Watumiaji wa bangi nchini Tanzania wameibuka na mbinu mpya ya kuchanganya kilevi hicho na vyakula mbalimbali kama vile majani ya chai, keki, biskuti, juisi pamoja na asali.
Kutokana na hilo serikali kupitia kwa Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Jenista Mhagama akiwasilisha taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2022, amesema serikali imeanza operesheni nchi nzima kwenye viwanda vinavyozalisha biskuti na bidhaa nyingine za vyakula.
"Kuna dada Arusha yeye na mume wake raia wa kigeni tulikuta wanatengeneza bidhaa zikiwemo biskuti, keki na asali zote zikiwa zimewekwa bangi kwa asilimia kubwa na zikiwa zimeshafungwa kwaajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi" ameongeza Waziri Jenista.
View attachment 2640961View attachment 2640962View attachment 2640964