DPN
Member
- Sep 28, 2020
- 97
- 180
Kugalagala hivyo kwa watu wa Ruvuma (wangoni); wao wanasema KUGALAUKA, ni ishara ya kuonesha furaha isiyo kifani au shukrani ya kiwango cha juu sana kwa jambo linalotendeka kwa mhusika/ wahusika.Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.
My jicho ......
Tuseme kwamba huu ni uchawa au ni udhaifu kwa kiongozi kuonyesha kitu kama hichi kwani alishindwa kushukuru kawaida hadi kufanya alichokifanya binafsi natafsiri ni ushamba wa maarifa. Ifike mahali hawa viongozi wafanye mambo yao kwa uwelidi na sio kuongozwa na mihemuko fulani.
Soma Pia: Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara
Ni sehemu ya mila na desturi za wenyeji wa huko; siyo uchawi wala uchawa; tembea uone.
Kila kabila lina mila na desturi zake.
Kwa mfano; kwa jamii ya Wachagga mtu anapoomba msamaha kwa mwenzake, huwa anakwenda kuomba msamaha akiwa jani la mmea uitwao SALE kwa anayemwomba msamaha.
Akifika kwa anayemwomba msamaha, huweka mmea huo mbele yake, huku mkosaji akiomba msamaha.
Mara nyingi msamaha hutolewa; japo wengine hupuuza mila hiyo na ubaya ubwela huendelea!!