Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyama vya siasa ndivyo vimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa sio wagombea, na kwamba wagombea wa vyama vilivyojitoa waliokata rufaa, matokeo ya rufaa yakitoka na wakishinda, majina yao yatajumuishwa kwenye karatasi za uchaguzi..

Hoja:

Ivi mtu akienguliwa na chama huwa anabaki kuwa mwanachama? Na mtu akivuliwa uanachama na ni diwani au mbunge huwa anabaki na cheo chake? Hii sheria imetungwa lini?

Kwanini wanalazimisha ushiriki kwanini hawafurahi wapinzani kuwaachia waendelee kushinda bila lupingwa

Jafo anaonesha alivyo na ubongo mdogo mno!

Tanzania ghafla bin vuu leo kuna wagombea bonafsi!

Maajabu!

Nyani akifa miti yote huteleza ndio Jafo na bwana mawe!
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
Kwa hamtaki ushindi wa 100% tena?
Mbona mnawalazimisha wakati wao wamejitoa ili kuwapa nafasi mpate ushindi wa kishindo?
Yaani kweli chama cha watu wasiojulikana mnaumia kuliko Chadema waliojitoa?
Haya kweli ni maajabu....
 
MATOKEO YA RUFAA ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA NOVEMBA 10.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO akizungumza Jijini Dodoma amesema katika zoezi la kuchukua fomu kuna makosa mbalimbali yalifanyika katika kujaza fomu nyingi ikiwa ni pamoja na kaukosea majina ya eneo pamoja na udhamini. .
.
Akizungumza jijini Dodoma JAFO amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya katika sehemu mbalimbali amegundua uwepo wa makosa hayo ambapo amesema baadhi ya maeneo wagombea wameigana na kufanya makosa yanayofanana. .
.
Amesema katika zoezi la kuchukua fomu asilimia zaidi ya 98 wagombea wamerudisha fomu na rufaa zaidi ya 13,000 zimewasilishwa ambapo kesho ndio rufaa zitatolewa ili kujua ngapi zimekubaliwa na ngapi zimekataliwa kwa wagombea wote waliowasilisha mapingamizi bila kujali vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi na watakaoteuliwa majina yao watakuwepo siku ya uchaguzi.
Kapumbavu kumbe nako haka.. nilikua najua kanazo , wake 4 wamekachanganyA
 
Basi limesema haliendi.. unasema unaenda.. labda utumie basi jingine.. akili zako ni za kumenya vitunguu tuu.

Sheria ya uchaguzi ipo.wazi
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyama vya siasa ndivyo vimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa sio wagombea, na kwamba wagombea wa vyama vilivyojitoa waliokata rufaa, matokeo ya rufaa yakitoka na wakishinda, majina yao yatajumuishwa kwenye karatasi za uchaguzi..

Hoja:

Ivi mtu akienguliwa na chama huwa anabaki kuwa mwanachama? Na mtu akivuliwa uanachama na ni diwani au mbunge huwa anabaki na cheo chake? Hii sheria imetungwa lini?

Kwanini wanalazimisha ushiriki kwanini hawafurahi wapinzani kuwaachia waendelee kushinda bila lupingwa
Mtu ana wake wanne na watoto 20 anaachaje kuchanganyikiwa ?
 
Kudhamini ni issue binafsi Kama Chama kinajitoa udhamini kilitakiwa kiwaambie wagombea wake na wao ndio waseme tunajitoa sababu mdhamini wetu kajitoa tunaomba msimamizi Kama una fomu ya mdhamini kujitoa nipe nimpelekee akajaze alete kwa maandishi.

Fomu za kudhamini wagombea vyama vilijaza kujitoa pia vijaze fomu vipeleke kutengua fomu zao za mwanzo.othetwise huko.kujitoa kwenye press ni matangazo tu ya vijiweni ambayo sio official.Jafo Yuko sahihi wote waliopitishwa watapigiwa kura
Kwa ufupi wewe hujitambuzi unafikiri kama mtoto darasa la pili ndio hasara ya kukabidhi ubongo wako kwa mtu mwingine akushikie.
 
