Elisha Sarikiel
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 905
- 1,540
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe, Selemani Jafo amesema ndani ya miaka mitatu ijayo matamanio yake ni kuona Halmashauri zinajitegemea zenyewe kupitia mapato ya ndani na kwamba ifike muda ziwe zinalipa watumishi wake mishahara.
“Nikiangalia hoteli kubwa ilivyo kuwa mjini ya ghorofa 11 nikiangalia soko lenu la Dodoma nikiangalia eneo la maegesho ya magari Nala, eneo la mapumziko na michezo Chinangali, Stendi ya Dodoma, ninapata uhakika kwamba halmashauri ya jiji la Dodoma inaenda kujitegemea,”.
Mheshimiwa Waziri Jafo ameonyesha matamanio hayo leo wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Government City Complex katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 59.3 hadi kukamilika kwake ambapo ametumia nafasi hiyo kulipongeza jiji la Dodoma kwa kutekeleza kwa kutumia mapato yake ya ndani na si fedha za serikali.
Pia alisisitiza “Hakuna halmashauri yoyote iliyofanya uwekezaji mkubwa kama huu hivyo nawapongeza jiji la Dodoma, nataka jengo hili liwe kielelezo na kama nilivyosema mimi matamanio yangu nataka nione halmashauri zinazoweza kujitegeme zenyewe ifike muda halmashauri iseme hata nikiwa na watumishi wangu nitawalipa mimi mwenyewe natamani itokee ndani ya miaka mitatu ijayo,” amesema Waziri Jafo.
Jiji kuwa na majengo yatakayotoa huduma mbalimbali kama malazi, vyakula, makazi, Ofisi na kumbi za mikutano:-
1. Jengo la hoteli ya kisasa itakayokuwa na ghorofa 11 na vyumba 117 katikati ya jiji ni "Dodoma City Hotel'’.
2. Jengo lenye ghorofa pacha jirani na viwanja vya Nyerere litakalojulikana kama ‘'Nyerere Square Plaza'’.
3. Jengo la ‘Dodoma City Complex’ ni ghorofa nne, eneo la Dodoma Makulu Barabara ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma.
4. Mradi wa ‘Nunge Investment’ ni jengo la ghorofa 9, huku likiwa na migahawa mingi ya kisasa ndani yake”.
5. Jengo lingine la ‘Dodoma City Plaza’ katika eneo ambapo kuna ukumbi wa ‘NK’ Jijini humo.
6. Pentagon Tower la ghorofa 10 la kisasa katika jiji la Dodoma;linalotarajiwa kuwa chanzo cha mapato kama miradi mingine.
7. Mradi wa jengo la ‘Government City Complex’ ni kitega uchumi cha jiji la Dodoma uliopo mji wa serikali.
Tufahamu kuwa mji wa Serikali kwa upande wa magharibi unapakana na kambi ya Jeshi ya Ihumwa, Kaskazini-Mashariki unapakana na kata ya Mtumba na upande wa Kusini unapakana na barabara kuu iendayo Dar es salaam.

Pia fahamu miradi ya majengo makubwa inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma; kwa mapato ya ndani kwa kutazama video kupitia Youtube kwa kubofya link >>>