Tunapoongelea mafanikio ya awamu ya 6.
Hatuwezi kuacha kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassa kwa Moyo wake Mtulivu wa kufikiria kuunda hii Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, pamoja na kumteua Mhe Dr Dorothy Gwajima kuwa engine ya wizara hii.
Kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo jirani wanajua vizuri tatizo la watoto waishio mitaani wanaotumikishwa kuombaomba jinsi lilivyokuwa kubwa hasa maeneo ya City Centre.
Miaka mitatu iliyopita kuanzia Fire [emoji91] ukiwa unapita Morogoro Road unaenda posta ama K/koo, Utakutana na kundi kubwa la watoto wanaoomba barabarani.
Ukipita hii barabara ya Ally Hassan Mwinyi Road, kuanzia Namanga, St Peter, Salenda Bridge mpaka posta mpya kuelekea Ferry utakutana na rundo la watoto wetu wa Tanzania.
Vile vile ukiwa unapita barabara ya Uhuru, kuanzia Ilala Boma, Congo - K/koo, Mnazi mmoja, mchafu koge, Kitumbini/Kiautu, CBE kwenda mpaka Ferry unakutana na kundi kubwa la watoto wakiwa wamechoka wanaomba omba barabarani.
Vilevile ukiwa unatokea Pugu Road /Nyerere Road, mpaka makutano ya Bibi Titi Road na Lumumba, Clock Tower, ukiwa unaelekea Posta ama Station kote huku utakutana makundi ya watoto
Waliokata tamaa na keaho yao[emoji24]
Mbaya zaidi ukiingia posta mpya pale tu Benjamin Tower ukishuka kwa daladala ama gari yako unapokelewa kwa kuzungukwa na mikono ya watoto wengi wa kitanzania waombaomba wengine wakiwa wamelala pale kwenye Korido za Mkapa tower.
Watakupokea kwa shikhamoo za kulipia huku wananyoosha mikono yao, wakiwa wamekuzunguka na kukusindikiza kwa mita mia.
Maeneo yoote mpaka Chuo cha Ifm Ocean Road Hospital, Jimkhana Beach
Kule kote kulikuwa na watoto hao wanaotumikishwa na kujitumikisha kuchafua taswira ya taifa pamoja na kuutweza utu wao bila wenyewe kujua.
Mara tu baada ya wizara ya Maendeleo kuundwa, waziri Gwajima haraka aliunda Kamati Maalum ya Taifa (TASK FORCE). Ya kumtengamanisha huyo anayetumikishwa mtaani, huku akiwa anakosa haki zake nyingi za msingi kama binadamu.
Mara baada ya kamati hii ya taifa leo tunaona hata kule Ferry kwenye mabanda ya kukaanga samaki na kule wanapifanya mnada wa samaki wale watoto waliokuwa wakitumikishwa kupaa magamba ya samaki hawapo tena baada ya kampeni mbalimbali za uelimishaji kwa jamii.
Kamati hii inafanya kazi nyingi ikiwemo kuvijengea uwezo vituo vya kulea watoto, pia kuwajengea uwezo wazazi na walezi ili kupunguza tatizo la udumavu wa malezi, pamoja na kuwapa watoto wahanga nafasi mpya ya kurudi shule kupata haki ya elimu, watoto waliovuka umri wa miaka 14 - 16 wanapelekwa vyuo vya ufundi kupata taaluma yeyote ya ufundi kama Veta na vyuo vingine stadi.
Leo tunashuhuda za watoto wengi walionusuliwa na kamati hii kupelekwa pale kurasini kwenye makao ya Serikali ya kulea watoto.
Kuhusu wale watoto watano pale ferry kwenye banda la abiria,
Watoto wawili wanatumika na wazazi wao baba na mama yao.
Watoto wawili wanatumikishwa na Shangazi yao na mtoto mmoja anatumikishwa na Dalali ambaye analipa elfu 30000 kila jumamosi kwa mama mdogo wa mtoto huyo, ambaye yeye ndiye mlezi wa mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 10 aliyefiwa na mama yake mzazi.
Kamati ipo kazini chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii
Ikiongozwa na Jemadari wetu Dr Dorothy Gwajima Wazir.
Lkn SISI SOTE KAMA WANA JAMII TUNATAKIWA TUUNGANE KWA UMOJA WETU KUKEMEA MATENDO YOOTE YA UVUNJIFU WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO PAMOJA NA KUKEMEA UKATILI KWA BINADAMU WOOTE.