Kuna watu wakifa asubuhi jioni tayari wamesahaulika.
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyama vya siasa ndivyo vimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa sio wagombea, na kwamba wagombea wa vyama vilivyojitoa waliokata rufaa, matokeo ya rufaa yakitoka na wakishinda, majina yao yatajumuishwa kwenye karatasi za uchaguzi..

Hoja:

Ivi mtu akienguliwa na chama huwa anabaki kuwa mwanachama? Na mtu akivuliwa uanachama na ni diwani au mbunge huwa anabaki na cheo chake? Hii sheria imetungwa lini?

Kwanini wanalazimisha ushiriki kwanini hawafurahi wapinzani kuwaachia waendelee kushinda bila lupingwa
 
Baada ya maneno hayo, siyo tu nimemshangaa jafo lakini nimeona kuna haja ya kumpuuza.

Sijui kama ni ikosefu wa weledi, low IQ and poor reasoning au ni kuchanganyikiwa.
 
Hivi si kila alipopita katika ziara yake alisisiza wapinzani wakatwe tu au? Labda kama hakuwa yeye alisema hayo maneno, vinginevyo ametoa majibu tofauti kwa wasimamizi wa uchaguzi katika halmashauri alizopitia na sasa kwa waandishi wa habari anatoa majibu tofauti. Ni vema mhe. Akawa na hofu ya Mungu
 
HAWA WATU WANATUHARIBIA NCHI SANA AISEE.WATATULETEA MAPIGANO YA WENYEWE MWISHOWE
 
Mambo yakiwa magumu na hayaendani na unachoamini kama kiongozi unaomba kujiuzulu.

Hivi kweli leo Jafo ni wakusema chama kimejitoa na sio mgombea? Aibu gani hii?
 
Huku ni kuchanganyikiwa samahani mheshimiwa jafo kama uko humu.
 
Kinagombea chama bila mgombea??katiba inaruhusu mgombea binafsi???
Kwani kwenye chama kuna mgombea mmoja? Kama kaenguliwa na wengine wamepitishwa kwenye chama husika kwanini aliyepitishwa asigombee?walioamua kususia wenyewe wana nafasi zao top rank.huoni wamewanyima haki hawa waliopitishwa kugombea uenyekiti?mbona zile chaguzi za marudio za ubunge baada ya kuunga juhudi hawakujitoa?,hakukuwa na figisu?,upinzani wapumbafu sana.

Katiba hairuhusu mgombea binafsi,sijasema kama kuna mtu kagombea binafsi,ila anaweza kuenguliea binafsi kwasababu anagombea nafasi moja,(mtaa).chama kinagombea nafasi nyingi(mitaa),kwahiyo akienguliwa mmoja au kadhaa...wengine waendelee..
 
Basi waandike barua ya kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wahusika yaani hao wasimamizi wa uchaguzi au msajili wa vya siasa,wakiainisha mambo ambayo hawakuridhishwa nayo katika mchakato mzima wa uchaguzi,hapo huenda msajili akakaa nao meza moja kujua nini kifanyike,kumbuka baada ya kugomea uchaguzi wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria,lakini pia wanaweza kupata mwanga wa chaguzi zijazo zitakavyosimamiwa,wasitangaze tu kwenye vyombo vya habari kisha wakaa kimya.hali itakuwa mbaya sana mwakani,yule dada wanamwita mange kimambi aliwahi kusema kuna uwezekano kusiwe na mbunge hata mmoja wa upinzani bunge la awamu inayofuata.dalili zimeanza kuonekana mapema kwenye huu uchaguzi, tunaelekea kubaya sio siri.
Akili za mwewe eti waandike barua za kujitoa kwani walisema ni wagombea binafsi?sheria hiyo ipo Tanzania ccm si mliikataa?wewe mbona unahangaika sana?wakati kichwani ubongo haupo.
 
Back
Top Bottom