#COVID19 Waziri Gwajima: Marekani imechanja 2.4% ya watu wake na J&J

#COVID19 Waziri Gwajima: Marekani imechanja 2.4% ya watu wake na J&J

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073.

Ambapo hao milioni 8 ni sawa na 2.4% ya raia wa Marekani wote.

Kwa mtazamo wangu hii chanjo hata Wamarekani wenyewe hawaiamini sana na ndio maana idadi ya watu wake waliochanjwa ni ndogo sana.

Ningependa kujua ni chanjo gani ambayo USA wamechanja asilimia kubwa ya raia wake? Je, kwanini wasingetupatia hiyo?

Sisi tukiweza kuchanja hii yote waliyotupa tutakuwa tumechanja zaidi ya asilimia 6 ya watanzania. Lakini kwao wamekomea tu 2.4%. Hapa kuna mambo ya kujiuliza na kujiridhisha.
 
Sometimes in life, it worth to be sceptical when the rest or majority are optimistic, and to be optimistic when the rest or majority are sceptical/pessimistic.

Gwajima anaepinga chanjo anaweza kuja kuwa sahihi siku moja.

Mimi binafsi kwa sasa sijui nisimame upande gani, ila muda ndio utanipa jibu
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani.

Sasa ukiangalia population ya USA ni watu 332,915,073...
Ni Pfizer(BNT162) na Moderna (mRNA-1273)
humo ndio ile mRNA tunayolishana matango pori inakuja kutuua ndio ipo humo😂😂😂😂
 
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekan...
Pfizer ndugu yangu...ndio ambayo wamarekani wanaitumia sana...
 
Ni kweli Wamarekani wengi walioamua kupata chanjo hawakuitaka hiyo Janssen vaccine kwa kuwa efficacy yake ya 66% ndiyo ndogo ukilinganisha na Pfizer na Moderna ambazo zote efficacy ni zaidi ya 90%.
Wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson. Waziri wa Afya, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali ya Marekani imetumia chanjo hiyo kuwachanja raia milioni 8 wa Marekani...
 
Hana akili huyu mtu. Kwa nini asilimia ndogo hiyo kuliko nyingine kama hii chanjo ndio bora? Wako wa Marekani hata kuandika ni taabu tupu.

Katamka jina Kibwetere isiwe kamlenga shemeji yake. Anaona Watanzania wanaotafakari hoja zitolewazo ndio wajinga na wanadanganywa wakati yeye kaolewa huko kwenye huo ukoo.
 
Uelewa wako ni finyu sana. Alichokiongea huyo ZWAZWA na nilichoandika mimi havifanani hata chembe!!!
Nadhani hapo mnatofautiana kwenye Gwajima yupi hasa mnayebishania
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
🤣🤣🤣🤣🤣Mkuu nilichoandika hakifanani na kauli zao wote wawili. Huyo mmoja alikuwa anaongelea chemical contents za chanjo husika kama kuna daktari wa Kitanzania anayezijua. Huyo mwingine anazungumzia idadi ya Wamarekani waliochanja ya milioni 8. Mimi nilikuwa namjibu muanzisha maada kwanini percentage ya Wamarekani waliochanja hiyo Janssen ni ndogo sana.

Nadhani hapo mnatofautiana kwenye Gwajima yupi hasa mnayebishania
 
Back
Top Bottom