Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

Mkuu kuna kitu ujakijua hapo,huyo ni mtumishi wa halmashauri hivyo usikute safari inaanzia mara mzigo unapelekwa mtwara au ruvuma hiyo.

Ukitia kwenye kirikuu si mtafika mzigo umepukutika wote kwenye sanduku.
Mwili si umepigwa dawa lakini!

Sema hapo inawezekana gari ilikuwa haitoshi labda ndomana wakamuweka juu!

Ova
 
Very bad!

Mitandao pia inasaidia kukemea yanayoendelea huko Chato na hivi karibuni mnaweza kuona serikali ikitoa tamko rasimi kujibu tuhuma zilizoko mitandaoni kuhusiana na miradi ya Chato.
Kama ambavyo watanzania masikini wanafanyiwa na serikali ya ccm kupitia BODI YA MIKOPO kuongeza deni pasipo haki kabisa na kupandisha makato.

Ila Mungu anajua tu
 
Kwani shida iko wapi?mbona kwenye ndege wanaweka kwenye buti na spare tyre .
Huo ni mzigo kama mizigo mingine mbona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ni utaratibu wa kawaida sana tu ila jumba bovu limemwangukia Yasini watumishi wengi kwenye Hamashauri nyingi ikiwemo Urambo na Kaliua wanasafirishwa hivyo kutoa nafasi kwa wasindikizaji hasa familia, gari inatolewa moja watu zaidi ya saba wanakwendaje?
 
Kaimu Mkurugenzi kaonewa. Yeye alitoa usafiri kama taratibu za Utumishi zinavyotaka, hakuelekeza marehemu abebwe juu ya carrier.

Inawezekana watumishi wenzake ndo waliosababisha. Walitaka wakae ndani ya gari ili wamsindikize marehemu kwao.

Hao waliobeba mwili na kuuoandisha huko ndo watuambie nani aliwaamuru na kwanini.

Muhimu tujifunze tu, maisha yana thamani ukiwa hai, ukifariki huwezi kuchagua treatment ya mwili wako. Tumtafute tu Mungu, huko mbeleni inawezekana hata ukifa wakapiga tu kiberiti mchezo ukaisha bila kufikishwa kwenu.
Unayo haki ya kuchagua upumzishwe vipi na wapi, ila tu uwe umejiandalia uwezo na nafasi ya kufanya hivyo (wosia/usia, fedha, ndugu, jamaa na marafiki with whom you share perception on Life and all that’s involved!)
 
Mkuu kuna kitu ujakijua hapo,huyo ni mtumishi wa halmashauri hivyo usikute safari inaanzia mara mzigo unapelekwa mtwara au ruvuma hiyo.

Ukitia kwenye kirikuu si mtafika mzigo umepukutika wote kwenye sanduku.
Huo ni utaratibu wa kawaida sana tu ila jumba bovu limemwangukia Yasini watumishi wengi kwenye Hamashauri nyingi ikiwemo Urambo na Kaliua wanasafirishwa hivyo kutoa nafasi kwa wasindikizaji hasa familia, gari inatolewa moja watu zaidi ya saba wanakwendaje?
 
Mwili si umepigwa dawa lakini!
Sema hapo inawezekana gari ilikuwa haitoshi labda ndomana wakamuweka juu !

Ova
Kiukweli hapo gari ilikuwa haitoshi kwa sababu hapo lazima watoke wasindikizaji kutoka halmashauri kwa maana kiongozi wa msafara kwa niaba ya mkurugenzi na ndugu au familia ya marehemu.

Ila mkuu haya mambo yanatofautiana kutokana na halmashauri moja na nyingine. Nilishashuhudia msiba wa mwalimu halmashauri fulani mkurugenzi alitoa pesa kukodi kosta nzima kubebea maiti pamoja na marehemu ambapo ukifanya mahesabu pembe za nchi hii haluna gharama ya kukodi kosta inazidi milioni moja na nusu.
 
Huo ni utaratibu wa kawaida sana tu ila jumba bovu limemwangukia Yasini watumishi wengi kwenye Hamashauri nyingi ikiwemo Urambo na Kaliua wanasafirishwa hivyo kutoa nafasi kwa wasindikizaji hasa familia, gari inatolewa moja watu zaidi ya saba wanakwendaje?
Mwili si umepigwa dawa lakini!
Sema hapo inawezekana gari ilikuwa haitoshi labda ndomana wakamuweka juu !

