Waziri Jaffo anataka kuwafukuza Wachina Kariakoo kwa kuuza bidhaa bei poa

Waziri Jaffo anataka kuwafukuza Wachina Kariakoo kwa kuuza bidhaa bei poa

Kama ulisikiliza hotuba ya kwanza ya mhe jaffo kwenye hili suala , kuna viongoz husika ambao walikula rushwa , na wengin wakawa wanampigia kumtaka aachane na hilo jambo.

Yes kuwatoa tu haitokuwa permanent solution, lazima wa clean na wale walio waruhusu

Maybe after last report tutaona
Mkuu hizi ni nyakati za uchaguzi kinachofanyika ni siasa, hakuna kitu kitafanyika wameshajua wadanganyika wanadanganyika kijinga!.
Huyu sindio alikuja na hoja ya kiwanda KILA kona ya Nchi 😂 kwamba hata ukiwa na cherehani moja wewe una kiwanda tiari!!🙌🙌 Business as usual.
 
China atawashinda tu,nashangaa siku zote wachina hiki,wachina kile mmeishajiuliza hivi vita ni vya nani kama si wahindi wanaomiliki Dar Central Business Hub.
Mhindi hana ujanja kwa Mchina,kibiashara,kitaluuma ndio hao wanajiita watanzania kumbe sio kweli na wameongezeka kila kukicha.
Je hao wachina wa Kariakoo hata 500 hawafiki angalia malaki ya wahindi wanafanya kwenye viwanda vya wahindi hawana work permit .
Waziri open your eyes.
Sasa unashauri nini hapo? tubadilishe sheria na tuondoe vibali vya kazi kwa kuwa wachina ni kidogo kuliko wahindi wasio na kibali? au tulifumbie macho japo lipo kinyume na kisheria?

Mi nadhani ni kweli tuna wimbi la wageni wasio na sifa za kufanya kazi na biashara hapa kwetu, labda hapo mwanzo tulikuwa vipofu na wahindi walikula na sisi bila kutushika mkono, sasa mchina ametushika mkono tufanyeje? ... regardless ya nani katushika mkono tunapaswa sasa tuwe tumeamka na kusimamia haki zetu.

Inawezakana pia kuna mtu wa tatu na wanne pia walikuwa wanakula kwenye sahani yetu lakini hawakutushika mkono ... tunachopaswa ni kuondoa wote wasio na sifa, regardless ni mchina, mhindi ama yeyote mwengine.
 
Mkuu upo sahihi kabisa.Kila siku utasikia viwanda vinajengwa na vinatoa ajira.LAKINI ajira ni kwa hao wahindi wahamiaji haramu kutoka Pakistan, India,Bangladesh na Srililanka. Hawa si wawekezaji wanatafutia watu wao ajira.
Leo nimeona kituko kingine eti mhindi kafungua hotel wafanyakazi ni wanawake lakini wahindi tu kwenye picha.
Kweli viwanda vimejengwa vingi lakini ajira ni za hao hao akina Patel na Vinod
 
Sasa unashauri nini hapo? tubadilishe sheria na tuondoe vibali vya kazi kwa kuwa wachina ni kidogo kuliko wahindi wasio na kibali? au tulifumbie macho japo lipo kinyume na kisheria?

Mi nadhani ni kweli tuna wimbi la wageni wasio na sifa za kufanya kazi na biashara hapa kwetu, labda hapo mwanzo tulikuwa vipofu na wahindi walikula na sisi bila kutushika mkono, sasa mchina ametushika mkono tufanyeje? ... regardless ya nani katushika mkono tunapaswa sasa tuwe tumeamka na kusimamia haki zetu.

Inawezakana pia kuna mtu wa tatu na wanne pia walikuwa wanakula kwenye sahani yetu lakini hawakutushika mkono ... tunachopaswa ni kuondoa wote wasio na sifa, regardless ni mchina, mhindi ama yeyote mwengine.
Wanaijeria 🙌
 
Waruhusiwe wajenge china town ili wafanye biashara zao kwa style yao.

Wafuate sheria za nchi, walipe kodi ila wawe na eneo lao kama Kariakoo ila wapewe mji wao tuone wateja wataenda wapi?

