Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Waziri Jafo amsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari.

IMG-20210113-WA0053.jpg



Tarime.JPG

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmasharauri ya Wilaya ya Tarime, Jumanne Yassin ili kupisha uchunguzi

Yassini anatuhumiwa kusafirisha mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Emmanuel Joseph Sizo juu ya Carrier ya gari, kama ambavyo baadhi ya picha za mtandaoni zilizosambaa zilionesha

Emmanuel alifariki Januari 10 kwa ajali ya gari Mkoani Singida, taarifa imesema kitendo cha kusafirisha maiti kwa utaratibu huo ni kinyume na kanuni Q.7(1) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma.

Pia soma >
Mkurugenzi wa Tarime mjini apata ajali Manyoni Singida
 
Yamesha tendeka. Marehemu kisha zikwa.Kwa nini kuendeleza maumivu kwa walio hai? Barua ya onyo ingetosha. Kama fedha zingelikuwa nje nje ka zamani sidhani kama huu uzembe ungelitokea.

Angelifanya zaidi ya hapo, angeambiwa;"Kapiga dili"na kazi hana. Kitumbua cha leo, mtu hula kinachoonekana mbele yake. Hajali ni cha moto au ni kibichi, tumbo litaamua.

Hapo tumbo limehamua kumharisha mtu. Nidhamu za woga
 
Jafo yuko vizuri, ila wengine walisema habari za mitandaoni zina maswali na majibu hukohuko sasa wakianza kufanyia kazi taarifa za mitandaoni itakuwa sio vyema sana!!. Ila heshima ya mtu aliyekufa HAIPO....ni sawa na mzoga..sema desturi zetu ndio tatizo yaani
 
Back
Top Bottom