Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Zanzibar inatawala Tanganyika.Najiuliza sipati jibu.
Je, ni;
- Dharau kwetu watawaliwa?
- Anatekeleza maelekezo ya bosi wake? au,
- Bosi bado anamtafuta wa kuchukua nafasi yake?
Hii trend ya kufumbia macho udhalimu tunaofanyiwa watanganyika inasikitisha sana, na inaleta hasira sasa, hivi tunachukuliwaje?
Mbona sasa tumegeuzwa kama kuku tunaokimbizwa na wafugaji kila wakitaka kumkamata wa kuchinja ili wanywe supu?
Kwa Bashe na upigaji wa sukari yalitokea tukayatazama, leo ni kama yameshapita. Hata hili la kutoa roho zetu nalo litaachwa lipite hivi hivi?
Kuagiza uchunguzi ufanyike sawa, lakini kiuhalisia wewe bosi kwa nafasi yako unachukua hatua gani nyingine kwa vitendo kutuonesha ulivyoguswa na mauaji ya asie na hatia?