Ova
 
..unaweza kukuta gari ni moja, tena dogo.

..halafu wanatakiwa wasafirishe mwili, familia, na vyakula vya kupeleka kwenye msiba.

..sidhani kama mkurugenzi alikuwa na nia mbaya.

Vyakula na mizigo mingine kama mavazi and the likes , mahali sahihi ni hapo walipoweka casket yenye mwili wa marehemu.

Wengine wangepanda basi za bei nafuu ili mradi kumsitiri mpaka mwisho marehemu na mwili wake.
 
Hiyo nauli ni kuongeza gharama kwa wafiwa.

Hata mimi ningependa wawe na gari maalum la kubeba mwili, na familia na waombolezaji wakodishiwe coaster.

Lakini huwezi kujua hali ya kifedha ya waliokutwa na msiba.

Sidhani kama kuna mtu anaweza kudharau msiba wa mwenzake.
 
Huo ni utaratibu wa kawaida sana tu ila jumba bovu limemwangukia Yasini watumishi wengi kwenye Hamashauri nyingi ikiwemo Urambo na Kaliua wanasafirishwa hivyo kutoa nafasi kwa wasindikizaji hasa familia, gari inatolewa moja watu zaidi ya saba wanakwendaje?
Hata Kama inaonekana ni utaratibu uliozoeleka huko kwenye halmashauri lakini ni kinyume na kanuni za utumishi. Ni bahati mbaya tu hayo mazoea yameendelea kwa sababu watu hawajui taratibu, hivyo wakurugenzi wamekuwa wakitake advantage kwa ignorance ya watu.

Hata Kama hakuna magari haiwezekani halmashauri ishindwe kukodi coaster itakayo accommodate mwili pamoja na wasindikizaji. Mtu amefariki ni lazima mwili wake upewe heshima hasa mkikumbuka namna mlivyoweza kuishi nae alipokuwa hai.

Imagine familia ya marehemu inasubiri mwili kwa ajili ya mazishi then gari linakuja likiwa na mwili kwenye carrier, hao ndugu zake watajisikia machungu kiasi gani.
 
Kumbuka watu wanatumbuliwa kwa mambo kama haya umeongeza budget kwa idhini ya nani labda umekula cha juu wakurugenzi wana taabu sana awamu hii wa nyang'hwale leo mwaka wa tatu na DT wake
 
Bongo Kuna visa sana mpaka miaka kumi inaisha unaweza kutengeneza series za kutosha tu, ila nimeona maiti zikisafishwa hivyo mara nyingi sana nilikua nashangaa mpaka nimeacha kushangaa nishaona kawaida maana unakuta wanabana matumizi eti wanatoa gari moja na hiyo hiyo watumishi wapande.
 
Huo ni utaratibu wa kawaida sana tu ila jumba bovu limemwangukia Yasini watumishi wengi kwenye Hamashauri nyingi ikiwemo Urambo na Kaliua wanasafirishwa hivyo kutoa nafasi kwa wasimdikiazaji hasa familia gari inatolewa moja watu zaidi ya saba wanakwendaje?
Unaonaje watu wanne kati ya wale saba wakae juu kwenye carrier na maiti iwekwe ndani
 
Ila ingekua ni kwa mtu mwingine ambae hana cheo ingekua ni kitu ya kawaida tu sivyo?
 
Waziri Jafo amsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmasharauri ya Wilaya ya Tarime, Jumanne Yassin ili kupisha uchunguzi

Yassini anatuhumiwa kusafirisha mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Emmanuel Joseph Sizo juu ya Carrier ya gari, kama ambavyo baadhi ya picha za mtandaoni zilizosambaa zilionesha

Emmanuel alifariki Januari 10 kwa ajali ya gari Mkoani Singida, taarifa imesema kitendo cha kusafirisha maiti kwa utaratibu huo ni kinyume na kanuni Q.7(1) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma.

Pia soma > Mkurugenzi wa Tarime mjini apata ajali Manyoni Singida
Mh. Waziri amemstahi sana huyu mtu. Alikuwa na uhalali wa kumfukuza kabisa kazi hata kabla maiti hajijawasili kule ilikokuwa inapelekwa. Maiti ni kitu chenye heshima kubwa mno, na ndiyo maana huwa inapigiwa saluti na wanajeshi wa ngazi zote jeshini
 
Back
Top Bottom