Waziri Jafo umekosea kulazimisha watu wenye taaluma kufanya kazi za propaganda

Hawa wanachaguliwa na tume ya uchaguzi na siyo wananchi
 
Huyu dogo nimemdharau Sana Kuna TISS mmoja aliniambiaga ni mmojawapo wa watu wanaofatiliwa au anaandaliwa kuteuliwa uraisi. Baadae yeye na lukuvi wako kwenye kapu moja wanapikwa lkn kwa tukio la Jana nimemdharau kabisa
Jafo ni dogo mtu alizaliwa 1973? basi sisi ni wachanga
 
Kuna kipengele kinasema utafanya na kazi ingine ambayo utapangiwa na mwajiri wako,hicho kipo mpaka China utakikuta
Waliokitunga si wajinga,ndio maana wengine tumeamua kujiajiri tu
Mkuu acha kujitoa ufahamu basi.
 
Viongozi wa Taifa hili ni hovyoooh tyuuh, hasa kutoka chama cha [emoji1637]
 
Nikiwa kada mkongwe nimesikitishwa sana na college mate wangu Jafo
 
Unajua hata mimi nilishangaa sana Waziri anamlaumu Mhandisi wa TARURA kuwa hajatimiza wajibu kuwaleta au kuwaalika wananchi washuhudie Uwekezaji Mkubwa wa Serikali Arusha. Sasa sijui Mhandisi ndiyo amekuwa Afisa Habari wa Arusha na viunga vyake. Yaani kwa maelezo yake anafikiri Mhandisi ni Mpinzani wa Juhudi za Serikali, wakati Mwamba ametimiza majukumu yake vizuri tuu.

Halafu anasema kabisa huyu hawezi kuongoza Jiji kama la Arusha mpelekeni Buhigwe au Kakonko huko(Kwa maana nyingine kumbe ukiwa huko Kakonko na Buhigwe ni kama ADHABU umepewa). Waziri anashindwa kujua kuwa watu ni waelewa juu ya Maendeleo na haihitaji kutumia nguvu kuuubwa kuyanadi.
 

kunywa maji alafu relax, alafu soma tena ulichoandika, then tafakari kwa makini, tumia medula sio tumbo mkuu utaelewa kuwa umekosea sana...ovaa
 
Mh. Jafo sio tu kachukua maamuzi ya ovyo na ya uonevu. Pia hajalitendea haki hili neno ' sabotage'
Nilimshangaa sn alipomuuliza "Wewe ni mpinzani? Unataka wananchi waseme Raisi hajafanya kitu huku Arusha? n.k". Ni aibu kubwa kulazimisha mioyo ya watu kufanya jambo wasilolipangilia. Kazi inaonekana hakuna haja ya kuforce watu kuimba mapambio. Waache kujitafutia riziki wakasimame barabarani? Aliwaandalia ujira? Jafo kajishusha kwa speed ya kutisha.
 
How far are you willing to kutetea madhaifu ya viongozi wa serikali? Inasikitisha kuona tuna wananch Aina yako!

Yan kuna mtu akiabdika kitu kumkadiria level ya elimu yake ni rahis sana aisee hivi mtu kweli anaona sawa yani ukiwa mtumish wa serikali ni mtumish wa CCM?
 
NI Ujinga Sana; Kama umefanya Kazi imeonekana inakuwaje Mpaka watu wawepo kwenye uzinduzi? Kama kazi imefanyika what i know ni kwamba Output inaongea; Huitaji Kutumia Nguvu Kubwa sana kuwaaminisha watu.

Suala kama Barabara inaonekana, hata watu wasipokuja watapita na wataifurahia tu; pasi na wao kuwepo kwenye uzinduzi. Sasa kweli Mtu aache shughuli za uzalishajai mali aende kwenye uzinduzi? Yeye Jffo ilikuwa ni sehemu yake ya Kazi, lakini wananchi wana kazi za uzalishaji mali mahalai pengine.

Duuh, nawaza hata kutokurudi mwaka huu; Maana Nchi yangu imekuwa na mambo ya Ajabu kweli kwenye Uongozi.
 
Kwani huo ulikuwa mkutano wa ccm!? Mwishoni mtawalazimisha wasomi kwenye vitengo wawe wanaanza na salamu ya "ccm hoyee" kwenye mikutano au hafla za uzinduzi wa miradi. Kama namuona vile Daktari wa Mkoa akiwasalimia wananchi kwa "ccm hoyee" kwenye uzinduzi wa wodi mpya.
 
Huyu jamaa sijawahi kuona utendaji wake zaidi ya maneno ya vitisho na kufokafoka , the way he talks unagudua tu anaigiza
 
Alitakiwa amkomalie Diwani wa Kata husika wala siyo Meneja wa TARURA hata kidogo.
Unaweza kukuta diwani alifanya kazi yake lakini alipoenda kwa meneja was TARURA kuhitaji fedha za kuandaa ubwabwa kwa wananchi (I mean wanaccm maana hao ni ubwabwa tuu) meneja akamtolea nje.
Ndio chanzo cha mgogoro
 
Viongozi wamepagawa ni mwendo wa sifà vifijo na nderemo ili wasitumbuliwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…