Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa

Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa

Kweli nyakati zimebadilika wakati tunakuwa tumechezea kichapo kweli ingekuwa wakati zama hizi kumbe wazazi walikuwa wanaenda selo
Maisha yanabadilika, enzi sisi tunachezea kichapo ni kama kina baba na mama walikua wanaambizana walee vipi.

Kila nyumba baba anaogopwa, baba fulani anaweza kukuchapa na huwezi kumsema kwa baba yako maana nae baba yako atakuongezea kichapo.

Siku hizi mbinu za kuwadhibiti watoto ni nyingi sio kipigo tu, watoto wenyewe lojolojo hawa na hapa mjini mabazazi ni wengi hayachelewi kumrubuni na akatokomea nayo.
 
Sasa Kwan Kuna shida gan hapo? Mbona ameadhibiwa Kawaida sana ? Yaan sku hizi taifa la kiherere sana !!! Wakiachwa mnaanza kua malezi mabaya Aya wakiadhibiwa umbeya Tena!!
Shida inaweza ikawepo,ila inatakiwa wasiende kwa pupa.Wadadisi ni nini hasa kinamfanya mama amwadhibu mwanae vikali hivyo.

Kama kweli kuna kosa sugu kafanya,ni sahihi tu maana wengine unajua tumekua kwa vipigo vikali ni basi tu Mungu alikua upande wetu hatujapata majeraha ya kudumu enzi zetu karne ya 20😂
 
Kwa kweli Karne ya 20 ilikuwa ni shida tupu hakuna Smartphone, Tv za kuhesaba, ndio kipindi AIDS inafanya unyama wake kimsingi tumshukuru mungu kwa uhai na kushuhudia Aya mabadiliko katika Kila nyanja
 
Unakuta huyo mama ni single mother anaishi na huyo mtoto Baba hajulikani alipo.
Mama anakamatwa anakwenda jela, malezi ya mtoto inakuaje huku nyuma? Nimejiuliza tu.
Tukiangalia kila kosa kwa staili hii hata wauaji tuwaachia huru

Huyu mama akamatwe na ashtakiwe sijui sheria zinasemaje ila km inawezekana antang'anywe huyo mtoto mpaka itakapothibitika atamlea bila kumfanyia ukatili
 
Kama mtoto hasikii na ni mtukutu, dawa siyo kusimika mfumo wa kumpiga, ni kwenda kliniki ya ustawi wa jamii ya marekebisho ya tabia. Ahsante kwa swali zuri
Katungeni sheria ya kuwanyang'anya watoto wazazi wa aina hii. Sijui kama hiyo sheria ipo!

Mzazi mlevi, katili na anayelea mtoto katika mazingira hatarishi anyang'anywe mtoto ikiwa ni pamoja na hatua za jinai kuchukuliwa dhidi yake.

Kama huyu unaweza kushangaa amekamatwa halafu akatoka sijui huko jela akaendeleza ukatili wake kwa mtoto!

Kwanza atafungwa kweli huyu?? na maukatili yake yote haya!
 
Kama mtoto hasikii na ni mtukutu, dawa siyo kusimika mfumo wa kumpiga, ni kwenda kliniki ya ustawi wa jamii ya marekebisho ya tabia. Ahsante kwa swali zuri
Vizuri lakini ni vyema mkatupa muongozo wa hicho kinachofanyika ustawi wa jamii kurekebisha tabia ili tuweze kuwarekebisha watoto wetu maana ni sisi tunaokuwa nao nyumbani tena kwa muda mrefu mpaka wanapoanza kujitambua
 
Katungeni sheria ya kuwanyang'anya watoto wazazi wa aina hii. Sijui kama hiyo sheria ipo!

Mzazi mlevi, katili na anayelea mtoto katika mazingira hatarishi anyang'anywe mtoto ikiwa ni pamoja na hatua za jinai kuchukuliwa dhidi yake.

Huyu anaweza kukamatwa halafu akatoka sijui huko jela akaendeleza ubabe wake!

Kwanza atafungwa kweli huyu?? na maukatili yake yote haya!
mtoto nani atamlea??
 
Back
Top Bottom