Waziri Jaffo anataka kuwafukuza Wachina Kariakoo kwa kuuza bidhaa bei poa

China atawashinda tu,nashangaa siku zote wachina hiki,wachina kile mmeishajiuliza hivi vita ni vya nani kama si wahindi wanaomiliki Dar Central Business Hub.
Mhindi hana ujanja kwa Mchina,kibiashara,kitaluuma ndio hao wanajiita watanzania kumbe sio kweli na wameongezeka kila kukicha.
Je hao wachina wa Kariakoo hata 500 hawafiki angalia malaki ya wahindi wanafanya kwenye viwanda vya wahindi hawana work permit .
Waziri open your eyes.
 
Waziri Jaffo amecharuka. Anasema Serikali italivalia njuga tatizo la Wachina na wageni wote wanaofanya biashara nchini bila kibali.

Kuanzia kesho,yaani kuanzia leo,anataka kuona njagu wanawachangamkia Wachina Kariakoo.

Waziri Jaffo anasema yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara hatakubali nchi hii ichezewe na wageni.
Kwa hiyo Waziri Jaffo anatangaza trade war with China.

People are being too clever for themselves with these trade wars.

Watu wanakuwa wajanja kupita kiasi.

Pia soma > DOKEZO - Kufurika kwa Wachina Tanzania ni fursa au janga?
Kwanini na wabongo wasiuze bei za chini? ni kukosa akili tu
 
Waziri Jaffo amecharuka. Anasema Serikali italivalia njuga tatizo la Wachina na wageni wote wanaofanya biashara nchini bila kibali.

Kuanzia kesho,yaani kuanzia leo,anataka kuona njagu wanawachangamkia Wachina Kariakoo.

Waziri Jaffo anasema yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara hatakubali nchi hii ichezewe na wageni.
Kwa hiyo Waziri Jaffo anatangaza trade war with China.

People are being too clever for themselves with these trade wars.

Watu wanakuwa wajanja kupita kiasi.

Pia soma > DOKEZO - Kufurika kwa Wachina Tanzania ni fursa au janga?
Kuelekea uchaguzi mkuu...........
 
Hakuna haja ya kufukuza mchina kwa fujo.

1. Ita wafanyabiashara wa ndani,

2. Jadili nao namna sahihi ya kupunguza bei ya bidhaa iwe chini.

3. Ongeza kiwango cha mtaji cha wafanyabiashara wachuuzi kutoka nje kuchuuza nchini.

Kwa ufupi tengeneza mazingira mazuri kwa raia wako kupata bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani kwa bei nzuri isiyoumiza na wafanyabiashara wakapata faida.
 
Waziri Jaffo amecharuka. Anasema Serikali italivalia njuga tatizo la Wachina na wageni wote wanaofanya biashara nchini bila kibali.

Kuanzia kesho,yaani kuanzia leo,anataka kuona njagu wanawachangamkia Wachina Kariakoo.

Waziri Jaffo anasema yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara hatakubali nchi hii ichezewe na wageni.
Kwa hiyo Waziri Jaffo anatangaza trade war with China.

People are being too clever for themselves with these trade wars.

Watu wanakuwa wajanja kupita kiasi.

Pia soma > DOKEZO - Kufurika kwa Wachina Tanzania ni fursa au janga?
Trump Tariff effect
 
Punguza utoto, sio kila kitu Cha kukirupukia na kufanya siasa za majitaka. Serikali ipo kwenye hatua ya kutatua tatizo kubwa la baadaye lakini unaleta utoto
Hamna lolote labda kama wewe ni kilaza ndio utasapoti ukilaza wa Jaffo!!, Kwamba wachina ndio wanasababisha ukosefu wa ajira kwa vijana?. Hizi ni ishara za Nchi kutokuwa na viongozi wenye akili ya kutatua changamoto za jamii ila wanatafuta pahali pakujifichia ..... Jambo ambalo sio utatuzi wa tatizo.
 
Analeta siasa kwenye uchumi!
Hana uwezo wa kufanya hivyo anaongea tu ili massa yaende
Mambo ya uchaguzi kaka, kila mtu anajipakulia na "nitoke vipi" ss hv mambo ya kidiplomasia anaibuka nayo tu kwa kuropoka kisa wamachinga wanasikiliza!
 
Heading inasema “anataka kuwafukuza wachona kariakoo” halaf post yako “wachina na wageni wote wanaofanya biashara bila vibali”

Kwanza kabisa ,TIC iko wazi, mgeni anataka kuwekeza lazima aje na kiasi fulani cha pesa, si kufanya biashara za uchuuzi, kitendo cha mchina au mgeni yoyote kuingia nchini kama muwekezaji halaf akaja kuvamia biashara za chini ambazo ziko nje ya mipaka yake ni kinyume na sheria.

