Waziri Jenister Mhagama: Tumebaini Uwepo wa Cake, Juisi na Biskuti Zenye Bangi

Mbona hamkutoa taarifa.
 
Ni kampuni kubwa tu mkuu watu wengi wanaipenda sana
 
Hata hizo soda na juisi ambazo vijana wetu wanapenda kunywa zina madhara makubwa zaidi ya bangi. Ni afadhali kunywa gongo kuliko kunywa vinywaji hvi. Vina madhara makubwa sana mwilini.
 
Ni kampuni kubwa tu mkuu watu wengi wanaipenda sana
Basi kama ni hiyo inajulikana, hakuna haja ya kuitaja. Wanajifanya waislamu safi kumbe wauaji wakubwa! Serikali inapaswa kuwachukulia hatua wapuuzi hawa.
 
Watu wanachangia bila hata kujiridhisha. Je bangi inalewesha Kwa kuliwa au kunywa au kuvuta. Siyo Kila habari ni ya kuaamini
Wewe unadhani waziri amekurupuka kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uwepo wa bangi kwenye vyakula tajwa? Haya, wewe tuambie unachofahmu kuhusiana na sakata hili.
 
Ni hatari. Wengi watakuwa wamekula bila kujua. Mimi situmii vitu hivyo miaka mingi sana
Wewe unadhani wenye viwanda wataongeza gharama na risk ya kukamatwa kwa kuweka bangi kwenye kila biskuti? Ili iwasaidie nini sasa? Hapa huyu waziri hakuelezea yote na ameacha hivyo makusudi ili aonekane amefanya kazi kubwa ya kuokoa taifa isiangamie. Wanaoweka bangi watakuwa vi wenye viwanda wenye order special na bila shaka hata biskuti zake zitakuwa na bei na faida zaidi.
 
Mkuu itabidi niache......vingine vyote vilivyotajwa hapo situmii ila hapo kwenye keki ndo waliponikea bangi! Binadamu tuna tamaa za ajabu. Kisa pesa tunawekeana bangi kwenye vyakula
Lengo lao ni kukufanya uwe teja ili uwe unanunua kila siku. Ni mbinu mojawapo ya kupanua soko la bidhaa.
 
Upewe maua yako
 
Mmh kwamba bangi ni depressant drug kwamba inakufanya unanyongea na kukosa nguvu?really???
 
wamesikia wapi kuwa bangi ina uraibu,waache kupotosha watu
 
Kibibi, leo umenikosha sana. Ungekua karibu ningekupa mabusu kadhaa!
 
Wauza mayai na karanga barabarani wawekwe mstari wa mbele kabisa pamoja na energy drinnk
 
Eti jamani! Kila siku inasemwa halafu hakuna muafaka unaofikiwa nini kifanyike kuihusu nayo haikomi ipo tu
Muafaka ni wewe mwenyewe uache kutumia hizo bidhaa ili kuepuka kujiingiza kwenye ulevi na uraibu. Kama ilivyo kwenye sigara, watengenezaji wanakuambia kabisa UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO. Ni juu yako kuamua kuacha kuvuta au uvute at your own risk bila kumlaumu mtu yeyote kwa kuwa umepewa tahadhari mapema.
 
Sigara ina nicotine ambayo ndio inaleta uraibu,bangi haina uraibu jamani mjielimishe maana ya uraibu
 
Bangi ilifaa ichanganywe na vitu vichachu vichachu na siyo vitamu kama biskuti na asali.
[emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…