#COVID19 Waziri Gwajima: IGP Sirro yupo sahihi, wanaonichonganisha nitawavua nguo hadharani. Asema Corona imesababisha vifo vya kutosha

Battle linaendelea, hakijaharibika kitu, Waziri Gwajima amempongeza IGP simon Sirro kwa kufanya kazi kwa utaratibu hivyo nae amesema tayari ameshamwandikia malalamiko yake.

CORONA IMESABABISHA VIFO VYA KUTOSHA
Izi ngojera nazo zimetuchosha, mpaka mda huu sioni shida ,chanjo tulisha sema Sio lazima ambae hataki Basi abaki yeye ila asipotoshe wengine,

Sasa hii ya mtu na shemeji yake yamekua MAIGIZO, ni swala la serikali kumtaka Gwajima kuacha kupotosha Basi, maana halazimishwi mtu kuchanja, Sasa mnaanza michambano, Mara mkono wa baunsa , enzi za usichana wake WENDA uyu mama Tabia ya kusutana alikua nayo sana
 
Sirro ameshasema kuwa haoni jinai, yaani Rais wa nchi kushutumiwa kupokea rushwa kwa Sirro haina shida
Kwani Rais hajachukua pesa za msaada sijui mkopo wa covid kwa masharti ya kutoa takwimu? Au hatukuona wakati wanasainiana na hao wenye pesa zao?
 
Mjadala umeisha lakini askofu anapotumia kanisa kuanzisha mjadala anakua kama anauamsha upya
 
Hii nchi ukiwa timamu ni ngumu sana kuishi
 
Mambo ya msingi ni ni kupunguza ongezeko la tozo za miamala ya simu isiyohimilika na wananchi tulio wengi, jambo la msingi lingine ni ongezeko la bei za nishati ya umeme( watu wanaotumia umeme kidogo kwa mwezi sasa wanatozwa hela sawa na wanaotumia umeme mwingi), ongezeko la bei za mafuta zinazopanda kwa namna wauzaji wanavyojisikia , na jambo lingine la msingi ni ongezeko la bei za pembejeo a kilimo.

Lema yupo Canada hawezi kujua mambo ya msingi yanayotugusa moja kwa moja raia wengi wa Tanzania. Nina mengi ila ngoja niishie hapa.
 
Tumeshasema, na hatutachoka kusema, hatuko tayari kufanyiwa majaribio, mtatuelewa tu.
 
Jasusi la Mbinguni. Waziri anaahidi kumvua mtu nguo hadharani? Hii ni attack au lugha mbaya!! Basata mko wapi

hicho ni kiswahili kama ni mpungufu wa tafsjda ya kiswahili utapata taaabu sana kuelewa alikua na maana gani
 
Bei ya mafuta imeongezeka kutokana na ongezeko la bei duniani ata wakitoa sh 100 itabaki 2300 ambayo bado ni bei kubwa , mbolea nayo imeongezeka kutokana na ongezeko la bei duniani
 
Viongozi vigeugeu hawatufai, Huyu Waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima amegeuka kichekesho, Baada ya IGP Siro kusema hawezi mkamata mtu bila barua na Serikali inafanya kazi kwa maandishi, Dkt Gwajima Waziri wa afya amekanusha kauli yake kuwa Yeye alisema Mchungaji Gwajima ahojiwe na sio kukamatwa

Hawa viongozi wanasoma upepo walisema chanjo hazifai zimetengenezwa haraka, Leo chanjo zinafaa

Hivi lengo la viongozi wa namna hii ni kulipeleka wapi Taifa?

Dakika moja wanakuwa vigeugeu

Naambatanisha video yake ya kukanusha
Your browser is not able to display this video.
 
She is right
 
Naye Siro ni Kigeugeu pia. Mara ngapi amewakamata Watu kwa kuagizwa tu hata na Katibu Kata Mwenezi wa CCM? Sema kaona Gwajima ni MCCM
 
Huyu mama ni mweupe kabisa kichwani,hana msimamo ndiyo maana Chidboy anamchana live.
 
Huyu kakutana na mtiti wa mawifi, lazima awe mpole vinginevyo anaweza kuhemea mahali pa kulala.....chezea mawifi wewe..
 
Ndo maana alitestiwa mitambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…