Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Upande wa kuleta wananchi kwenye uzinduzi wa mradi wa serikali, ni upande wa siasa na vitengo vyao vya propaganda, na kamwe siyo kazi ya meneja!

Nashangazwa sana na hawa ccm! Juzi tu wamewapa wafungwa kazi za chama.

Hapa meneja naye anapewa kazi ya siasa na propaganda. Utadhani nchi ya kikomunisti!

Hii nchi bhana! Ndo maana tunabakia maskini pamoja na utajiri wa rasilimali tulionao! Vichwa vibovu kabisa!

Huwa wanaachiwa hivi kama alivyosema Maghufuli kuwaambia wakurugenzi kuwa inakuwaje awateuwe halafu ccm wasishinde uchaguzi.

Kuna hali mbaya huko tunakoelekea kama tunataka demokrasia ya kweli.
 
Upande wa kuleta wananchi ni wa siasa, siyo kazi ya meneja! Nashangazwa sana na hawa ccm! Juzi tu wamewapa wafungwa kazi za chama. Hapa meneja naye anapewa kazi ya siasa na propaganda. Utadhani nchi ya kikomunisti!

Hii nchi bhana! Ndo maana tunabakia maskini pamoja na utajiri was rasilimali! Vichwa vibovu kabisa! Huwa wanaachiwa hivi kama alivyosema Maghufuli kuwaambia wakurugenzi kuwa inakuwaje awateuwe halafu ccm wasishinde uchaguzi. Kuna hali mbaya huko tunakoelekea kama tunataka demokrasia ya kweli.
Mkuu, labda ilikuwa no tenda, Magereza wakaibuka washindi ktk tenda hiyo ya kupandisha bendera za CCM utajuaje?
 
Meneja ana wajibu wa kuhakikisha anamkumbusha MKURUGENZI AANDAE uwepo huo wa watu....

MKURUGENZI naye Ana MAKOSA kwa sababu yeye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za MAENDELEO....

Think thrice
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

View attachment 1502024
 
Mhe Waziri msamehe tuu; sisi wananchi na wapiga kura tuko kwenye mihangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku
 
Upande wa kuleta wananchi ni wa siasa, siyo kazi ya meneja! Nashangazwa sana na hawa ccm! Juzi tu wamewapa wafungwa kazi za chama. Hapa meneja naye anapewa kazi ya siasa na propaganda. Utadhani nchi ya kikomunisti!

Hii nchi bhana! Ndo maana tunabakia maskini pamoja na utajiri wa rasilimali tulionao! Vichwa vibovu kabisa! Huwa wanaachiwa hivi kama alivyosema Maghufuli kuwaambia wakurugenzi kuwa inakuwaje awateuwe halafu ccm wasishinde uchaguzi. Kuna hali mbaya huko tunakoelekea kama tunataka demokrasia ya kweli.
Alafu waziri mzima anamuuliza meneja wa mradi eti wewe ni mpinzani?
 
Jafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.
Sijui unamkubali kwa lipi mshamba huyu hivi kweli unamtoa mtu kazini kwasababu hakuna umati wa watu. Huyu ni meneja TARURA wala sio mwanasiasa, angepaswa kuwalaumu wana CCM mkoa, wilaya, etc. Da ndio maana nafanya biashara zangu naishi kwa uhuru na furaha kabisa kuliko utumwa wa kuajiriwa.
 
Wakati wafungwa wanapandisha za ccm, polisi wanashusha za chadema. Mtafanya hivyo hata wakati wa kampeni?
Kushusha bendera za Chama chochote haikubaliki, tena police wanaolinda Amani sio vizuri hata kidogo, lakini ni wapi na Kwa nini?
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA Jijini Arusha, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kushuhudia barabara zilizokamilika alizokuwa akizitembelea.

Waziri Jafo amesema, “Mnataka Serikali ionekane haijafanya kitu wakati Wananchi ndio barabara yao? Kama ni barabara ya Wananchi mbona Wananchi hawapo hapa? Au unataka Serikali ionekane haijafanya kitu katika maeneo yao?”

Waziri Jafo amemuhoji Meneja huyo ambaye pia ndio Mratibu wa barabara za Jijini humo “Kwanini hii tunazindua barabara hii Wananchi hawapo? Unataka Rais aonekane hajafanya kitu? Rais ameweka fedha hapa. Mmeficha halafu kesho na kesho kutwa mseme Rais hajafanya kitu?”

Aidha, Meneja huyo alipoanza kujitetea na kusema kuwa alidhani Mtendaji (Mkurugenzi) amefanyia kazi suala hilo, Waziri Jafo alimwambia “Wewe si barabara zako? Unafanya sabotage ili Rais aonekane hajafanya kitu halafu kesho Wananchi waseme hakuna lolote Rais amefanya?”

Waziri Jafo amemalizia “Ninyi ndio wataalamu mnaofanga Serikali ionekane haijafanya jambo wakati sisi hapa Arusha tumewekeza fedha nyingi. Mji wa Arusha tumetandaza Barabara ila wewe unaficha hata Wananchi hapa jirani wasijue tumeweka barabara”

View attachment 1502024
Kazi kuu ya meneja kaifanya

Uhamasishaji sio kazi ya Injinia

Halmashauri ingebeba jukumu
 
Back
Top Bottom