Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tukio la video ya mtoto akiadhibiwa vikali na mama yake, lililopostiwa na mwanahabari Tweve Devota kupitia mtandao wa X, limezua taharuki mtandaoni. Mama huyo, anayeishi Mbezi Mwisho, Dar es Salaam, anadaiwa kumtesa mtoto wake mara kwa mara.
Dkt. Gwajima D , Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, alijibu kwa haraka kupitia mtandao wa X, akiahidi kuchukua hatua mara moja. Alitoa mwaliko wa ushirikiano kutoka kwa mtoa taarifa ili timu yake ifike eneo hilo haraka na kumsaidia mtoto huyo.
Majibu ya Waziri Dorothy Gwajima yalionyesha uwajibikaji wa dhati wa ofisi yake, akisisitiza kwamba visa vya ukatili kwa watoto haviwezi kuvumiliwa na kwamba hatua stahiki lazima zichukuliwe kwa ushirikiano wa jamii.
Soma, Pia: Waziri Gwajima chukua hatua kwa ukatili huu aliofanywa mtoto shule ya Msingi Kitefu, Halmashauri ya Meru