Waziri Gwajima atoa pole kifo cha Graison, mtoto wa Chief Godlove Dodoma, ataka ulinzi kwa watoto

Waziri Gwajima atoa pole kifo cha Graison, mtoto wa Chief Godlove Dodoma, ataka ulinzi kwa watoto

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima ametoa pole kwa wazazi wa mtoto Graison Kanyenye aliyeuawa na watu wasiojulikana, huku akiwataka wazazi au walezi kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto.

Screenshot 2024-12-27 110119.png

Tukio hilo lilitokea Ilazo Extension jijini Dodoma Desemba 25, 2024, wakati mfanyabiashara Zainab Shaban maarufu Jojo alipomuacha mtoto huyo nyumbani kwa rafiki yake wa kiume ambaye ni Ofisa Uvuvi Mtera, Hamis Mpeta.

Pia, Soma: Dodoma: Mtoto wa miaka 6 auawa kikatili na watu wasiojulikana

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi, tukio hilo lilitokea Desemba 25,2024 saa 1.00 asubuhi ambapo Mpeta akiwa na mama wa mtoto Zainab walibaini mtoto huyo kuuawa baada ya kurejea kutoka matembezini.

"Walimkuta mtoto huyo akiwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na shingoni amekatwa na kitu chenje nja kali. Katika tukio hilo ni kwamba mama wa mtoto alimwacha chini ya uangalizi dereva bodaboda anayejulikana kwa jina la Kelvin Gilbert."
Screenshot 2024-12-27 110457.png

Katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari leo Ijumaa Desemba 27, 2024, Dk Gwajima amesema wizara yake imepokea kwa taarifa hizo za masikitiko kwa simanzi kubwa kutokana na mtoto huyo kukatishwa uhai wakati ndiyo kwanza alikuwa anaanza safari ya ndoto za maisha yake.
 
Back
Top Bottom