Hapa Tanzania na nchi nyingi za kiafrika bunge na mahakama vipo kama mapambo tu na hutumika na wanasiasa wakitaka kufanya mambo yao. Inashangaza jinsi watanzania wengi wasivyojua haki zao na taratibu za kupata haki zao!
Kwanini watu wengi hufikiri kuwa waziri ana mamlaka ya kuamua haki kati ya pande mbili zinazozozana juu ya jambo flani? Ni kwasababu ya ujinga wa sheria.
Hovyo hizi hufanyika sana hapa nchini na hata kwenye chaguzi zetu ambapo wanasiasa ndio wanakuwa waamuzi wa nani ashinde nani ashindwe! Haya yanaweza kutokea kwenye nchi ambazo watu wake hawana weledi wa mambo na wajinga.
Waziri au mwanasiasa anaweza kusaidia mchakato wa kupata haki kupitia Mahakama ufanyike lakini sio kuingilia Mahakama au yeye mwenyewe kutoa haki kama hakimu. Hovyo hii inafanyika nchini kwetu na watu kwasababu hawajui taratibu, kanuni na sheria basi wanaona ni sawa kabisa, hapana!