Waziri Jenister Mhagama: Tumebaini Uwepo wa Cake, Juisi na Biskuti Zenye Bangi

Waziri Jenister Mhagama: Tumebaini Uwepo wa Cake, Juisi na Biskuti Zenye Bangi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Watumiaji wa bangi nchini Tanzania wameibuka na mbinu mpya ya kuchanganya kilevi hicho na vyakula mbalimbali kama vile majani ya chai, keki, biskuti, juisi pamoja na asali.

Kutokana na hilo serikali kupitia kwa Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Jenista Mhagama akiwasilisha taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2022, amesema serikali imeanza operesheni nchi nzima kwenye viwanda vinavyozalisha biskuti na bidhaa nyingine za vyakula.

"Kuna dada Arusha yeye na mume wake raia wa kigeni tulikuta wanatengeneza bidhaa zikiwemo biskuti, keki na asali zote zikiwa zimewekwa bangi kwa asilimia kubwa na zikiwa zimeshafungwa kwaajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi" ameongeza Waziri Jenista.

FxZe0rGWIAMEUCz.jpg
FxZe026X0AAEhUt.jpg
FxZewUEXsAAk09z.jpg
 
Bangi hizo za kwenye biskuti na asali haziendi kuliwa au kuvutwa, zinakwenda kwenye viwanda vya madawa ya Binadam yenye "extracts" za bangi.

Bangi iruhusiwe tu iwe inalimwa kwa uhuru na isafirishwe kihalali, ina faida kubwa sana kuliko madhara.

Sigara na pombe zina madhara zaidi ya bangi.
 
Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la leo 31/5/2023, imedhahadharishwa kwa walaji wa vyakula tajwa kupunguza ulaji wake kwani imebainika bidhaa hizo zinatiwa bangi ndani yake. Lengo hasa la watengenezaji bidhaa hizi kutia bangi ndani yake ni kuwajengea wateja uraibu ili kuongeza mauzo kwa kuwa wateja wakishakuwa waraibu watakuwa wana hamu ya kununua kila siku. Ikipita siku mtu hajala keki, biskuti chocolate au majani ya chai atakuwa anajisikia kuwa na uraibu mkubwa hadi atakapoipata bidhaa husika.

MAONI YANGU
Naishauri serikali ichukue tahadhari kukomesha vitendo hivi kwa kuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa zinamowekwa bangi ni watoto wadogo. Tusipokuwa makini tutakuwa tunakuza kizazi cha mateja. Miaka michache ijayo taifa litakuwa limejaa waraibu kila kona.

Niliwahi kupata tetesi kuwa akina mamalishe wanaouza maandazi, chapati, kacholi na mihogo kwenye maeneo ya shule za msingi nao hutia dawa za kulevya kwenye vyakula ili kuwajengea wanafunzi uraibu. Ikiwa tutaenda namna hii bila kuchukua hatua za kukomesha vitendo hivi viouvu taifa lijalo litakuwa la walevi, mateja na waraibu. Tunapaswa kuziba ufa kabla ya kujenga ukuta.

Chanzo: Wasafi FM kipindi cha mapitio ya magazeti.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom