Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

huyu aliwaziri kwani nani asitejua barabara zinajengwa na serikali,
nani asiyejua kuna barabara ipi ya lami
Alafu kwa arusha barabara ni jambo la kawaida mno labda uvcccm wangepewa buku 7 waende hapo kushangilia barabara iliyojengwa kwa kodi zao wenyewe.
 
Kwa nini yeye Jafo na yeye hakutangazia kwenye TBC kama anakwenda kufungua hiyo barabara? Alitakiwa aweke matangazo ya ratiba yake kwenye TBC na magzeti ya serikali ajionee mwenyewe.

Kama ilivyo kazi yake yeye ni uzinduzi na meneja huyo kazi yake ilikuwa ninkusimamia kiwango. Yeye sio Press Secretary wa jimbo au Wilaya. Kuna wapiga zumari munawachagua kwa kazi hiyo na kuwabandika jina la DAS. As the saying goes, "the harder they come the harder they go"
 
Mimi nadhani ni Sawa tu,

Maana yake halisi ni Sawa na Baba kujenga nyumba ya pili Halafu asiimbie familia yake kuwa amejenga nyumba nyingine mahali, Halafu akaweka wapangaji wasijue hata familia yake

Irrelevant.
 
Moja kati ya mawaziri nawakubali kwenye awamu hii ni Jafo, ila kwa hili la leo kaniangusha sana
Yuko sahihi na alichoongea kizito sana
Uzinduzi wa barabara wananchi wengi wanatakiwa kuhudhuria mfano mialiko ilitakiwa iende kwa wadau wa barabara mfano umoja wa wenye mabasi,magari ya mizigo , daladala,boboda,waananchi ambao hizo barabara zinapita ambao walifaidi ajira ,kuuzia vyakula vibarua ,wajenzi nk ,makondractor ,wafanyabiashara wa maeneo hayo barabara inapita wakiwemo wa vituo vua mafuta vilivyoko hayo maeneo walio supply mafuta na watakaofaidi uwepo nk ambao wengine walifaidika kwa kuuza vifaa mbalimbali kwenye mradi

Pia viongozi wa maeneo barabara inapita mfano wajumbe wa nyumba kumi,madiwani,wabunge ,viongozi wa serikali za mitaa,viongozi wa dini nk

Viongozi wa vyama na serikali na mashirika ya umma kama TRA ambako hukusanya kodi , taasisi za kijamii

Uzinduzi maana yake ni kukabidhi mradi kwa wananchi kuwa kodi zenu jamani hizo hapo na kazi mlitupa kwa kodi zenu hiyo.Sasa waziri hawezi kabidhi barabara kwa meneja wa Tarura anakabidhi kwa wananchi

Hilo tukio ni la TARURA lakini alitakiwa kushiriksha wadau mbalimbali .Ahakikishe wadau wakabidhiwa wapo
 
Haya uliyouaongea kwa chuga ni inapplicable. Labda sehemu nyingine ya Tz
 
Hii serikali ya kijinga sana hii......washamba na malibukeni wa madaraka
 
Hapo issue siyo kujaza watu kwenye barabara,walimtafutia tu sababu. Ukitaka kumwua mbwa mpe jina baya.
 
Kazi ya kukusanya wananchi sio kazi ya meneja. Meneja ni mtalaamu na mtendaji anayesimamia miradi ya maendeleo.

Ujio wa waziri unasimamiwa na viongozi wa kisiasa, vivyo kukusanya watu ilikuwa ni kazi ya DC/DED kuwataarifu makatibu tarafa na kata ambao nao iliwapasa kuwasiliana na watendaji wa vijiji na mitaa.

Nafikiri fagia fagia Arusha imechukua sura mpya
 
Hilo kosa ni la kumuondoa mtu kweli?Kwa taarifa yake watu kama yeye Jaffo ndio wanaosasabisha hii serikali ichukiwe kwa maamuzi kama haya
Jafo katika hili nimemdharau kabisa na amefanya uonevu wa wazi kabisa na hata alivyo kuwa anaongea anaonesha kabisa kama anakisa kingine na huyo meneja wa tarura ila akakosa pa kumshikia
 
Endeleeni tu kutetea kunyanyaswa kwa binadamu wenzenu ila jueni mwisho wenu u karibu.

Mnayoyafanya hata kwenye sera zenu na miongozo yenu hayapo. CCM mnasema binadamu wote ni sawa, sasa hapo jaffo alivyomuuliza huyo eti au wewe ni mpinzani ni sahihi???

Unajifanya unaandika utetezi kumbe umeandika ujinga mtupu. Nani kakwambia kuzinduliwa mradi ndo kuukabidhi kwa mwananchi??? Nani kakwambia mtumishi wa umma moja ya majukumu yake ni kufanya siasa??? Nani kakwambia mradi usipozinduliwa hautimiki??? Kwani iyo barabara hata kama mwananchi hayupo kwenye kuzinduliwa kwake haioni????

Nakwambia tena hizi ni dalili kuwa CCM mmefikia mwisho katika kuiongoza Tanzania. Hamuwezi mkafanya uonevu huu wa waziwazi na mkabaki salama.
 
Dah utawala wa Sheria umekufa kibudu
 
Kazi kweli kweli! Tanzania yetu sote kweli tumefikia hapo!
 
WanaCCM wanaodaiwa kutapakaa kila kona ya nchi huku kukiwepo ofisi za chama za CCM kila wilaya hadi ngazi za kata na viongozi wa mitaa walioshinda kwa kishindo Nov 14 2019 na makada wa UVCCM waliopachikwa uDAS, DED, RAS, DC, RC lakini wananchi wanaomuunga mheshimiwa hawaonekani lazima kuna muskheli katika propaganda na takwimu za Polepole kuhusu hali ya kisiasa Tanzania !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…