Kama wateja wataenda kariakoo basi tutakuwa tumetatua tatizo.
 
wachina sio wajinga wale, pia sijui kama unajua mashariti ya mikopo tunayo pewa kutoka huko china
Niliwahi kuwauliza watu wanahisi kwamba serikali inaweza kuamua tu kuamka na kufukuza wachina..Watu wanaingia mikataba ya Mikopo yenye masharti ya Ushirikiano wa masoko na masoko ya china na nchi za Africa. Watu wanakuja na hoja za Uchumi wa kwenye vitabu tu 😃😃😃 Wachina wamefika kuishi.
 
Mimi kwa upande wangu kwa kiasi flan nakubaliana nae lakin kwa kiasi kikubwa sikubaliane nae, mimi nikiwa na mdau mkubwa kkoo nafanya biashara lakin pia nina majengo yemye frem, kwa utafiti wangu mdogo, hii vita wameianzisha wahindi na baadhi ya waarabu wenye hela zao, sasa wanawatanguliza watu weusi na sababu iko wazi hizi jamii zilikuwa ndio zinacontrol kila kitu kuhusu biashara au uchumi sasa wananusa harafu ya kuingiliwa kitumbua chao na kudhibitiwa na wachina soon, so mimi ningeshaur kwa serikali yetu, wafanye kama walivyofanya Dubai, mgeni akitaka kufungua biashara hapa kwetu lazima awe shea na mwenyeji ili kwanza tupate uzoefu, pili na mtaji baadae. Lakin kwanini hii kampein inawalenga wachina tu tuna wahindi wengi sana na waturuki, waarabu hasa wa Lebanon na wa Egypt na wayemen wanafanyabiashara hapa bila vibali vyovyote. Kuna wakenya, waganda, Burundi, Malawi,wanyarwanda nk nk. Wote wanafanyabiashara kwanini wachina tu. Wamesahau watanzania kwa asili ni wavivu wa kufikir. So akija mgeni kuna watu wanajifunza kwa kuona na wengine kwa kutenda so mi nafikri wagen wawekewe kodi kubwa zaid ili tuifanye dar yetu ni hub ya kibiashara hapa east afrika. Watanzania changamkien fursa serikali inataka kodi hata akiondoka mchina watakuja wengine hatuwez miaka 70 tukaishi maisha ya kulalamika tu. Kaa na mchina Ingia nae makubalianao akushushie mzigo na wewe ujiongeze. Tusipofanya hivyo hakuna wa kumlaumu. Niishie hapo kwa leo.
WEWE PEKEYAKO NDIYO UMEONA UKWELI ...YANI TUNAUMIA NA MCHINA AMBAYE VITU VYOTE TUNAVYO TUMIA VINATOKA KWAO ...UNAFIKI... ...WAHINDI NA WAARABU NDIYO WAPO NYUMA YA HIVI VITA WAKUWATUMIA MISUKURE YAO YA KIBANTU ... ILA MCHINA ATAWASHINDA KIVYOVYOTE ...wawekezaji wakubwa ndiyo wabaya wanaoingia mikataba ya mabilioni kifisadi na wapumbavu wa sisiemu
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt selemani Jafo amefanya ziara ya ghafla katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam na Kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi unafanywa na wageni kwa kushirikiana na wazawa.
 
View attachment 3326626
Aende na kule lugoba kwenye wanako pasua kokoto, na lisiishie baada ya uchaguzi
 
Tumepewa Fursa na Waziri wa Vianda Dr. Suleiman Jafo Kukusanya Taarifa kwa Haraka Oparation Kubwa inaendelea. Naomba hii Fomu Ijazwe kwa Haraka ukishindwa nitumie Details Inbox

Msemaji JWK
 
Sasa, hapa Jaffo haoni yeye ndiyo amefeli? Hao wanaomuangusha anawafanya nini? Siku zote hizo waziri ulikuwa wapi? Usalama wa taifa unafanya nini? Mbona baadhi ya wazawa wamelisema hili kitambo ulifanya nini?

Leo ndiyo unatuonesha unachapa kazi. Si utani huu?
 
Back
Top Bottom