Hamna trade war hapo, kama kwao wanalinda biashara za wazawa na wako ruthless usipofuata sheria, why tz ikifanya hivyo ni dhambi?

Is not about bei rahis, but rule of law na protection ya wafanya biashara wa ndani
Nani alikwambia hao wachina wachuuzi wa kariako walikuja kama wawekezaji?, Nani aliwapokea na kuwaruhusu kufanya uchuuzi happy kariako!.
 
Punguza utoto, sio kila kitu Cha kukirupukia na kufanya siasa za majitaka. Serikali ipo kwenye hatua ya kutatua tatizo kubwa la baadaye lakini unaleta utoto
Sasa unatatua tatizo kwa tatizo ulilitengeneza? Nani anatoa vibali vya wachina kuingia nchini? Acheni kutufanya wajinga
 
Waziri Jaffo amecharuka. Anasema Serikali italivalia njuga tatizo la Wachina na wageni wote wanaofanya biashara nchini bila kibali.

Kuanzia kesho,yaani kuanzia leo,anataka kuona njagu wanawachangamkia Wachina Kariakoo.

Waziri Jaffo anasema yeye kama Waziri wa Viwanda na Biashara hatakubali nchi hii ichezewe na wageni.
Kwa hiyo Waziri Jaffo anatangaza trade war with China.

People are being too clever for themselves with these trade wars.

Watu wanakuwa wajanja kupita kiasi.

Pia soma > DOKEZO - Kufurika kwa Wachina Tanzania ni fursa au janga?
Mimi kwa upande wangu kwa kiasi flan nakubaliana nae lakin kwa kiasi kikubwa sikubaliane nae, mimi nikiwa na mdau mkubwa kkoo nafanya biashara lakin pia nina majengo yemye frem, kwa utafiti wangu mdogo, hii vita wameianzisha wahindi na baadhi ya waarabu wenye hela zao, sasa wanawatanguliza watu weusi na sababu iko wazi hizi jamii zilikuwa ndio zinacontrol kila kitu kuhusu biashara au uchumi sasa wananusa harafu ya kuingiliwa kitumbua chao na kudhibitiwa na wachina soon, so mimi ningeshaur kwa serikali yetu, wafanye kama walivyofanya Dubai, mgeni akitaka kufungua biashara hapa kwetu lazima awe shea na mwenyeji ili kwanza tupate uzoefu, pili na mtaji baadae. Lakin kwanini hii kampein inawalenga wachina tu tuna wahindi wengi sana na waturuki, waarabu hasa wa Lebanon na wa Egypt na wayemen wanafanyabiashara hapa bila vibali vyovyote. Kuna wakenya, waganda, Burundi, Malawi,wanyarwanda nk nk. Wote wanafanyabiashara kwanini wachina tu. Wamesahau watanzania kwa asili ni wavivu wa kufikir. So akija mgeni kuna watu wanajifunza kwa kuona na wengine kwa kutenda so mi nafikri wagen wawekewe kodi kubwa zaid ili tuifanye dar yetu ni hub ya kibiashara hapa east afrika. Watanzania changamkien fursa serikali inataka kodi hata akiondoka mchina watakuja wengine hatuwez miaka 70 tukaishi maisha ya kulalamika tu. Kaa na mchina Ingia nae makubalianao akushushie mzigo na wewe ujiongeze. Tusipofanya hivyo hakuna wa kumlaumu. Niishie hapo kwa leo.
 
Nani alikwambia hao wachina wachuuzi wa kariako walikuja kama wawekezaji?, Nani aliwapokea na kuwaruhusu kufanya uchuuzi happy kariako!.
Actualy is why nimesema kuna cheating, sheria za TIC zipo wazi, kuna biashara wawekezaj kutoka nje (raia wa nje) hawaruhusiwi kufanya.

Hamna aliewaruuhusu wachina kuwa wachuuzi, ile ni cheating. Is why gov inachukua hatua.

Iko hivi , sheria ya uwekezaji ya mwaka2022 (Tanzania Investment Act, 2022): Sheria hii inalenga kuvutia uwekezaji mkubwa nchini. Inatoa vivutio na kinga kwa wawekezaji wa kigeni wenye mitaji kuanzia Dola za Kimarekani 500,000.
Mantiki ya sheria hii ni kwamba uwekezaji wa kigeni unapaswa kuwa katika miradi mikubwa inayoleta teknolojia, mitaji mikubwa na fursa za ajira, badala ya kujihusisha na biashara ndogondogo za kila siku ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania. Ikiwa mwekezaji wa kigeni anakuja nchini kwa ajili ya "uwekezaji" lakini anajihusisha na biashara za rejareja Kariakoo, anaweza kuwa anakiuka madhumuni na matakwa ya sheria hii ya uwekezaji.

