gwajima leo ameelezea suala askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kupinga chanjo ya Covid-19 na kudai pamoja na ushemeji walionao haungani na itikadi zake.

Pia ameshangaa wanaomuamini akitolea mfano wa Askofu kudai atamfufua Amina Chifupa kitu ambacho hajatimiza mpaka sasa. Pia amemshangaa kuchukua ubunge ilhali alishasema ni cheo kidogo kwake.

Mwisho Dkt Gwajima amemshangaa askofu Gwajima kukutwa na mrembo na kudai ni mkono wa baunsa.

Waziri Gwajima amesema Askofu amejigeuza msemaji wa sekta ya afya na kulitaka Jeshi la Polisi na Takukuru wamuite atoe maelezo ya chanjo feki alizosema pia atoe ushahidi wa yeye waziri Gwajima na Rais kupewa pesa.
================

Waziri Dorothy Gwajima: Tumepata walimu waliosomea kwenye mitandao wakajipa vyuo vikuu kama ndugu yangu anayeitwa askofu Gwajima. Yule ni shemeji yangu lakini mitazamo, sera, imani na itikadi tofauti.

Mimi sifungamani na mtu kwasababu eti shemeji yangu. Mimi waziri wa afya, nimeapa kwa viapo vya Amiri Jeshi mkuu na Majeshi yote, wewe ni mume wangu, shemeji yangu, mjomba wangu, ni dada yangu unaleta za kuleta, ninakuambia hiyo hapana na nanyanyua sheria zikushughulikie.

Habari ya kutuambia sisi zile chanjo zimewekwa vitu havieleweki, eti mule ndani zina sumaku. Sasa leteni hizo sumaku muweke hapa, mimi nimeshachanja hapa, muje muweke. Shilingi muweke, balbu muweke maana mimi nimetangaza milioni mbili kwa mtu ambae atachanjwa balbu iwake, nimekaa nazo mpaka nimeshakula laki tano, imebaki milioni moja na nusu.

Gwajima.jpg

Mtu ameanzisha kanisa lake, ndo kanisa mibara ya waziri wa afya, yeye ndio msemaji mkuu wa sekta ya afya, anatetea watanzania kuliko mama Samia Suluhu alieapa kwa majeshi yote na sheria zote, yeye ndio mtetezi wa watanzania.

Lakini watanzania sijui huwa mnasahau vipi haya mambo, huyu sio ndio alisema atamfufua Amina Chifupa! Yuko wapi sasa? Huyu si ndio aliewaambia hataki ubunge cheo kidogo akauchukua!

Lakini si huyu aliekutwa na yule mrembo, akasema mkono wa baunsa! Lakini huyu si yeye yule aliekuwa CCM akaenda CHADEMA sasa hivi anasema yuko tayari kurudi, arudi tena CHADEMA!

Hoja zake za kisayansi zimeshajibiwa na wanasayansi wote labda kama hamfatilii, yuko yeye pamoja na wenzake.

Sasa mimi kwa dhamana niliyonayo kama waziri wa afya nimechoka kuvurugiwa wizara, naelekeza Majeshi yote ya Polisi na Takukuru waende wakatumie sheria zao wamuite awaeleze maana kwamba amesema pesa pesa pesa.

images (1).jpeg

Mimi waziri wa Afya na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tumepigwa pesa pesa pesa, chanjo ziingie. Sasa yeye si anajua, alikuwa shahidi, alikuwa anatuchungulia, atutajie na alietupa na tulipokelea wapi na yeye alikuwa yuko wapi chini ya sheria ya Takukuru na leo nitasaini tamko langu, La sivyo tutaendelea kuchezeana sana hii nchi.

Amesema chanjo ni feki, chanjo feko zinathibitishwa kisayansi, akatuletee ile batch number ambayo ni feki ni batch ipi na ziko wapi? Kachomwa nani? Tufanye hivi vitu kisheria!

