Pre GE2025 Waziri Jafo: Zaidi ya Viwanda 28,000 Vimejengwa Ndani ya Miaka 4 ya Rais Samia.Ampongeza Kwa Kuleta Mageuzi Makubwa ya Uwekezaji

Pre GE2025 Waziri Jafo: Zaidi ya Viwanda 28,000 Vimejengwa Ndani ya Miaka 4 ya Rais Samia.Ampongeza Kwa Kuleta Mageuzi Makubwa ya Uwekezaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Awamu ya Samia ndio imetafsiri maana halisi ya Tanzania ya viwanda na sio vi wonder kama kule tulikotoka. Pia soma Rais Samia anatafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo

========================
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko makubwa aliyoyafanya katika sekta ya viwanda nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha saruji cha Maweni Limestone mkoani Tanga leo Alhamisi Februari 27, 2025, Dkt. Jafo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2019-2021, Tanzania ilikuwa na viwanda takribani 52,000, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia, idadi ya viwanda imeongezeka na kufikia viwanda 80,179.

Nawakumbusha tuu kwamba sera ya Kufungua Nchi inalipa na imeleta majibu .👇👇

========================

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko makubwa aliyoyafanya katika sekta ya viwanda nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha saruji cha Maweni Limestone mkoani Tanga leo Alhamisi Februari 27, 2025, Dkt. Jafo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2019-2021, Tanzania ilikuwa na viwanda takribani 52,000, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia, idadi ya viwanda imeongezeka na kufikia viwanda 80,179.

Dkt. Jafo ameeleza kuwa, mabadiliko haya ni matokeo ya juhudi za Rais Samia, ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kutafuta na kuvutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani, na kuifanya Tanzania kuwa eneo salama la uwekezaji.

Ameongeza kuwa, hatua hizo za Rais Samia zimepanua fursa ya ajira kwa vijana wa Kitanzania, jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

“Rais Samia, umefanya mabadiliko makubwa katika sekta ya viwanda, na takwimu zinaonesha wazi kuwa idadi ya viwanda nchini imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Huu ni ushahidi wa juhudi zako za kuhakikisha kuwa sekta binafsi, viwanda, na biashara zinakuwa ndio lango kuu la kuajiri vijana na watu wengi,” alisema Dkt. Jafo.

Kwa upande mwingine, Dkt. Jafo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya viwanda kama njia mojawapo ya kupunguza tatizo la ajira nchini, huku akielezea jinsi viwanda vinavyosaidia katika kuajiri vijana na kutoa fursa za kimaisha kwa wananchi.
 
🚮🚮🚮🚮

Kwa hiyo Kila kijana ana sifa za kufanya kazi kiwandani?

Akili kizibo,viwanda vingi ni Capital intensive na sio Labour intensive wewe kubwa la manyumbu 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFfnc09oQaI/?igsh=dGl0NXZuOHUwcnVh

Kwani viwanja haviajiri HR? Haviajiri watu wa mazingira? Haviajiri wahasibu? Au unadhani ni watu wa vocational education tu wanaoajiriwa viwandani?

Kuwa na akili japo kidogo tu!

Pimaga hata taarifa kabla ya kuileta humu.
 
Back
Top Bottom