Waziri Jaffo anataka kuwafukuza Wachina Kariakoo kwa kuuza bidhaa bei poa

Mkuu hizi ni nyakati za uchaguzi kinachofanyika ni siasa, hakuna kitu kitafanyika wameshajua wadanganyika wanadanganyika kijinga!.
Huyu sindio alikuja na hoja ya kiwanda KILA kona ya Nchi 😂 kwamba hata ukiwa na cherehani moja wewe una kiwanda tiari!!🙌🙌 Business as usual.
 
Nguvu y soda
KAZI ni kipimo cha utu
 
Sasa unashauri nini hapo? tubadilishe sheria na tuondoe vibali vya kazi kwa kuwa wachina ni kidogo kuliko wahindi wasio na kibali? au tulifumbie macho japo lipo kinyume na kisheria?

Mi nadhani ni kweli tuna wimbi la wageni wasio na sifa za kufanya kazi na biashara hapa kwetu, labda hapo mwanzo tulikuwa vipofu na wahindi walikula na sisi bila kutushika mkono, sasa mchina ametushika mkono tufanyeje? ... regardless ya nani katushika mkono tunapaswa sasa tuwe tumeamka na kusimamia haki zetu.

Inawezakana pia kuna mtu wa tatu na wanne pia walikuwa wanakula kwenye sahani yetu lakini hawakutushika mkono ... tunachopaswa ni kuondoa wote wasio na sifa, regardless ni mchina, mhindi ama yeyote mwengine.
 
Mkuu upo sahihi kabisa.Kila siku utasikia viwanda vinajengwa na vinatoa ajira.LAKINI ajira ni kwa hao wahindi wahamiaji haramu kutoka Pakistan, India,Bangladesh na Srililanka. Hawa si wawekezaji wanatafutia watu wao ajira.
Leo nimeona kituko kingine eti mhindi kafungua hotel wafanyakazi ni wanawake lakini wahindi tu kwenye picha.
Kweli viwanda vimejengwa vingi lakini ajira ni za hao hao akina Patel na Vinod
 
Wanaijeria 🙌
 
Waruhusiwe wajenge china town ili wafanye biashara zao kwa style yao.

Wafuate sheria za nchi, walipe kodi ila wawe na eneo lao kama Kariakoo ila wapewe mji wao tuone wateja wataenda wapi?

Kama wateja wataenda kariakoo basi tutakuwa tumetatua tatizo.
 
wachina sio wajinga wale, pia sijui kama unajua mashariti ya mikopo tunayo pewa kutoka huko china
Niliwahi kuwauliza watu wanahisi kwamba serikali inaweza kuamua tu kuamka na kufukuza wachina..Watu wanaingia mikataba ya Mikopo yenye masharti ya Ushirikiano wa masoko na masoko ya china na nchi za Africa. Watu wanakuja na hoja za Uchumi wa kwenye vitabu tu 😃😃😃 Wachina wamefika kuishi.
 
WEWE PEKEYAKO NDIYO UMEONA UKWELI ...YANI TUNAUMIA NA MCHINA AMBAYE VITU VYOTE TUNAVYO TUMIA VINATOKA KWAO ...UNAFIKI... ...WAHINDI NA WAARABU NDIYO WAPO NYUMA YA HIVI VITA WAKUWATUMIA MISUKURE YAO YA KIBANTU ... ILA MCHINA ATAWASHINDA KIVYOVYOTE ...wawekezaji wakubwa ndiyo wabaya wanaoingia mikataba ya mabilioni kifisadi na wapumbavu wa sisiemu
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt selemani Jafo amefanya ziara ya ghafla katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam na Kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi unafanywa na wageni kwa kushirikiana na wazawa.
Your browser is not able to display this video.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt selemani Jafo amefanya ziara ya ghafla katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Dar es Salaam na Kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi unafanywa na wageni kwa kushirikiana na wazawa.
View attachment 3326626
Aende na kule lugoba kwenye wanako pasua kokoto, na lisiishie baada ya uchaguzi
 


Tumepewa Fursa na Waziri wa Vianda Dr. Suleiman Jafo Kukusanya Taarifa kwa Haraka Oparation Kubwa inaendelea. Naomba hii Fomu Ijazwe kwa Haraka ukishindwa nitumie Details Inbox

Msemaji JWK
 
Sasa, hapa Jaffo haoni yeye ndiyo amefeli? Hao wanaomuangusha anawafanya nini? Siku zote hizo waziri ulikuwa wapi? Usalama wa taifa unafanya nini? Mbona baadhi ya wazawa wamelisema hili kitambo ulifanya nini?

Leo ndiyo unatuonesha unachapa kazi. Si utani huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…