Lakini pia sheria ya utaratibu wa ajira za wataalamu wa kigeni (Non-Citizen Employment Regulation Act, Cap 436): Sheria hii inasimamia ajira za raia wa kigeni nchini Tanzania. Wageni wanaofanya biashara nchini wanatakiwa kuwa na vibali vya kazi na vibali vya ukaazi vinavyoendana na aina ya shughuli wanazofanya. Ikiwa raia wa kigeni anafanya biashara ya rejareja Kariakoo bila kibali sahihi cha kumruhusu kufanya shughuli hiyo, anakuwa anavunja sheria hii. Kuna uwezekano kuwa vibali vya kazi na ukaazi walivyopata havikuwa kwa ajili ya biashara ndogondogo au rejareja.
 
Anawafurahisha wajinga wa hili Taifa
Hivi unajua hata ukoloni ulivyokuja wazungu walikuja kama marafiki na zawadi tofauti tofauti kwa mababu zetu? ni kweli sio haki kama unauziwa shati la 5k kwa 20k, ila serikali hapo ndo inapopaswa kuingilia kati udhibiti wa bei kama kweli hali ipo hivo. Mbona kwenye kuagiza magari TRA wanakadiria kodi kulingana na thamani ya gari sokoni na sio invoice yako uliyolipia? So inawezekana serikali kujua bei hali za bidhaa na kudhibiti inapohitajika ila sio kuwaacha wageni kushikilia uchumi wetu.

Unapaswa kuelewa kuwa kama taifa tutakuwa katika hatari kubwa sana ya kiuchumi kama tutaruhusu wageni kushikilia biashara hasa soko kuu la kariakoo.

Unadhani wachina ndo wamejua leo tofauti ya bei za bidhaa huko kwao na kwetu? wanafanya hivi makusudi ili kuwaondoa sokoni wafanya biashara wazawa, ili wao ndo washikilie soko. Tukiruhusu ifikie hapo tumekwisha!!!
 
Actualy is why nimesema kuna cheating, sheria za TIC zipo wazi, kuna biashara wawekezaj kutoka nje (raia wa nje) hawaruhusiwi kufanya.

Hamna aliewaruuhusu wachina kuwa wachuuzi, ile ni cheating. Is why gov inachukua hatua.

Iko hivi , sheria ya uwekezaji ya mwaka2022 (Tanzania Investment Act, 2022): Sheria hii inalenga kuvutia uwekezaji mkubwa nchini. Inatoa vivutio na kinga kwa wawekezaji wa kigeni wenye mitaji kuanzia Dola za Kimarekani 500,000.
Mantiki ya sheria hii ni kwamba uwekezaji wa kigeni unapaswa kuwa katika miradi mikubwa inayoleta teknolojia, mitaji mikubwa na fursa za ajira, badala ya kujihusisha na biashara ndogondogo za kila siku ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania. Ikiwa mwekezaji wa kigeni anakuja nchini kwa ajili ya "uwekezaji" lakini anajihusisha na biashara za rejareja Kariakoo, anaweza kuwa anakiuka madhumuni na matakwa ya sheria hii ya uwekezaji.

Lakini pia sheria ya utaratibu wa ajira za wataalamu wa kigeni (Non-Citizen Employment Regulation Act, Cap 436): Sheria hii inasimamia ajira za raia wa kigeni nchini Tanzania. Wageni wanaofanya biashara nchini wanatakiwa kuwa na vibali vya kazi na vibali vya ukaazi vinavyoendana na aina ya shughuli wanazofanya. Ikiwa raia wa kigeni anafanya biashara ya rejareja Kariakoo bila kibali sahihi cha kumruhusu kufanya shughuli hiyo, anakuwa anavunja sheria hii. Kuna uwezekano kuwa vibali vya kazi na ukaazi walivyopata havikuwa kwa ajili ya biashara ndogondogo au rejareja.
Nani anapaswa kuwajibika kwq haya!, Hayupo?, Amechukuliwa hatua gani?, Amepewa rushwa kuidhinisha vibali fake kwa watu wasio na vigezo!!. Tunapotaka kutatua changamoto lazima tunaangalia kiini cha changamoto husika!. Kuwafukuza tu inaotsha? Kama waliohusika na kutoa vibali wapo kazini wataacha kutoa?.
 
Kama ulisikiliza hotuba ya kwanza ya mhe jaffo kwenye hili suala , kuna viongoz husika ambao walikula rushwa , na wengin wakawa wanampigia kumtaka aachane na hilo jambo.

Yes kuwatoa tu haitokuwa permanent solution, lazima wa clean na wale walio waruhusu

Maybe after last report tutaona
 
Back
Top Bottom