Waziri Jafo umekosea kulazimisha watu wenye taaluma kufanya kazi za propaganda

Sikutegemea wajitokeze watu wa kutetea alicho fanya waziri. Lakini watu ndivyo tulivyo.
Nilikuwa makini kuona mhandisi kakosea nini, sababu niliyoisikia nilishangaa.

Bora hizo hatua angemchukulia nje ya camera za waandishi. Bila shaka hata wana CCM wengi makini wamesikitika.
 
Jafo mwanza nilikuwa namkubali sana toka uchaguzi wa serikali za mitaa nikaona ni hopeless kabisa
 
CCM ya zamani ungeona anajitokeza hata kiongozi chamani akipinga ule uonevu. Shida ni CCM ya sasa, wao kazi yao ni kuunga mkono udhalimu wowote ule. Watapinga pale mwenyekiti akijitokeza kupinga tu.
Very pathetic
 
Kuna kipengele kinasema utafanya na kazi ingine ambayo utapangiwa na mwajiri wako,hicho kipo mpaka China utakikuta
Waliokitunga si wajinga,ndio maana wengine tumeamua kujiajiri tu
Alipangiwa kazi iyo na mwajiri wake?? Fichaga upumbavu wako ndugu
 
Alipangiwa kazi iyo na mwajiri wake?? Fichaga upumbavu wako ndugu
Mwisho wa siku ni weww na huyo jamaa yako mtaonekana wapumbavu kwa kung'ania kazi isioendana na taaluma
Kumshambulia Jaffo hakuwasaidii,mwambie jamaa yako aache kazi
 
Watu hujionyesha peupe wako vipi kwa matendo yao.

Aidha kumfurahisha bila aibu yule aliye mteua, hawa ndio boot lickers, au kufanya kazi kwa maadili yenye kuonyesha dhamana ya uongozi.

Jafo kapewa wizara ambayo vyatu ni vikubwa kwake.

Hatujasahau singeli aliyotoa na ku-rap mpaka mkandarasi SKOL akazimia kule Dodoma.

Leo kazi imefanyika kule Arusha sasa anataka kazi ikimalizika watu wa kusifu na kuabudu waitwe kumsifu hadharani.

Jafo hafai. Jafo kijana mdogo mwenye wake wanne nasikia, yeye weledi wa kazi hakuna, anaona sifa ni kumpa aliye mteua.

Wananchi wa Kisarawe tupeni mtu mwingine, huyu Jafo heri achukue nafasi ya Polepole kwenye chama.

Msimchague Jafo, mtu ambaye anaona heri punda afe, mzigo wa sifa za bwana zifike.
 
Ndio Tanzania hii.
Nakumbuka nikiwa form five Lindi secondary school, alikuja waziri mkuu Mizengo Pinda mkoa wa Lindi kwenye ghafla fulani. Headmaster alitupa Uhuru wa kwenda mjini viwanjani bila kuandika kwenye daftari la departure. Pia akatuambia tusivae uniform ilhali pale shule nguo za nyumbani ni marufuku hata kuzihifadhi kwenye tranka au begi.
Bwana weee tulitupia na kufurahi sana ile siku kumbe ilikuwa ni issue ya propaganda ya kumpamba waziri mkuu aone Lindi tunaipenda serikali .
CCM hii tabia ya kuzoa wanafunzi na watumishi kwenye ghafla hawajaanza leo
 
Mtanisamehe, ngoja nilisema kama mnatukana tukana! Nipige madongo yoyte mnataka. Mzaramo kazi anayoijua ni kucheza mdundiko. Sishangai Jafo kufanya ushenzi kama huu! sishangai katu! mtu ambaye hana mdundiko kichwani hawezi kum- victimise mwanadamu mwenzake kama alivyofanya kwa kijana wa TARURA! Shetani amlaani jafo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…