#COVID19 Waziri Gwajima: Kanda ya Ziwa, Kilimanjaro kumeathirika zaidi na Corona

#COVID19 Waziri Gwajima: Kanda ya Ziwa, Kilimanjaro kumeathirika zaidi na Corona

Daladala.
Mwendokasi.
Pantoni.
Viwanja vya mipira.
Masokoni.

Yani mtu ni mpinzani wa serikali anataka COVID itambulike vizuri lakini.
Hataki level seat ktk daladala,Hataki kupunguza mikusanyiko ktk Masoko.

In short wengi hao wanaleta maslahi binafsi.Nani kakwambia hizi tahadhari zikiwekwa zitamuacha mtu salama?
Hata hao watumishi wategemee kuyumba kwa mishahara yao na per diem,Semina ya posho nayo yote itapukutika labda sekta ya afya tu.
Hapo ndo utarudi na kusema kweli njia ya JPM ilikua ni busara kubwaa kwa nchi za Kimaskini.

Umeandika kama ulikuwa kwenye boda boda na njia ni fulu mashimo.

Tokea wapi? Au tokea pande za buseresere mkuu?
 
Sina uelewa wa kanda zote.

Hapa tunazungumzia kanda ya ziwa.
Hata hii pia huijui
kanda ya ziwa.png
 
Wanajitahidi IMF wanazidi kubada screw kuongeza masharti ya kupewa msaada wa corona. Hii yote ni kampeni ya kutegeneza mazingira ya huo msaada. Na IMF waongeze masharti zaidi na ndio njia ya kuadabisha wasio na misimamo wanao sukwasukwa na upepo na kutapakaa kama majani ya miti makavu.
 
Dr. Gwajima basi wekeni lockdown huko kanda ya ziwa na kilimanjaro !

Kuhusu hilo waziri amekutangulia mkuu:

Kuhusu suala la “ Lockdown” Waziri Gwajima alisema Tanzania haina mpango wa kuweka wananchi wake “Lockdown” na kusisitiza kuwa watawekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Sikia Chaggadema, mimi kwetu ni MARA.

Shinyanga siyo mkoa ulioko kanda ya ziwa.

Kanda ya ziwa ni Kagera, Mara, Mwanza na Geita.

Kwahiyo wewe unameza kila unachokiona humu JF?

chagga dema jina zuri ulitakiwa ujengewe sanamu lako tunaomba tutumie jina hili chaggadema
 
Hao watu wanaodondoka sana ni wangapi?

Kwa ugonjwa gani? Lini? Wapi? Saa ngapi? Umejuaje?

We ni mchawi au nabii?
Wewe huna akili. Unabisha tu. Kwani kuugua Corona ni aibu ?!. Corona si kaswende wala gonorhea uone aibu. Ni ugonjwa wa mlipuko tena usioangalia ukada wako. Muulize Jiwe aliyeibeza
 
Wanajitahidi IMF wanazidi kubada screw kuongeza masharti ya kupewa msaada wa corona. Hii yote ni kampeni ya kutegeneza mazingira ya huo msaada. Na IMF waongeze masharti zaidi na ndio njia ya kuadabisha wasio na misimamo wanao sukwasukwa na upepo na kutapakaa kama majani ya miti makavu.
Kwamba hakuna maambukizi ya Corona? Kwamba hizi taarifa na wale wagonjwa hospitali ni wa kuigiza? Mama hana roho ya kutoa watu roho, JIWE alikuwa na roho ya damu, hakujali watu kufa.
 
Waziri kaachana na ule upumbavu wa awamu ya tano wa kutumia kachumbari kama dawa ya Corona na kudanganya eti mabeberu hayatupendi yametuletea Corona.
 
Kuhusu hilo waziri amekutangulia mkuu:

Kuhusu suala la “ Lockdown” Waziri Gwajima alisema Tanzania haina mpango wa kuweka wananchi wake “Lockdown” na kusisitiza kuwa watawekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Waambie wako Watanzania kati ya hawa 60M miili yao ni hekalu la Holy Ghost. Wasije ichezea kwa hiyo chanjo yao wabayo iagiza. Mungu wa Mbinguni hata wacha salama awaangalie wakichezea mahekalu yake atawaharibu wao, 1 Wakorintho 3:16-17.
 
Wanajitahidi IMF wanazidi kubada screw kuongeza masharti ya kupewa msaada wa corona. Hii yote ni kampeni ya kutegeneza mazingira ya huo msaada. Na IMF waongeze masharti zaidi na ndio njia ya kuadabisha wasio na misimamo wanao sukwasukwa na upepo na kutapakaa kama majani ya miti makavu.

Kulikuwa na mawazo haya:

IMG_20210706_203616_157.jpg

Unaonaje kama tungeachana na sintofahamu hii ya mikopo na misaada, ili tupambane na gonjwa hili bila ya kuhusianisha pesa?
 
Mwongo huyu mbona hatuoni kitu? Huku hata huo umbea hamna tunasikia tu kwenye mitandao, huu ugonjwa wa kuleta mnaukuza sana. Eti walipungikiwa mitungi? Aiseee siasa mbaya.
Hawa jamaa wako njema sana kwa proganda, hali ni tofauti kabisa na mitandaoni na matamko yanayotoka.
Na kama hali ingekuwa mbaya kweli sidhani kama ziara za mikoani na press conference zingekuwa zinafanyika wakati huu.
 
Yeye aliwaambia kuwa Corona haipo imeletwa na mabeberu na watu wameacha kuchukua tahadhari na sikuhizi hawanawi ila watu wengi wamekufa Sana na ya Sasa ni mbaya kuliko janauri imagine kijijini kwa siku wanaweza zikwa watu hata watano, nadhani wizara ya afya na yenyewe imelala haichukua hatua nzuri ka ummy alivoweza kuhamasisha
Kijiji gani hicho na kiko mkoa gani mkuu?
 
Back
Top Bottom