Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Upande wa kuleta wananchi kwenye uzinduzi wa mradi wa serikali, ni upande wa siasa na vitengo vyao vya propaganda, na kamwe siyo kazi ya meneja!

Nashangazwa sana na hawa ccm! Juzi tu wamewapa wafungwa kazi za chama.

Hapa meneja naye anapewa kazi ya siasa na propaganda. Utadhani nchi ya kikomunisti!

Hii nchi bhana! Ndo maana tunabakia maskini pamoja na utajiri wa rasilimali tulionao! Vichwa vibovu kabisa!

Huwa wanaachiwa hivi kama alivyosema Maghufuli kuwaambia wakurugenzi kuwa inakuwaje awateuwe halafu ccm wasishinde uchaguzi.

Kuna hali mbaya huko tunakoelekea kama tunataka demokrasia ya kweli.
 
Mkuu, labda ilikuwa no tenda, Magereza wakaibuka washindi ktk tenda hiyo ya kupandisha bendera za CCM utajuaje?
 
Meneja ana wajibu wa kuhakikisha anamkumbusha MKURUGENZI AANDAE uwepo huo wa watu....

MKURUGENZI naye Ana MAKOSA kwa sababu yeye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za MAENDELEO....

Think thrice
 
Mhe Waziri msamehe tuu; sisi wananchi na wapiga kura tuko kwenye mihangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku
 
Alafu waziri mzima anamuuliza meneja wa mradi eti wewe ni mpinzani?
 
Jafo namkubali ila sababu alizotoa kwa meneja wa TARURA ni za kijinga na kishamba kupindukia.
Sijui unamkubali kwa lipi mshamba huyu hivi kweli unamtoa mtu kazini kwasababu hakuna umati wa watu. Huyu ni meneja TARURA wala sio mwanasiasa, angepaswa kuwalaumu wana CCM mkoa, wilaya, etc. Da ndio maana nafanya biashara zangu naishi kwa uhuru na furaha kabisa kuliko utumwa wa kuajiriwa.
 
Wakati wafungwa wanapandisha za ccm, polisi wanashusha za chadema. Mtafanya hivyo hata wakati wa kampeni?
Kushusha bendera za Chama chochote haikubaliki, tena police wanaolinda Amani sio vizuri hata kidogo, lakini ni wapi na Kwa nini?
 
Kazi kuu ya meneja kaifanya

Uhamasishaji sio kazi ya Injinia

Halmashauri ingebeba jukumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…