#COVID19 Waziri Gwajima: Kanda ya Ziwa, Kilimanjaro kumeathirika zaidi na Corona

#COVID19 Waziri Gwajima: Kanda ya Ziwa, Kilimanjaro kumeathirika zaidi na Corona

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa mujibu wa Dkt. Gwajima, huku kumeathirika zaidi:

“Maeneo ya kanda ya ziwa pamoja na Kilimanjaro yameathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo, na ilihitajika mitungi ya ziada kutokana na eneo la kanda ya ziwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo,” alisema Gwajima."

Mwenye masikio na asikie:

“Nataka hapo wananchi watuelewe, tuvae barakoa, tunawe mikono na maji tiririka pia tujiepushe na misongamano isiyo ya lazima. Katika wakati huu hakuna ulazima wa mtu kwenda katika miziki au kupanda katika gari lililojaza watu,” amesisitiza Dk Gwajima."

--------
My take:

Tahadhari zaidi maeneo hayo ikiwamo kupunguza safari zinazoweza kuepukika, kutoka au kwenda maeneo hayo ni jambo la busara zaidi.
 
Daladala.
Mwendokasi.
Pantoni.
Viwanja vya mipira.
Masokoni.

Yani mtu ni mpinzani wa serikali anataka COVID itambulike vizuri lakini.
Hataki level seat ktk daladala,Hataki kupunguza mikusanyiko ktk Masoko.

In short wengi hao wanaleta maslahi binafsi.Nani kakwambia hizi tahadhari zikiwekwa zitamuacha mtu salama?
Hata hao watumishi wategemee kuyumba kwa mishahara yao na per diem,Semina ya posho nayo yote itapukutika labda sekta ya afya tu.
Hapo ndo utarudi na kusema kweli njia ya JPM ilikua ni busara kubwaa kwa nchi za Kimaskini.
 
Huko Kilimanjaro watu wanapuputika kweli, Bora serikali ilete tu hizo chanjo maana Hali si nzuri na watu hawachukui tahadhari ka kipindi coronavirus ilivoingia
... siasa ziliingia zika-braiwash watu wakadhani kwa kuwa kiongozi mkubwa kasema hakuna Corona basi ni kweli hakuna Corona. Sijui watanzania ujinga utatutoka lini tuweze kupima vitu kwa uhalisia wake na kuuona ukweli badala ya kusikiliza maneno ya wanaoitwa viongozi mengine yakiwa ya kilaghai. Ona sasa katuachia msala watu wamekuwa wajinga kabisa hata kuamini maelekezo ya wataaalamu imekuwa tatizo.
 
Daladala.
Mwendokasi.
Pantoni.
Viwanja vya mipira.
Masokoni.

Yani mtu ni mpinzani wa serikali anataka COVID itambulike vizuri lakini.
Hataki level seat ktk daladala,Hataki kupunguza mikusanyiko ktk Masoko.

In short wengi hao wanaleta maslahi binafsi.Nani kakwambia hizi tahadhari zikiwekwa zitamuacha mtu salama?
Hata hao watumishi wategemee kuyumba kwa mishahara yao na per diem,Semina ya posho nayo yote itapukutika labda sekta ya afya tu.
Hapo ndo utarudi na kusema kweli njia ya JPM ilikua ni busara kubwaa kwa nchi za Kimaskini.
... mashuleni na vyuoni? Hawa watoto wanaambukizana huko halafu jioni wanawapelekea wazazi wao! Dah; hatari sana!
 
... siasa ziliingia zika-braiwash watu wakadhani kwa kuwa kiongozi mkubwa kasema hakuna Corona basi ni kweli hakuna Corona. Sijui watanzania ujinga utatutoka lini tuweze kupima vitu kwa uhalisia wake na kuuona ukweli badala ya kusikiliza maneno ya wanaoitwa viongozi mengine yakiwa ya kilaghai. Ona sasa katuachia msala watu wamekuwa wajinga kabisa hata kuamini maelekezo ya wataaalamu imekuwa tatizo.
Yeye aliwaambia kuwa Corona haipo imeletwa na mabeberu na watu wameacha kuchukua tahadhari na sikuhizi hawanawi ila watu wengi wamekufa Sana na ya Sasa ni mbaya kuliko janauri imagine kijijini kwa siku wanaweza zikwa watu hata watano, nadhani wizara ya afya na yenyewe imelala haichukua hatua nzuri ka ummy alivoweza kuhamasisha
 
Back
Top Bottom