Waziri Jenister Mhagama: Tumebaini Uwepo wa Cake, Juisi na Biskuti Zenye Bangi

Waziri Jenister Mhagama: Tumebaini Uwepo wa Cake, Juisi na Biskuti Zenye Bangi

Kama ikitokea siku Nina hamu ya chai, ambayo ni nadra mno kwangu basi natumia herbal tea kama ya mchaichai ambao nimeupanda nyumbani ili kufukuza mbu
 
Kuna soda kampuni fulani nilizoea kunywa ilikuwa ikifika muda ninaokunywaga nguvu mwilini zinaisha/kama sijala kwa siku mbili
Baada ya hali hiyo niliamua kupunguza mpaka sasa hali hiyo haipo.
Nadhani hata kwenye soda hasa zenye gesi hayo madawa yapo. Hii dunia ni ngumu sana
Upo Sawa kabisa. Nahisi ulitumia Energy Drink mojawapo kati ya zile nyingi zilizopo sokoni. Vinywaji hivi, ambayo ni vya kuongeza nguvu, hujenga uraibu .
 
Hamna bangi ya kuchezea hivyo sisi wavutaji ndio tunajua labda kama Kuna some sorts of chemicals ila sio ganja kama ganja we kiwanda kizima kichakate biscuit za cannabis Hilo swala ni gumu acheni kutishia watu
 
Achana na hizo keki mkuu.....ni hatari.....kula vyakula vya asili.
Mkuu itabidi niache......vingine vyote vilivyotajwa hapo situmii ila hapo kwenye keki ndo waliponikea bangi! Binadamu tuna tamaa za ajabu. Kisa pesa tunawekeana bangi kwenye vyakula
 
Bangi hizo za kwenye biskuti na asali haziendi kuliwa au kuvutwa, zinakwenda kwenye viwanda vya madawa ya Binadam yenye "extracts" za bangi.

Bangi iruhusiwe tu iwe inalimwa kwa uhuru na isafirishwe kihalali, ina faida kubwa sana kuliko madhara.

Sigara na pombe zina madhara zaidi ya bangi.
Ndio maana nakupenda bibie...😘
 
Bangi hizo za kwenye biskuti na asali haziendi kuliwa au kuvutwa, zinakwenda kwenye viwanda vya madawa ya Binadam yenye "extracts" za bangi.

Bangi iruhusiwe tu iwe inalimwa kwa uhuru na isafirishwe kihalali, ina faida kubwa sana kuliko madhara.

Sigara na pombe zina madhara zaidi ya bangi.
Mwandisi katika sigara nakukubalia kabisa kwa sababu kumtibu mtu aliyaathirika kwa kansa ya tumbaku ni balaa miaka zaidi ya 10 ilikuwa inagharimu zaidi ya 6,000,000 sasa sijui kwa sasa.
ila kwenye pombe kwakweli watuache tu tupambane na hali yetu kwanza inakuza pato la ndani kwa kodi zake na inatoa ajira kwa watu wengi zisizo rasmi na chache rasmi.
 
Watu wanachangia bila hata kujiridhisha. Je bangi inalewesha Kwa kuliwa au kunywa au kuvuta. Siyo Kila habari ni ya kuaamini
 
Mbna tumekulaa sanaaaa.
Kwani haina madharaaa.
 
Mwandisi katika sigara nakukubalia kabisa kwa sababu kumtibu mtu aliyaathirika kwa kansa ya tumbaku ni balaa miaka zaidi ya 10 ilikuwa inagharimu zaidi ya 6,000,000 sasa sijui kwa sasa.
ila kwenye pombe kwakweli watuache tu tupambane na hali yetu kwanza inakuza pato la ndani kwa kodi zake na inatoa ajira kwa watu wengi zisizo rasmi na chache rasmi.
Takwimu za USA zinaonesha vifo vinavyosababishwa na ulevi ni vingi sana.

Hapa kwetu utakuta ni hivyo hivyo tu sema hatuna takwimu za kutosha.

Mimi naamini ajali nyingi za Magari Tanzania zinasabishwa na ulevi.
 
WATU WENGI WALIOZUNGUMZA KUHUSU BANGI KWENYE HII MADA MMELETA STORY ZA VIJIWENI ILA BANGI IPO TOFAUTI NA MNAVYO FIKIRI
 
Back
Top Bottom