Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, alidai atamfufua Chifupa pia alikutwa na Mrembo akasema mkono wa Baunsa

Waziri Gwajima: Askofu Gwajima ni shemeji yangu, alidai atamfufua Chifupa pia alikutwa na Mrembo akasema mkono wa Baunsa

Huyu Dorothea amuulze Makonda kilichomkuta pindi alipotaka kupambana na Askofu
 
Waziri wa Afya, Dkt Gwajima leo ameelezea suala askogu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kupinga chanjo ya Covid-19 na kudai pamoja na ushemeji walionao haungani na itikadi zake.

Pia ameshangaa wanaomuamini akitolea mfano wa Askofu kudai atamfufua Amina Chifupa kitu ambacho hajatimiza mpaka sasa. Pia amemshangaa kuchukua ubunge ilhali alishasema ni cheo kidogo kwake.

Mwisho Dkt Gwajima amemshangaa askofu Gwajima kukutwa na mrembo na kuiita mkono wa baunsa.

Waziri Gwajima amesema Askofu amejigeuza msemaji wa wizara ya afya na kulitaka Jeshi la Polisi na Takukuru wamuite atoe maelezo ya chanjo feki alizosema pia atoe ushahidi wa yeye waziri Gwajima na Rais kupewa pesa.
================

Waziri Gwajima: Tumepata walimu waliosomea kwenye mitandao wakajipa vyuo vikuu kama ndugu yangu anayeitwa askofu Gwajima. Yule ni shemeji yangu lakini mitazamo, sera, imani na itikadi tofauti.

Mimi sifungamani na mtu kwasababu eti shemeji yangu. Mimi waziri wa afya, nimeapa kwa viapo vya Amiri Jeshi mkuu na majeshi yote na Majeshi yote, wewe ni mume wangu, shemeji yangu, mjomba wangu, ni dada yangu unaleta za kuleta, ninakuambia hiyo hapana na nanyanyua sheria zikushughulikie.

Habari ya kutuambia sisi zile chanjo zimewekwa vitu havieleweki, eti mule ndani zina sumaku. Sasa leteni hizo sumaku muweke hapa, mimi nimeshachanja hapa, muje muweke. Shilingi muweke, balbu muweke maana mimi nimetangaza milioni mbili kwa mtu ambae atachanjwa balbu iwake, nimekaa nazo mpaka nimeshakula laki tano, imebaki milioni moja na nusu.


Mtu ameanzisha kanisa lake, ndo kanisa mibara ya waziri wa afya, yeye ndio msemaji mkuu wa sekta ya afya, anatetea watanzania kuliko mama Samia Suluhu alieapa kwa majeshi yote na sheria zote, yeye ndio mtetezi wa watanzania.

Lakini watanzania sijui huwa mnasahau vipi haya mambo, huyu sio ndio alisema atamfufua Amina Chifupa! Yuko wapi sasa? Huyu si ndio aliewaambia hataki ubunge cheo kidogo akauchukua!

Lakini si huyu aliekutwa na yule mrembo, akasema mkono wa baunsa! Lakini huyu si yeye yule aliekuwa CCM akaenda CHADEMA sasa hivi anasema yuko tayari kurudi, arudi tena CHADEMA!

Hoja zake za kisayansi zimeshajibiwa na wanasayansi wote labda kama hamfatilii, yuko yeye pamoja na wenzake.

Sasa mimi kwa dhamana niliyonayo kama waziri wa afya nimechoka kuvurugiwa wizara, naelekeza Majeshi yote ya Polisi na Takukuru waende wakatumie sheria zao wamuite awaeleze maana kwamba amesema pesa pesa pesa.

View attachment 1895930

Mimi waziri wa Afya na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tumepigwa pesa pesa pesa, chanjo ziingie. Sasa yeye si anajua, alikuwa shahidi, alikuwa anatuchungulia, atutajie na alietupa na tulipokelea wapi na yeye alikuwa yuko wapi chini ya sheria ya Takukuru na leo nitasaini tamko langu, La sivyo tutaendelea kuchezeana sana hii nchi.

Amesema chanjo ni feki, chanjo feko zinathibitishwa kisayansi, akatuletee ile batch number ambayo ni feki ni batch ipi na ziko wapi? Kachomwa nani? Tufanye hivi vitu kisheria!

Hatuwezi tukawa na Serikali ambayo mtu anajinyanyua tu anampita na Rais, mara anaitwa Rashid, mara anaitwa Gwajima, mimi sielewi yeye yuko wapi alafu anavuruga vuruga, tunaacha mambo, tunasumbuana kama vile nchi hii haina sheria.

Kwahiyo tunahitaji Gwajima Askofu popote ulipo, nasimama kama waziri wa Afya wa nchi hii, ukatutafutie na kututhibitishia hiyo chanjo ambayo ni fake tuipeleke kwa mkemia mkuu, kama wa Dar es Salaam humuamini twende Nairobi, twende Naijeria, twende kokote tukathibitishe kwamba hizi ni fake.

Na wale waliochanjwa feki ututajie, ututajie twende tukawachukue, tuwapeleke maabara tuchukue damu zao, tuangalie kama anti bodies waliotakiwa kuzalishwa na johnson and johnson wamezalishwa ama hawajazalishwa.


View attachment 1895773
Huyu Waziri wa Afya kama Bi Kidude
 
Jumapili hii kitawaka....hii itakuwa tetra manifestation
 
Kwenye hii battle ya gwajimazi,

Askofu Gwajima hatuboi kwa shemeji yake ambaye ni waziri wa afya Dr. Gwajima.

Huyu mama sio wa mchezo mchezo..atakuwa amelelewa pwani huyu.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hii iko Tanzania tu!. Waziri wa Afya tena mtaalamu katika fani hiyo anaacha kupambana na gonjwa la UVICO badala yake akidhani anajibu hoja anajiingiza kwenye malumbano na mchungaji anayeshawishi waumini wake juu ya chanjo ya UVICO, tena kwa kujaribu kutumia isivyo vyombo vya Dola kulinda maslahi yake binafsi.....Aibu gani hii?.😳
 
Hii nchi ya Tanzania ina Ujinga mwingi sana
 
Bongo bwana Kila kitu easy tu,
Hii nchi Kila kukicha Kuna episode mpya za comedy,yaani licha ya matatizo yetu Kama nchi ila kwenye vituko hatujambo yaani utakuta jambo la serious linageuka Futuhi na kuundiwa Memes eg swala la tozo liligeuka kua kituko pale Mwiguluiza Nchembazimana aliposema tuhamie Burundi,Mbowe the Taliban boy a.k.a Gaidi,ukiachana na ya Mzee mpili uwiiiiiii Leo ni Gwajimas reality show live!
Keep watching!
 
The battle of unconventional methods loading.......
IMG_20210817_220019.jpg
 
Hii ngoma nzito, kipindi cha bashite Gwajiboy alirusha makombora mazito bila kupata kashkash yoyote toka kwa mpinzan, lakini safari hii mpinzani katupa kombora pia haya yetu macho na masikio Gwajiboy atajibu nini jpili.

Ila huyu Doroth angempuuza tu uyo jamaa, hapo ni kama kachokoza moto wa kifuu, yule kiumbe atatema nyongo sana hanaga stara yule ohooo
 
Yaani Sirro unamaana kauli ya waziri haitoshi mpaka aandike official letter?
Kabisa waziri katoa tamko halitekelezwi au ndiyo tuseme Gwajiboy anaogopwa? Akina Mbowe huwa wanakamatwa halafu ndiyo mnaanza uchunguzi manake huwa mahakamani mnasemaga uchunguzi haujakamilika lakini watu wanakuwa ndani tayari, kwanini msimkamate kama alivyoagiza waziri then ndiyo mchunguze kama ana jinai au la.
GWAJIBOY IS UNTOUCHABLE.[emoji123][emoji123]
IMG_20210818_000150.jpg
 
Wabongo mna shida,kwa hiyo hujasoma kulichoandikwa au hujamsikia waziri wa afya alipoongea na kujibu hoja za Ngwajiboy? Hoja zenyewe asilimia kubwa ni upuuzi unaopingana na sayansi ambayo anajaribu kuizungumzia,hana point ya maana,lakini yote yashajibiwa.

mkuu unaelewa maana ya kinga?
 
Waziri wa Afya, Dkt Gwajima leo ameelezea suala askogu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kupinga chanjo ya Covid-19 na kudai pamoja na ushemeji walionao haungani na itikadi zake...
Rubbish tupu.
 
Back
Top Bottom