Pre GE2025 Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alichofanya Mhe. Mhagama ni kitendo ambacho kinahesabila Ni heshima kubwa kwenye Jamii ya Wangoni huko Peramiho na Ruvuma.
 

Attachments

  • Snapinsta.app_461054338_545471604565975_8071883766470126917_n_1080.jpg
    167.8 KB · Views: 5
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama amegalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.

Chanzo: mwananchi_official

Yaani huko Kugalagala Kwako kote ni Kujipendekeza Kwake ili akuone uko nae na asiwaze Kukutumbua? SS Haaminiki.
 
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.

Picha na Edwin Mjwahuzi


 
Kama Waziri anaweza kufanya mambo ya aibu hivi mchana! Je gizani anaweza kufanya nini aendelee kuwa Waziri?!
 
Kitu Kinachonitia Hofu sana Ni kwamba Huyo Ndiyo Mshauri wa Rais kwa Upande wa Afya..

Ni vigumu sana Kushauri kitu kwa Kutilia Mkazo kama Atatishiwa au Kukataliwa Mawazo yake..

Napata Hofu sana..

Eeh Mungu wangu Chama changu Kinaenda wapi?😭😭

Najua Kuwa Siwezi kuhama Kwenda Upinzani, Chadema au ACT ila Naumia Nikiyaona haya..

Kwa Uchungu kabisa..
CC:- Tlaatlaah
 
Kajiandaa kabisa na gauni la vumbi
 
Dokta umeadimika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…