Hatuwezi tukawa na Serikali ambayo mtu anajinyanyua tu anampita na Rais, mara anaitwa Rashid, mara anaitwa Gwajima, mimi sielewi yeye yuko wapi alafu anavuruga vuruga, tunaacha mambo, tunasumbuana kama vile nchi hii haina sheria.

Kwahiyo tunahitaji Gwajima Askofu popote ulipo, nasimama kama waziri wa Afya wa nchi hii, ukatutafutie na kututhibitishia hiyo chanjo ambayo ni fake tuipeleke kwa mkemia mkuu, kama wa Dar es Salaam humuamini twende Nairobi, twende Naijeria, twende kokote tukathibitishe kwamba hizi ni fake.

Na wale waliochanjwa feki ututajie, ututajie twende tukawachukue, tuwapeleke maabara tuchukue damu zao, tuangalie kama anti bodies waliotakiwa kuzalishwa na johnson and johnson wamezalishwa ama hawajazalishwa.

PIA, Soma

=▷ Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia

=▷ Serikali yaagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

=▷ IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

Kwani na sisi tukimuuliza dokta Gwajima si ni yeye alisema tujifukize na kupiga nyungu mpaka akatengeneza video yeye na mumewe kutuhamasisha Watanzania?

Imekuwaje sasa amebadili gear angani? Au kwasababu bwana yule amesha resti in pisi?
 
Kwani na sisi tukimuuliza dokta Gwajima si ni yeye alisema tujifukize na kupiga nyungu mpaka akatengeneza video yeye na mumewe kutuhamaisha Watanzania?

Imekuwaje sasa amebadili gear angani? Au kwasababu bwana yule amesha resti in pisi?
Hahaha, na sisi wananchi tumshangae.. si ni yeye alituaminisha kujifukiza ndio mpango mzima tukawaacha wanasayansi.. inakuaje tumuamini bado!
 
Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji.

Waziri huyo amewashangaa wananchi wanaomuamini “huyu shemeji yangu Askofu Gwajima, hivi si ni yeye alisema atamfufua Amina Chifupa, Je alimfufua? Hivi si ni yeye alisema ubunge ni jambo dogo hawezi kuwa mbunge lakini hivi sasa ni mbunge. Hivi si ni yeye alikutwa na mrembo akasema ni mkono wa baunsa.. inakuwaje mnamuamini bado.”
Siasa zinaenda vuruga familia Sasa, kitakachofuata ukoo wa Gwajima watamtenga waziri, waziri umechemka, hiyo ngoma ungemuachia naibu wako halafu wewe unabaki pembeni ukinywa maji ya Kilimanjaro.

Wewe si unaona boss wako anatoa pasi kali KWA washambuliaji wa Chadema Halafu anakaa pembeni Kama vile haoni
 
Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji.

Waziri huyo amewashangaa wananchi wanaomuamini “huyu shemeji yangu Askofu Gwajima, hivi si ni yeye alisema atamfufua Amina Chifupa, Je alimfufua? Hivi si ni yeye alisema ubunge ni jambo dogo hawezi kuwa mbunge lakini hivi sasa ni mbunge. Hivi si ni yeye alikutwa na mrembo akasema ni mkono wa baunsa.. inakuwaje mnamuamini bado.”
Hili beef naliona litaingia hadi kwenye familia hizi mbili, Watoto kwanza ndiyo wataanza kuchukiana! Nawashauri wote wawili walimalize mapema kabla Moto haujafika mbali!!
 
Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji.

Waziri huyo amewashangaa wananchi wanaomuamini “huyu shemeji yangu Askofu Gwajima, hivi si ni yeye alisema atamfufua Amina Chifupa, Je alimfufua? Hivi si ni yeye alisema ubunge ni jambo dogo hawezi kuwa mbunge lakini hivi sasa ni mbunge. Hivi si ni yeye alikutwa na mrembo akasema ni mkono wa baunsa.. inakuwaje mnamuamini bado.”
Doroth amepiga pale pale kwenye mshono
 
Back
Top Bottom