Members,Siri aliyoitoa Selemani Jaffo huko Arusha inafikirisha sana na kutoa picha halisi ya chama cha mapinduzi
Mosi,Kumbe watu wanakusanywa na kulazimishwa wajitokeze waonekane wengi wakati wa uzinduzi wa miradi na kampeni za ccm
Hili jambo la kukusanya watu wasiojielewa kama mifugo ili waje kupiga makofi uzinduzi wa barabara ya lami halina afya hata kidogo kwa mustakabali wa Taifa
Leo hii watu wengi wanafahamu ni kazi ya serikali kuweka lami na kujenga miundombinu ,hili sio ombi ni lazima kwa kuwa wanatuumiza kwenye kodi
Jambo baya zaidi unalazimisha watumishi wenye taaluma zao wakakusanye watu ili waje kukushangilia wewe na barabara ya lami
Pili,Watendaji wenye taaluma zao mfano engineers,Waganga wakuu wa hospital za wilaya na afya na wengine wanalazimishwa kujiingiza kwenye siasa kwa nguvu ili kusifu na kupiga makofi,Nini kosa la yule mtendaji wa serikali
Je?Yule mtendaji anayelazimishwa kukusanya watu Arusha na Selemani Jaffo alipewa pesa za mafuta na vipaza sauti ili ashawishi wananchi kuja kushangilia barabara ya lami
Kwa hili Jaffo kubali umekosea na omba msamaha watu watakusamehe,Kubali umeteleza
Yule mtumishi anayesimamia barabara Arusha hukutaka kumsikiliza uliona hoja zake zina mashiko ,Ulikuwa na hasira na frustration zako na mihemko isiyokuwa na maana kama Waziri
Selemani Jaffo ukiwa na hasira jaribu kunywa maji mengi na kutulia kwanza ,Ulevi wa madaraka ulioonyesha kwa mtumishi Arusha mwenye taaluma yake kumlazimisha akaswage watu kama mifugo halikubariki kabisa
Propaganda fanyeni nyie wana siasa,ccm Arusha ilikuwa wapi kukusanya hao watu waje kukushangilia wewe na barabara ya lami
Je Arusha hakuna katibu wa chama cha mapinduzi au Mwenyekiti wa ccm Arusha
Umetumia madaraka yako vibaya sana ,Watu walikuamini lakini sasa wanapata picha yako halisi kuwa wewe ni katili ,mpenda sifa na usiyetaka kusikiliza hoja za watumishi wa uma
Yule mtumishi aliyesimamia barabara Arusha kama engineer ulipasa kumsifu na kumpa hongera yake,Kitendo cha kumlazimisha engineer akatafute watu waje kukupigia makofi wewe na barabara ya lami ni aibu kubwa,Hata bosi wako hawezi kukubaliana na ulichokifanya Arusha kumuondoa mtumishi wa uma kisa hajatafuta watu wa kukupigia makofi wewe na kupigia makofi barabara ya lami