SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Mvua ndiyo hizo tayari,swali la nyongeza tafadhaliWaziri siku ya Jumatatu ulitoa tamko na kutuahidi watanzania kuwa baada ya siku mbili utakuja na suluhu ya tatizo la umeme na ukame unaoikabili nchi yetu kwa sasa.
Waziri leo ni Jumamosi lakini tunaona uko kimya wala huna habari kabisa na umesahau kama ulitoa ahadi ya kutupatia muujiza ndani ya wiki hii...
Waziri watanzania hawajasahau maana tatizo la ukame na umeme bado lipo hivyo tunaomba utupatie huo muujiza utakao kuwa suluhu kama ulivyo ahidi...
Mh waziri kama itakupendeza kwa niaba ya watanzania naomba nikuongezee siku mbili zingine ili ikiwezekana kama sio jumatatu au jumanne utupatie huo muujiza utakao kuwa suluhu la haya matatizo ya ukame na umeme.
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app