Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa

Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa

Tukio la video ya mtoto akiadhibiwa vikali na mama yake, lililopostiwa na mwanahabari Tweve Devota kupitia mtandao wa X, limezua taharuki mtandaoni. Mama huyo, anayeishi Mbezi Mwisho, Dar es Salaam, anadaiwa kumtesa mtoto wake mara kwa mara.
Dkt. Gwajima D , Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, alijibu kwa haraka kupitia mtandao wa X, akiahidi kuchukua hatua mara moja. Alitoa mwaliko wa ushirikiano kutoka kwa mtoa taarifa ili timu yake ifike eneo hilo haraka na kumsaidia mtoto huyo.
Majibu ya Waziri Dorothy Gwajima yalionyesha uwajibikaji wa dhati wa ofisi yake, akisisitiza kwamba visa vya ukatili kwa watoto haviwezi kuvumiliwa na kwamba hatua stahiki lazima zichukuliwe kwa ushirikiano wa jamii.
Soma, Pia: Waziri Gwajima chukua hatua kwa ukatili huu aliofanywa mtoto shule ya Msingi Kitefu, Halmashauri ya Meru

Mama mwenyewe anahitaji elimu ya malezi na msaada kulea watoto ana stress sana.
 
Kweli nyakati zimebadilika wakati tunakuwa tumechezea kichapo kweli ingekuwa wakati zama hizi kumbe wazazi walikuwa wanaenda selo
Kichapo cha kawaida kabisa hiko ,wangemuona mama yangu ( alale salama ) enzi hizo basi angekuwa jela sahv maana hiko kichapo hata robo hakifikii ,huyo mtoto kachapwa kikawaida sana
 
mara nyingi watu wa hivo wana stress sina hakika kama baba yuko
Niko pamoja nawe, lakini kwanini mzazi Stress zake zimsababishie maumivu mtoto badala ya kumtafuta mwenza wake na kugombana nae!? It doesnt make any sense!
 
Back
Top Bottom