Pre GE2025 Waziri Jafo: Zaidi ya Viwanda 28,000 Vimejengwa Ndani ya Miaka 4 ya Rais Samia.Ampongeza Kwa Kuleta Mageuzi Makubwa ya Uwekezaji

Pre GE2025 Waziri Jafo: Zaidi ya Viwanda 28,000 Vimejengwa Ndani ya Miaka 4 ya Rais Samia.Ampongeza Kwa Kuleta Mageuzi Makubwa ya Uwekezaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Awamu ya Samia ndio imetafsiri maana halisi ya Tanzania ya viwanda na sio vi wonder kama kule tulikotoka. Pia soma Rais Samia anatafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo
========================
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko makubwa aliyoyafanya katika sekta ya viwanda nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha saruji cha Maweni Limestone mkoani Tanga leo Alhamisi Februari 27, 2025, Dkt. Jafo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2019-2021, Tanzania ilikuwa na viwanda takribani 52,000, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia, idadi ya viwanda imeongezeka na kufikia viwanda 80,179.

Nawakumbusha tuu kwamba sera ya Kufungua Nchi inalipa na imeleta majibu .👇👇
😂😂😂Nimecheka kwa nguvu kinoma. Eti viwanda elfu 30, yaani vingi kuliko China.
 
Kwani viwanja haviajiri HR? Haviajiri watu wa mazingira? Haviajiri wahasibu? Au unadhani ni watu wa vocational education tu wanaoajiriwa viwandani?

Kuwa na akili japo kidogo tu!

Pimaga hata taarifa kabla ya kuileta humu.
Ni utapeli tu hakuna hata kiwanda kimoja
 
Aisee hili taifa hili daaah. Majizi ccm ni laana kwa watanzania kama huyu mleta uzi sjui hata aibu haoni hv kweli tz imejenga viwanda elfu 30 vko wp na vnatengeneza nn na nn jamani au vina produce machawa maana sielewi huyu punguwani naye humu analeta takwimu za kizwazwa ili tukubali kweli taifa hli limejenga viwanda elfu 30 chn ya mama abdul wkt hata kiwanda cha soksi, sindano, stick hakuna sa hvyo ni vyann au ni vya magari.

View: https://x.com/InvestTanzania/status/1897354617908015117?t=gKyGcER2N9b6bEEKPbtJqg&s=19
 
Back
Top Bottom