Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Akili za mwewe eti waandike barua za kujitoa kwani walisema ni wagombea binafsi?sheria hiyo ipo Tanzania ccm si mliikataa?wewe mbona unahangaika sana?wakati kichwani ubongo haupo.
Ubongo ukiwa kwenye kichwa chako inatosha...[emoji119][emoji119]
 
Jamani hivi kuna sheria zinazoruhusu wagombea binafsi katika nchi hii? Chama kinacho mdhamini mtu kinatangaza kujitoa kwenye uchaguzi nyie mnalazimisha mna faidika na nn? Kama ni hivyo ruhusuni wagombea binafsi.[QUOTE="YEHODAYA, post: 33419274, member: 315573"
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
[/QUOTE]
 
Akili za mwewe eti waandike barua za kujitoa kwani walisema ni wagombea binafsi?sheria hiyo ipo Tanzania ccm si mliikataa?wewe mbona unahangaika sana?wakati kichwani ubongo haupo.
Na kama hujaelewa nilimaanisha viongozi wa vyama vya upinzani vilivyogomea uchaguzi viandike barua rasmi kwa msajili wa vyama vya siasa ili dhamira yao iwe "official",tofauti na sasa ambapo wame press tu kwenye vyombo vya habari, sijasema hao wagombea uenyekiti ndio waandike barua.

Empty set kabisa wewe!!
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa mfano mbunge atakapovuliwa uanachama na chama chake inakuwa pia anapoteza nafasi yake ya ubunge kwenye jimbo husika. Hao wanacha waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali kwenye serikali za mitaa wamefanya hivyo kwa kutumia ridhaa aliyopewa na chama chake. Chama ndio chenye sauti ya mwisho juu ya mgombea anaye kiwakilisha chama husika.
 
Hivi waliosababisha makosa hata uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 ukafutwa wameshitakiwa au kuwajibishwa wapi?. Hasara ya sh ngapi ilipatikana?. Ni dosari zipi hasa zilitolea hata ukafutwa?. Why not huu???
 
MATOKEO YA RUFAA ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA NOVEMBA 10.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO akizungumza Jijini Dodoma amesema katika zoezi la kuchukua fomu kuna makosa mbalimbali yalifanyika katika kujaza fomu nyingi ikiwa ni pamoja na kaukosea majina ya eneo pamoja na udhamini. .
.
Akizungumza jijini Dodoma JAFO amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya katika sehemu mbalimbali amegundua uwepo wa makosa hayo ambapo amesema baadhi ya maeneo wagombea wameigana na kufanya makosa yanayofanana. .
.
Amesema katika zoezi la kuchukua fomu asilimia zaidi ya 98 wagombea wamerudisha fomu na rufaa zaidi ya 13,000 zimewasilishwa ambapo kesho ndio rufaa zitatolewa ili kujua ngapi zimekubaliwa na ngapi zimekataliwa kwa wagombea wote waliowasilisha mapingamizi bila kujali vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi na watakaoteuliwa majina yao watakuwepo siku ya uchaguzi.
Mheshimiwa Jafo amepitia fomu za ccm ambazo wagombea wamepita bila kupinhwa? Sina hakika kama fomu za wagombea wa ccm zimejazwa vizuri. Je, hawa wagombea wa vyama vya upinzani ndo mara ya kwanza wanajaza hizi fomu? Ukizipitia hizi fomu wagombea wa ccm ndo waliokosea ujazaji wa fomu katika maeneo mengi. Lakini Mh. Jafo anafahamu katika baadhi ya maeneo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi baada tu ya kupokea fomu za wagombea wa ccm waligunga ofisi ili wasipokee fomu kutoka kwa vyama vya upinzani? Je, Mh. Jafo anafahamu kuwa hata barua za pingamizi kutoka kwa wapinzani hazikupokelewa kutokana na wasimamizi wasaidizi kutoonekana ofisini siku ya kupokea pingamizi? Haya mambo yaliyofanyika yanatia aibu na hasira kwa watu wenye utu na kujali heshima ya taifa letu kimataifa. Upuuzi huu umeratibiwa na wakuu wa mikoa na wilaya kwa baadhi ya maeneo wakiwashinikiza wasaidizi wao na ndo hao hao tena wasikilize rufaa. Haya si maigizo tu? Shame to our Nation
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
Tumia kichwa kufikiri,sio ma.ta.ko.
 
Hivi tatizo liko wapi? Kama walishakatwa, sasa kwanini mnawalazimisha tena wagombee? Kuna nini, watu waache unafiki.
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Hebu weka hiko kipande kipo kwenye sheria au kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mie nimesoma kanuni tu ambayo inasema ukiwa mgombea unapaswa uwe umedhaminiwa na chama.....sasa chama kimeshasema hakitashiriki uchaguzi mgombea atadhaminiwa au atapeperusha bendera ya chama gani?
 
hati ya dharura

muswada unasukwa

kujitoa kosa la jinai

katibu wa chama na mgombea kuunganishwa

uhujumu wa mipango ya serikali

nataka niwaerezeni ukweri

rpc uwarinde wanaosema ukweri wa changamoto bira kuficha

na hiro bango rako ra reo kamuonyeshe mkeo

nikisema CCM OYEEE

mnaitika MAENDEREO HAYANA CHAMA
 
Anayejitoa ni mgombea sio mbowe. Pia hakuna document yoyote ya mgombea aliyoandika kuiarifu tume kuwa amejitoa hivyo wale wote waliorudisha form zikakubaliwa basi watapigiwa kura
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyama vya siasa ndivyo vimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa sio wagombea, na kwamba wagombea wa vyama vilivyojitoa waliokata rufaa, matokeo ya rufaa yakitoka na wakishinda, majina yao yatajumuishwa kwenye karatasi za uchaguzi..

Hoja:

Ivi mtu akienguliwa na chama huwa anabaki kuwa mwanachama? Na mtu akivuliwa uanachama na ni diwani au mbunge huwa anabaki na cheo chake? Hii sheria imetungwa lini?

Kwanini wanalazimisha ushiriki kwanini hawafurahi wapinzani kuwaachia waendelee kushinda bila lupingwa
Pumbavu kweli huyo Jafo..

Vikao haviishi nasikia yeye, bashiru, polepole, Meko na wengine toka juzi..

Wagombea wote wapo chini ya udhamini wa vyama..

Vyama vikishajitoa maana yake wagombea automatically wamekosa uhalali.
 
Ni wazi kuwa katiba hairuhusu wagombea binafsi hivyo wagombea ambao vyama vyao vilivyowadhamini vimejitoa wamekosa sifa kugombea.

Waziri Jafo na chama chako mmevuruga uchaguzi kwa nia ya kutaka kujipa ya ile idadi kubwa ya wapigakura mliyoiandikisha kuwa yote inaipenda CCM!

Kinachoonekana sasa ni jibu la kwanini mlilazimisha ipatikane idadi mkubwa ya wapigakura na hats kutishia kuwachukulia adhabu viongozi ambao maeneo yao yatashindwa kuandikisha watu wengi, hapa mlitegemea ushindi zaidi ya uchaguzi uliopita wa Rais.
 
Back
Top Bottom